Timu za mkoani huwa zinakera sana ila basi tu!

Timu za mkoani huwa zinakera sana ila basi tu!

Marefa pia wanachangia kuzikandamiza timu za mkoani.

Goli la Max Nzengeli lingefungwa na Ihefu refa asingelikubali.

Goli halari la Obrey ,Chirwa alilowafunga Yanga, lingefungwa na Yanga Refa angelikubali.

Marefa ama wanahongwa au wanaziogopa timu za Simba na Yanga.
Inawezekana wanawaogopa mashabiki wao au wao pia wanazipenda hizo timu.

Ukiangalia hata maswala ya faulo, timu ya Yanga inafanya faulo nyingi sana lakini zinapiuziwa na Waamuzi. hasa mabeki wake.

Mfano Goli alilofunga KI AZIZ dhidi ya Ihefu Beki wa Ihefu alifanyiwa rafu mbaya hadi akaanguka na Azizi Ki kabla ya kufunga goli.

Penati nyingi wanapewa Simba na Yanga. Sikumbuki ni lini Penati ilitolewa dhidi ya Simba au Yanga.
Sasa mzee watu golini hawafiki unawapaje penalt??

Mpira hawakai nao ni butu butu tu, hizo fauls wanazipataje??

Ni kweli marefa wanazingua ila sio kwa asilimia kubwa kiasi kwamba waamue mechi zote 60 za simba + yanga.

Yanga kawapiga watu tano tano, tatu, nne hizo zote ni penalty na kubebwa na refa??

Uwezo wa timu za mikoni ni mdogo sana zikokutana na hizi timu mbili.
Jana game ilikua wazi kabisa yeyote anashinda ila mashujaa hata langoni kwa simba hawafiki, wanabutua tu na kukazana kuzuia.
 
Changamoto ni wachezaji wazawa level yao ya kujitambua ipo chini mno

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Sijui kwanini timu za mkoani zinapenda sana kutoka sare!

Yaani neno ushindi kwao ni msamiati ambao haujazoeleka

Hebu angalia mfano mechi ya jana ya yanga dhidi ya geita! Yanga form ilikuwa ipo chini mno yaani geita wangekuwa wana uchu wa ushindi wangeshinda mechi ya jana.

Angalia mfano wa pili wa mechi ya leo ya simba na mashujaa. Simba walikuwa wanaruka ruka uwanjani lakini mwisho wa siku wanapata matokeo kwa mazingira ambayo kama ingekuwa timu inayojua kutumia nafasi basi leo ingeibuka na ushindi

Timu za mkoani haziamini kama simba na yanga zinafungika wakicheza nazo utaona kabisa wanatafuta angalau droo au wafungwe goli chache spirit yao ya upambanaji inakuwa ipo chini mno.

Kwa kifupi wajitafakari kwa kuwa tunaongalia hizi mechi tumelipia ili tuone burudani ila mwisho wa siku tunakereka na mechi zinazochezwa upande mmoja.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Njaa baba
 
Back
Top Bottom