Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Sasa mzee watu golini hawafiki unawapaje penalt??Marefa pia wanachangia kuzikandamiza timu za mkoani.
Goli la Max Nzengeli lingefungwa na Ihefu refa asingelikubali.
Goli halari la Obrey ,Chirwa alilowafunga Yanga, lingefungwa na Yanga Refa angelikubali.
Marefa ama wanahongwa au wanaziogopa timu za Simba na Yanga.
Inawezekana wanawaogopa mashabiki wao au wao pia wanazipenda hizo timu.
Ukiangalia hata maswala ya faulo, timu ya Yanga inafanya faulo nyingi sana lakini zinapiuziwa na Waamuzi. hasa mabeki wake.
Mfano Goli alilofunga KI AZIZ dhidi ya Ihefu Beki wa Ihefu alifanyiwa rafu mbaya hadi akaanguka na Azizi Ki kabla ya kufunga goli.
Penati nyingi wanapewa Simba na Yanga. Sikumbuki ni lini Penati ilitolewa dhidi ya Simba au Yanga.
Mpira hawakai nao ni butu butu tu, hizo fauls wanazipataje??
Ni kweli marefa wanazingua ila sio kwa asilimia kubwa kiasi kwamba waamue mechi zote 60 za simba + yanga.
Yanga kawapiga watu tano tano, tatu, nne hizo zote ni penalty na kubebwa na refa??
Uwezo wa timu za mikoni ni mdogo sana zikokutana na hizi timu mbili.
Jana game ilikua wazi kabisa yeyote anashinda ila mashujaa hata langoni kwa simba hawafiki, wanabutua tu na kukazana kuzuia.