Timu za Tanzania tuna cha kujifunza kwenye upigaji wa penati

Timu za Tanzania tuna cha kujifunza kwenye upigaji wa penati

Pamoja na yanga kufanyiwa mtimanyongo kwenye goli la Aziz Ki,

Lazima tukubali kuwa timu zetu za Tanzania zina udhaifu mkubwa kwenye upigaji penati.

Inafika hatua, tukifika kwenye mikwaju ya penati tunahesabu kuwa tumeshatolewa tayari na mara nyingi tunashinda pale ambapo kipa atasave mikwaju mingi ya penati (kuanzia 3) na hapa ndio maana Ally Salim na Diara huwa wanaimbwa sana endapo timu zao zikishinda kwa penati

Bado tunaishi na slogan ya kuwa " PENATI HAZINA MBABE" ila sio kweli penati zina wababe.

Angalia zile penati tatu za wachezaji wa Mamelody, penati zimepigwa kiufundi kiasi kwamba kipa yoyote hawezi kudaka na akidaka basi lazima ateguke mgongo.

NB
Nazungumzia zaidi Simba na yanga maana mashindano ya klabu bingwa sometimes si rahisi kupata matokeo ndani ya dakika 90 au 180 na hapo mshindi analazimika kupatikana kwa mikwaju ya penati

Yes, tuna maumivu ila kuna haja ya benchi la ufundi kulifanyia kazi eneo hili.
wanakuja kukubishia
hatujui kupiga penati isitoshe hata wachezaji wetu wa kigeni nao walewale. sijui ndio yale ukikaa na mwehu unakua mwehu
 
nawashauri Yanga, wajitahidi kusajili wachezaji wengine wenye uwezo mzuri wa kufunga, aina za mayele, pacome yupo ila akipata shida hakuna mbadala. mechi zote mbili kama hawa pacome na kama tungekuwa na wafungaji, sundowns walikuwa wanafungwa magoli hata zaidi ya mawili. aziz ki hata lile goli hakutakiwa kupiga vile, angekuwa pacome lilikuwa goli lile. angalia magoli aliyokosa mzize kwenye mechi zote mbili, na wengine, utaona kuna pengo la wafungaji. kwenye ulinzi, yanga wapo vizuri,wala wasiongeze mwingine.
mtumishi umetisha umecharaza ukweli
 
Kwani mama Kubwa, ulivyoona wewe lile shuti la Aziz Ki mpira uliingia ndani kwa asilimia 100 au lah? Kama mpira ulikuwa ni goli basi Yanga na Mamelod wamelazimisha ionekane ni nguvu sawa wakati kiuhalisia Yanga alishaizidi Mamelodi kwa kumfunga goli moja
Umejibu kistaarabu ngoja nikupe mfano. Kati ya Mwaka 91 au 92 Kenya walifanya Uchaguzi kuna vyama viwili nilikuwa vinachuana Sana mpaka dakika ya mwisho wakati wanatangaza wakaipa ushindi Chama tawala. Damu ilimwagika Hadi wakaunda Serikali ya umoja WA Kitaifa Kiongozi mmoja WA upinzani aliwaambia wafuasi wake kuwa imekuwa rahisi kuporwa Kwa sababu ya TOFAUTI ndogo ya kura. Maana yangu Yanga ingewashindilia goli nyingi hata wangeiba wangejisumbua. kuhusu mstari Mie ni shabiki maandazi mambo ya Sheria nitasema uongo.
 
Jibu lako lipo hapa chini mama Mkubwa. Angalia hiyo video halafu linganisha na yaliyotokea kote kote. Halafu mbaya zaidi mnayajadili ya wenzenu huku mnasahau kuwa kwenye hatua hii nyie ndio timu pekee mliyofungwa kwa aggregate ya goli tatu kwa sifuri. View attachment 2956922
Kufungwa ni kufungwa Tu. Ingekuwa Yanga anaendelea na michuano tungemsifia Kwa kutofungwa.
 
Back
Top Bottom