Timu za watoto wa kihuni

Bogota Fc mashabiki wake wote wakabaji sugu Manzese makaburini,wakiongozwa na marehemu Ali Mapua.Uswahili watu wanapiga mpira bwana.
 

morogoro pale saba saba kulikuwa na timu moja sijui kama mpaka sasa ipo inaitwa saba saba united ambayo kocha wake alikuwa fundi amri ibrahim. sasa ukitaka uone vituko vya humu unaweza usiwe unaangalia kabisa komedy za akina masanja na vunja mbavu kwani nakumbuka kuna siku moja nilibahatika kuhudhuria mazoezi yao ambapo huyo kocha kabla tu ya kuanza kuwachezesha akajifanya anawaita wachezaji wote na kuwataka kucheza mpira wa kistaarabu kisha akaanzisha mpira na akawa anaenda kwa mabeki wa kila upande na kuwaambia kwa kujificha ficha kuwa wachezeeni rafu mafowadi ili wakomae na bahati nzuri hao mabeki wenyewe aliokuwa akiwaambia nadhani hata hayati bob marley angewaona walivyokuwa wakivuta bangi kuliko yeye angeamuru wanyongwe hivyo fowadi mmoja akajipendekeza ambapo alipigwa mguu wa shingo na akatoa sauti ya ( yalaa kocha! ) ambapo alisikika kocha amri ibrahim akisema ( mwongeze nyingine ) ambapo yule mchezaji aliyekuwa amegala gala aliamka upesi na haraka huku akiendelea na mazoezi kana kwamba hakuchezewa rafu ile mbaya. hiyo tisa kumi ni kwamba huyu kocha alikuwa hakupi namba katika kikosi chake kama huna kovu au pengo katika mwili wako na kama huchezi rafu mazoezini na yeye mchezaji wake akiwa anapata kadi sana katika mechi alikuwa akimpa hela kama zawadi. nakumbuka timu yoyote pale mkoani morogoro ikiwa inacheza na saba saba united basi lazima ambulances zitakuwa standby huku kitengo cha wagonjwa mahututi pale hospitali kuu ya mkoani morogoro madaktari wakiwa tayari tayari kupokea majeruhi. mnaomjua beki fikiri magoso ndiyo katokea hapo na kama mtu yoyote yupo nae karibu huko kwake sasa aishipo amwangalie vizuri kuanzia usoni mwake, mfumo mzima wa kimpangilio wa meno yake na miguu yake. matege makubwa na yaliyopinda ya fikiri magoso hayakutokana na uumbaji wa mwenyezi mungu bali ni aina ya rafu alizokuwa akichezewa na wenzake wa saba saba united wakiwa mazoezini wakati akiwa nao enzi hizo na ndiyo maana hadi akasajiliwa na reli enzi hizo na kuwa tishio kwa mafowadi wote nchini tanzania isipokuwa tu kwa msela mwenzie marehemu ( r.i.p ) said mwamba kizota a.k.a baba tosha ambaye walipokuwa wakikutana ilikuwa ni shughuli na huku watu wengi wakijifunza aina za rafu kutoka kwao. mpira wa kibongo bhana balaa tupu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…