Timu za watoto wa kihuni

Timu za watoto wa kihuni

Shughuli enzi hizo ilikuwa uwanja wa Barafu.
Kulikuwa na Entebe ya Shibam Magomeni, Kiboko Msheli ya Magomeni Makuti, Magomeni Kondoa, Kagera Rangers, Linea Messina, Nzige Army.
Ilikuwa ikipigwa mechi ya Entebe na Kagera Rangers au Messina Line, uwanja ulikuwa unabeba zaidi ya watu Elfu 8.
Wachezaji wengi wa kwenye Ligi kwenye miaka ya mwishoni mwa 1980 walitoka kwenye timu hizi.
Mfano; Bakari Iddi, Kingsley Malwilo,Muscat Said, Kasa Musa, Ally Maumba, Issa Athumani (marehemu) Kasongo Athumani nk.
Zamani kulikuwa na mpira bana, mechi ya Mchangani lakini kuanzia saa 8 mchana uwanja wa Barafu ushajaa, kusubiri vichekesho vya Mbamba wa Entebe, Ally Waya na mdogo wake Honda.
 
Yeah soka la mchangani lipo vizuri sana. Hivi Issa Athumani alizikiwa Sauzi au walimrudisha bongo?
 
Nadhani alizikwa Bongo, ingawa sina uhakika sana.
Enzi hizo refarii Mandemla, anachezesha akiwa Tumbo wazi na Kisu kiunoni na Mwenzake Tindo.
Kaka asikwambie mtu, zamani kulikuwa na mpira, na wachezaji wenye afya ya mpira na miili ya mpira, sio sasa hivi mchezaji ukimuangalia Damu 2 Maji 1.
 
Hanna KaMa kagera rangers n.a. friends rangers hawa majirani kinesi ilikua atari mwanzoni mwa 2000.

Pia kuna abajalo vs friends watemi kuna van dame wa abajalo n.a. Eli mzozo
 
Linea messina vs bomu ya ilala ngoma ilikuwa mwananyamala lake rangers,ngoma ilikuwa ngoma sikumbuki matokeo yalikuwaje ila ninachokumbuka ni Jinsi vurugu lililotokea bomu walikuwa na shabiki lao hilo full karate tulichezea kichapo
 
Orodha ya timu za mpira wa miguu za watoto wa kihuni pamoja na vituko vyao katika soka, premier league na mchangani, bila kusahau wana soka waliokuwa wanacheza soka la kihuni.

Mimi naanza na timu zangu...

1. NYOTA NYEKUNDU.
2. CONGO UNITED
3.SIFA UNITED watoto wa Tandale....
5. ASHANTI YA ILALA

4. Kuna watu wanaitaja na AFRICAN SPORT ya TANGA but sijalithibitisha hilo.

ONGEZA NYINGINE NA VITUKO VYAO KWENYE SOKA.

KISA KIMOJA : NYOTA NYEKUNDU walikuwa na beki wao anaitwa JOHN BOSCO ambae baadae alisajiliwa na Simba. Kabla hajasajiliwa Simba, Madaraka Suleiman mzee wa Kiminyio, alisajiliwa Majimaji ya Songea akitokea Sifa United ya Tandale.

Maji maji wakaja kucheza na Nyota Nyekundu uwanja wa taifa. John Bosco akawa ndo anamkaba Madaraka. John Bosco alimchezea sana rafu Madaraka, ila Madaraka akawa ana mkaushia tu. Kala sana vipepsi nakadhalika..

Game ilivyoisha Madaraka akamfuata John Bosco nje ya dimba. Akamwamkwida akimwambi:

" We msengwile unaniona mi fala eeh kwa sababu nachezea Majimaji? Unaniona mi mngoni?" John Bosco alichezea kichapo cha haja. Wachezaji wengine wa Nyota Nyekundu wakakaushia tu kwa sababu wanajuma madaraka mtoto wa SIFA UNITED ya Tandale na moto wa watoto wa SIFA UNITED walikuwa wanaujua."

Dondosha jina la timu yoyote iliyo kuwa inacheza mpira wa kihuni pamoja na vituko vyao.
Mkuu Sifa United ipo Manzese Mlimani sio Tandale
 
Waya Mkali ya Arusha..Ilikuwa timu ya majambazi,wakabaji na wababe wote wa Unga limited na ngarenaro.Kapteni wa timu ni marehemu King Kola mwenyewe.Hii ni mwisho
 
Shughuli enzi hizo ilikuwa uwanja wa Barafu.
Kulikuwa na Entebe ya Shibam Magomeni, Kiboko Msheli ya Magomeni Makuti, Magomeni Kondoa, Kagera Rangers, Linea Messina, Nzige Army.
Ilikuwa ikipigwa mechi ya Entebe na Kagera Rangers au Messina Line, uwanja ulikuwa unabeba zaidi ya watu Elfu 8.
Wachezaji wengi wa kwenye Ligi kwenye miaka ya mwishoni mwa 1980 walitoka kwenye timu hizi.
Mfano; Bakari Iddi, Kingsley Malwilo,Muscat Said, Kasa Musa, Ally Maumba, Issa Athumani (marehemu) Kasongo Athumani nk.
Zamani kulikuwa na mpira bana, mechi ya Mchangani lakini kuanzia saa 8 mchana uwanja wa Barafu ushajaa, kusubiri vichekesho vya Mbamba wa Entebe, Ally Waya na mdogo wake Honda.
Daaah mkuu umenikumbisha mbali sana na uwanja wa Barafu na kiboko msheli.. Enzi hizo home palikuwa hapo somanga gemu zikichezwa pakitokea tafran utashangaa watu wanavyokatiza makaburini pale kwa spidi ya ajabu…. Daaah those were the dayz
 
Bercelona ya mwanza na balewa fc ya nera achanao hao,pia Toto Africans in tim ya wahuni Julio anahabari nao
 
Umenikumbusha mbali Sana yamebaki majina tu kwasasa kidogo OPEC unaweza kusema IPO lakini zingine zote zimebaki majina
 
Bercelona ya mwanza na balewa fc ya nera achanao hao,pia Toto Africans in tim ya wahuni Julio anahabari nao

Barcelona ya pale Uhuru ilikuwa mixer wahindi, waswahili na waarabu watata..jamaa walikuwa wanapiga mpira safi saana wa Gonga yaani moja moja saafi wakanifanya niwapende na wakatalunya wa spain.

Duh!! Skoba, Said Mbuzi..kizazi jeuri hiki.
 
California FC ya Mabatini.. Opec ya Igogo.. Lumumba Rovers na AFC Lumumba. Hizi timu bado zipo?

Wazazi wa fonia wale..kuna beki yao moja inaitwa Kasanga ukiiona msuli wa mbu ila shughuli yake uwanjani ni dunia.. ilikuwa na makovu kila sehemu ya paja sababu ya kuslide kwenye ule uwanja wa mkavu wa Nyamagana...stopper yao iliitwa Madoa mwamba. Timu ikitaka kwenda uwanjani wachezaji na mashabiki wanaenda kwa mchakamchaka. Hatari!!

Machezaji yalikuwa long time.
 
Kuna timu moja ipo kigoma inaitwa WAYEGE FC inatokea sehemu moja inaitwa gungu... Ilitisha sana mwanzoni mwa miaka ya 2000... Wengi wa timu hii walikuwa ni wezi wa mafuta kwenye treni zinazosafirisha mafuta... Timu hii ndio katokea bakari kigodeko ambaye kwa sasa anakipiga chini ya JULIO...
WALIKUWA ni watu wa vurugu usipime
 
Barcelona ya pale Uhuru ilikuwa mixer wahindi, waswahili na waarabu watata..jamaa walikuwa wanapiga mpira safi saana wa Gonga yaani moja moja saafi wakanifanya niwapende na wakatalunya wa spain.

Duh!! Skoba, Said Mbuzi..kizazi jeuri hiki.
Bila kumsahau Aron Nyanda,ngasa pia alipita hapo kabla ya opec
 
Back
Top Bottom