Timu za watoto wa kihuni

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nyie watu mmenikumbusha mtaani kwetu kabisaaaa ! Kwa bi. Mtinge muuza vitumbua[emoji23] [emoji23] [emoji23]
sawa sawa kabisa
 
Nilichogundua kumbe masta wengi wa soka hapa bongo wengi wametokea timu za mchangani halafu za kihuni,kweli maisha yanabadilika
 
Shada Fc ya kinondoni shamba hii timu ilikua na wahuni balaa wanakuja na makopo ya mavi wanajimwagia siku timu yao ikicheza watoto tunakatazwa kwenda uwanjani those days uwanja wa Hananasif
 
Walikua na muhuni wao anaitwa Regan mwili mdogo anazunguka uwanjani mwanzo mwisho ule wako umguse umekwisha
 
Umenikumbusha mbali Sana yamebaki majina tu kwasasa kidogo OPEC unaweza kusema IPO lakini zingine zote zimebaki majina
Waazilishi wengi wa hizi timu wameshafariki Kutona na mambo ya anasa na ujana kwa mfano pombe, dawa za kulevya, hiv/aids na waliopo wengi wao ni watu wazima age ya 60s plus 70s
 
Hanna KaMa kagera rangers n.a. friends rangers hawa majirani kinesi ilikua atari mwanzoni mwa 2000.

Pia kuna abajalo vs friends watemi kuna van dame wa abajalo n.a. Eli mzozo
Huyu Van damme aliingia kwa chafu moja pale kwa Macheni alipigwa ngumi moja tu ndio ni ngumi moja bila ya nyongeza ikamtupa ndani ya Body ya pickup ugomvi ukaishia hapo.
 
Kuna chama maeneo ya Tandika Daresalaam linaitwa SIFA POLITANI.Ni balaaa,ndo alipotekea Seleman Mkati aliyesajiliwa Yanga,Juma mazoo aliyesajiliwa Reli Morogoro na Ibrahim ramadhan Ibingi aliesajiliwa Yanga....baba hili chama ni Nyoko kwa fujo uwanja wa MABATINI TANDIKA.na wapinzan wao au wahuni wenzao walikuwa timu inaitwa SOWETO FC na MZIZI FC za MTONI TAMBUKARELI DSM.mbali na Uhuni Hawa Wana Mpira Wanaujua.

Kitambo hicho MUSTAPHA HOZA beki ya Simba,baadae ikasajiliwa kariakoo Lindi alikuwa anacheza FURAHA FC Ya Tandika .Huku Obby Stereck Mwambungu aliekua anachezea GEREZANI FC ya kariakoo baadae akasajiliwa SIGARA FC, Na Beki Julius Mwakatika,alietokea SIFA POLITAN FC Ya TANDIKA
 
Kiboko Msheli
Tesema
 
Kule Ukerewe kulikuwa na timu inaitwa Majini Weusi! Yaani ukiwaroga ni kama umejiroga!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…