Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Timu za Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi zimeanza kwa kishindo katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa ushindi katika michezo mitatu kwenye mashindano hayo yanayoendelea mkoani Kilimanjaro.
Mafanikio hayo yamekuja kufuatia ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo kutembelea timu hiyo na kufanya kikao na watumishi wanaoshiriki katika michezo, ambapo alisisitiza kuiwakilisha Wizara vyema wakizingatia nidhamu na kujituma kwenye miche,o yote watakayocheza wakiongozwa na dhamira ya ushindi kwa kila mchezo.
Soma Pia: Ardhi FC yaianza shimiwi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ras Lindi
Katika mchezo wa mpira wa miguu, timu ya Ardhi FC imeanza vizuri baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya RAS Lindi. Ushindi huo umeipa timu hiyo mwanzo mzuri katika mashindano hayo huku ikionyesha dhamira ya kufanya vizuri katika michezo inayofuata.
Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba, timu ya wanawake ya Ardhi imepata ushindi wa 2-0 dhidi ya Wizara ya Mambo ya Nje, huku timu ya wanaume ya Ardhi nayo ikishinda kwa matokeo ya 2-0 dhidi ya RAS Singida jambo linalo ongeza matumaini kwa timu hizo katika kuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Katika mchezo wa mpira wa pete, timu ya Ardhi wanawake imeonyesha kiwango kizuri baada ya kuifunga RAS Njombe kwa magoli 41-2.
Matokeo hayo yanazifanya timu za Wizara ya Ardhi kuanza vyema mashindano ya SHIMIWI, huku wachezaji wakitarajiwa kuendelea kupambana katika michezo inayofuata na kuendeleza ushindi kwa ajili ya kuiwakilisha vyema Wizara yao.