Tetesi: Tip From Deep Inside: Uchunguzi wa Kesi 9 za Ufisadi Mkubwa Umekamilika.Soon Vigogo Kizimbani

Tetesi: Tip From Deep Inside: Uchunguzi wa Kesi 9 za Ufisadi Mkubwa Umekamilika.Soon Vigogo Kizimbani

tungefurahi mafisa wangepelekwa kwa issue zifuatazo. EPA,IPTL, RICHMOND, UUZAJI NYUMBA ZA SERIKALI, RADAR, MIKATABA YA MADINI nk.
 
Kuna vita gani hapa?
Serikali kumkamata mtuhumiwa mnnaminishwa ni vita?
Ama kweli hata umtwange mpumbavu kinuni Upumbavu haumtoki!!!
Mimi namaanisha vita dhidi ya ufisadi. Kutokuwa na macho maana yake, kusiwe na double standard.
 
Wanabodi.

Nimepokea tetesi from deep inside kuwa kuna kesi nyingine 8 za ufisadi ambazo uchunguzi umekamilika na sasa ziko mezani kwa DPP zikisubiri kibali cha kupelekwa mahakamani.

Hili ni bandiko la ile jf advantage, be the first to know kuwa baada ya James Rugemalila na Habinder Sing kupandishwa kizimbani, uchunguzi kuhusu kesi nyingine 8 za ufisadi mkubwa zimekamilika hivyo soon kuna Vigogo wengine wakubwa watapandishwa kizimbani.

Source: A reliable tip from deep inside!.

Hata hivyo source hiyo from deep inside haikusema kesi hizo nane ni kesi zipi za ufisadi upi na wala ni vigogo gani hao watakao pandishwa kizimbani, ni kina nani na wamefanya nini!.

Awali kulipandishwa uzi
TAKUKURU kwa sasa wanachunguza kashfa za RICHMOND, EPA na Rada ...
taarifa hii TAKUKURU, inazungumzia uchunguzi, taartifa ya source wangu, inasema uchunguzi umekamilika, kesi ziko mezani kwa DPP, zinasubiri tuu uamuzi wa DPP.

Naomba msiniulize lolote kuhusu hiyo reliable source from deep inside kwa mujibu wa kanuni ya kihabari iitwayo "the confidentiality of the source".

Umuhimu wa tip hii ni kukupatia tuu info wewe mwana jf be the first to know kwa kuwa wa kwanza kujua. Information is power, kitendo cha kujua kuna kesi kubwa 9 za ufisadi mkubwa ni power kubwa ya uthibitisho. kuwa serikali ya Magufuli iko very serious katika vita hii ya ufisadi na haitanii!.
My Take.
Msihamanike sana kudhania sasa ndio ile mikesi yote ya ufisadi mkubwa itaibuliwa. No. Kuna kesi za ufisadi za touchables na za untouchables. Zitakazo fikishwa mahakamani ni only za touchables, zile za untouchables zenyewe haziguswi!.

Pia kupandishwa kwa kesi mahakamani ni one thing thing, kushinda kesi is another na haki kutendeka is quite another thing!.
Mfano hai ni hii kesi ya kwanza kati ya hizo 9 iliyopandishwa mahakamani, serikali tayari imeishashi... kesi hata kabla kesi haijaanza kusikilizwa!.

Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.
Stay tuned.

Paskali
Ninachojua kwa uhakika ni kuwa ESCROW na ya RADA ndio tayari zipo zinasubiria mesenja azipeleke kwa pilato
 
Wanabodi.

Nimepokea tetesi from deep inside kuwa kuna kesi nyingine 8 za ufisadi ambazo uchunguzi umekamilika na sasa ziko mezani kwa DPP zikisubiri kibali cha kupelekwa mahakamani.

Hili ni bandiko la ile jf advantage, be the first to know kuwa baada ya James Rugemalila na Habinder Sing kupandishwa kizimbani, uchunguzi kuhusu kesi nyingine 8 za ufisadi mkubwa zimekamilika hivyo soon kuna Vigogo wengine wakubwa watapandishwa kizimbani.

Source: A reliable tip from deep inside!.

Hata hivyo source hiyo from deep inside haikusema kesi hizo nane ni kesi zipi za ufisadi upi na wala ni vigogo gani hao watakao pandishwa kizimbani, ni kina nani na wamefanya nini!.

....

My Take.
Msihamanike sana kudhania sasa ndio ile mikesi yote ya ufisadi mkubwa itaibuliwa. No. Kuna kesi za ufisadi za touchables na za untouchables. Zitakazo fikishwa mahakamani ni only za touchables, zile za untouchables zenyewe haziguswi!.

Pia kupandishwa kwa kesi mahakamani ni one thing thing, kushinda kesi is another na haki kutendeka is quite another thing!.

...

Paskali

Mkuu Paskali

Usipende sana kucheza na akili za Watanzania. Wenye hasira kali na mizengwe inayoendelea wapo. Labda heri angalau safari hii umetoa tahadhari za kutosha.

Ni mtu mjinga kweli kweli - mwenye IQ zero - ndiye anayeweza kuamini kwamba kuna utawala wa CCM wenye jeuri ya kuendesha kesi zote dhidi ya mafisadi kwa nia ya dhati bila kuangalia sura ya mtu.

Kwanza dili za kifisadi zote tunazozifahamu waidhinishaji wake wakuu walikuwa wenyeviti wa kitaifa wa CCM huku wahandisi wakuu wakiwa wanasheria na watendaji wakuu wa serikali. Wasiogusika. Sasa, atokee wapi huyo mwenye kibri ya kushikisha adabu mafisadi waliotumia madaraka yao kuhujumu taifa halafu wakawahi kujikinga kwa sheria ya kutoshitakiwa katika mazingira yoyote yale!

Kule tu kutotaka katiba irekebishwe ni kielelezo tosha cha hawa jamaa kupania kuendelea kuwa untouchables. Sie tuendelee kuangalia mazingaombwe ya makinikia ...
 
Mkuu Pasco!! ingawa haujagusia angalau moja ya hizo kesi 8, nafikiri na hii hapa chini ni moja wapo, isipokuwepo basi hakutakuwa na kesi bali maigizo.

Zitto amuanika Waziri wa Ujenzi Bwana Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni
  1. May 14, 2013
    Ndugai amekuwa mtetezi wa ufisadi bungeni. Ni baada ya kamanda Zitto Kabwe kumuanika Waziri wa Ujenzi Bwana Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni. Baada ya Zito kutoa hoja ya kutoa shilingi ya mshahara wa Magufuli, Ndugai akakurupuka kufunika hoja, eti kisa Zito ni Mwenyekit wa PAC. Safari bado ngumu.
    "Mwaka 2011 tulipohoji kifungu chenye Fedha tshs 252bn kwenye Wizara ya Ujenzi, Naibu Waziri Harrison Mwakyembe alijibu "hizi Ni Fedha za miradi maalumu ya barabara ambapo tukipata misaada ya wafadhili hizi ndio michango yetu Kwa miradi". Bunge likapitisha. Hazina ikatoa pesa zote kwenda Wizara ya Ujenzi.

    Mwaka huu tumehoji, hizi Fedha zilitumika namna gani? Waziri John Magufuli akasema "tulilipa Madeni".

    Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anasema kwenye taarifa yake "ilitengenezwa miradi hewa ya barabara yenye namba ya mradi hewa. Pia hakuna uthibitisho kuwa Madeni yalilipwa kwani hakuna nyaraka za kuonyesha malipo". Tumehoji kutaka majibu, tumepigwa chenga.

    Kweli? Tshs 252 bilioni hazina maelezo? Tutahakikisha Uwajibikaji katika hili"
    Agosti 24, 2013 - Mwananchi
    Tuhuma nzito: Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

    Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge.

    Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012.

    Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

    “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa kiasi cha Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

    Alisema katika majumuisho ya Bajeti ya wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Mwakyembe wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha.

    Alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.

    “Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara,” Zitto alisema akikariri maneno ya Dk Magufuli wakati anawasilisha bajeti.

    “Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Mwakyembe wakati akifanya majumuisho.

    “Hizi ni fedha kwa ajili ya counterpart fund,” alimkariri Lukuvi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.

    Zitto alisema CAG alihoji mwaka huu kuhusu matumizi ya fedha hizo na alitoa taarifa akidai kuwa fedha hizo zilikuwa miradi hewa na kasma kivuli.

    Zitto alisema kuwa Dk Magufuli na Katibu Mkuu wake walipohojiwa walidai kutumia fedha hizo kulipa madeni.

    “Kwa nini mlidanganya Bunge? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba fedha za madeni. Kwa nini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa kulipwa?” Zitto alimhoji Balozi Mrango.

    Katika majibu yake, Balozi Mrango alisema kwa nia njema, fedha hizo zilitumika kuwalipa makandarasi waliokuwa wamechachamaa, huku baadhi yao wakisisitiza kusitisha kuendelea na miradi. Hivyo wakalazimika kuomba fedha kwa njia hiyo ili miradi kuendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.

    Zitto hakuridhishwa na majibu hayo akisema hapakuwa na haja ya kutumia fedha hizo kuwalipa makandarasi wakati kulikuwa na kasma yao ya awali. Alisema kama kulikuwa na haja hiyo, wizara isingeita mradi rasmi.

    “Jambo hili siyo sahihi hata kidogo kulidanganya Bunge na hadi sasa wewe na waziri wako hamuonyeshi kukubali kosa hili, hata Waziri Lukuvi naye alisisitiza bungeni kwamba fedha hizo zinaombwa ili kutekeleza mradi maalumu lakini sasa imebainika sivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge tutawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ili wahojiwe nao wajieleze kwa kulidanganya,” alisema Zitto.

    Pia kamati hiyo imeitaka wizara hiyo kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu matumizi ya Sh100 bilioni zilizotumika kinyume na maombi yaliyowasilishwa kwenye Bajeti ya mwaka huo wa fedha.

    CAG ameshauri madeni yote ambayo Wizara ya Ujenzi inadaiwa yaorodheshwe ili yawe wazi kuepuka migongano katika matumizi ya fedha.

    Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Lukuvi alisema haelewi chochote na kusisitiza kuwa akipata taarifa rasmi za Kamati ya PAC, atatoa ufafanuzi.

    Halmashauri zinavyotafuna mabilioni

    Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAACc), imeeleza namna mamilioni ya fedha za Serikali zinavyoibwa kutoka Hazina kupitia halmashauri za wilaya huku Ilala ikitajwa kuongoza kwa ufisadi huo.

    Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mbarouk Mohammed aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Hazina imekuwa ikipeleka fedha kwenye halmashauri zikiwa zimezidi na kwamba kiasi kinachozidi hakirudishwi badala yake huliwa.

    Alisema kamati hiyo imefanya uchunguzi kwenye halmashauri 43 na kubaini kwamba mtindo huo ndiyo unaotumika kuiba fedha za Serikali.

    “Mwaka 2011/12 kiasi cha Sh1.5 bilioni zilipelekwa zikiwa zimezidi kwenye halmashauri hizo lakini hazikurudishwa Hazina kama inavyoonyesha kwenye ripoti ya CAG.

    Alisema kati ya kiasi hicho, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilipewa ziada ya Sh213 milioni ikifuatiwa na Geita iliyopewa Sh129 milioni.

    “Fedha hizo za mishahara zilipelekwa kwenye halmashauri hizo na Hazina kimakosa zikiwa zimezidi lakini watendaji wa hawakuzirudisha kama wanavyotakiwa kisheria badala yake zikayeyuka,” alisema.

    Mwenyekiti huyo alisema kuwa uchunguzi huo pia ulibaini kwamba katika halmashauri hizo 43 kiasi cha Sh693 milioni hulipwa mishahara hewa ambayo wafanyakazi wake walishakufa na wengine kustaafu.

    Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ililipa mishahara hewa yenye thamani ya Sh79.4 milioni ikifuatiwa na Ukerewe iliyolipa Sh57.5 milioni.

    Kwa upande wa fedha za miradi ya maendeleo, mwaka 2011/12, Hazina ilipeleka katika Halmashauri ya Mbarali, Mbeya Sh724 milioni kwa ajili ya Mradi wa Maendeleo ya Elimu Sekondari wakati mradi huo ulikuwa ukihitaji Sh70 milioni tu.

    “Kiasi cha Sh654 milioni zilipelekwa kimakosa na Hazina lakini badala ya kurudishwa zilitumiwa katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.

    Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ilipelekewa ziada ya Sh500 milioni na Mvomero ilipewa Sh85 milioni. “Kuna mtandao mkubwa wa Hazina na halmashauri ambao ukiachwa utaendelea kupoteza fedha nyingi za walipakodi,” alisema.
Zitto amuanika Waziri wa Ujenzi Bwana Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni
 
Wanabodi.
Pia kupandishwa kwa kesi mahakamani ni one thing thing, kushinda kesi is another na haki kutendeka is quite another thing!.
Mfano hai ni hii kesi ya kwanza kati ya hizo 9 iliyopandishwa mahakamani, serikali tayari imeishashi... kesi hata kabla kesi haijaanza kusikilizwa!.

Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.
Stay tuned.

Paskali

Hao umeficha nini? je kuna rafu kwenye hizi kesi? kwa nini unaionya mahamaka kutodhalilisha?
 
Pascal bila kusahau ile skendo ya uuzwaji wa nyumba za serikali katika mazingira yenye utata , wakat mkuu sana akiwa waziri

Afu eee eeee nimekumbuka bila kusahau na ile skendo ya kivuko kile walichopewa wale wazee wa mabaka baka na skendo zingine kwenye tenda za barabara

Ntafurahi kuona hizo nazo zikiwemo ili tujue huu u serious wake
 
Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Siku tukijuwa kujiheshimu wenyewe ndiyo tutajuwa kuheshimu binaadam wengine.

Binadam hata awe na makosa hatakiwi kudhadhalishwa mbele ya vyombo vya sheria. Hukumu ndiyo utaamua adhabu ama la. Na kama ni adhabu basi nayo hutolewa kwa mujibu wa sheria.

Tatizo kubwa la kutoheshimu haki za binadam huanzia kwenye malezi majumbani mwetu. Tunalea watoto kama watumwa, fimbo kwa kwenda mbele.

Mtoto aliyelelewa hivyo (abused) utegemee nini kutoka kwake?

Eid Mubarack, mama yangu mpendwa...umetumia akili kubwa saaana kufikisha ujumbe wako ila mimi nimekuelewa saaamna,yaaani una maanisha kua matendo ya ukubwani ni matokeo ya malezi toka utotoni, kwahiyo kwa mfano kama kuna kiongozi anatabia ya kuropoka ropoka na kuongea kauli za kukera na kuwadhalilisha watu, au kutokufuata utaratibu na kutumia busara iliotukuka, hii inatoa picha ya malezi aliolelewa na roho mbaya ya kibaguzi na kutokua na huruma ambayo imetokana na malezi mabaya aliolelewa na watu alioishi nao... asante saaana bi faiza fox kwa darsa kuntu ila kwa ulul albaab tu ndio wamekuelewa
 
Wataguswa wale waliohama chama.. alafu wale wabosi wao eti ni untouchable.
 
Kama hawa wengine akin JR hawaja nyongwa msitupe abari nyingine za kesi mnatutania sisi soyo watoto wadogo kwanini mnatuzingua nani aliwambia hatuna kumbu kumbu !!!
 
Mimi naunga mkono sana ila sipendi ubaguzi.Utakuta niwatu flani flani tu watashitakiwa wengine no!hizi vita za kibaguzi hazijawahi kimwacha mtu salama.Haki isipotendeka "kibiti"nyingine inakuja.Wateule wake No sasa miaka kumi ikiisha kama tusipoimarisha mifumo tutajikuta na yeye watu wake wanashtakiwa hivyo hivyo na sasa wakwaake itakiwa uvunjaji wa katiba.Mark my word wazungu wanasema
Upopo upopo acha tumalize mwaka kwa amani mkuu punguza punguza speed ya maono!!!
 
Wanabodi.

Nimepokea tetesi from deep inside kuwa kuna kesi nyingine 8 za ufisadi ambazo uchunguzi umekamilika na sasa ziko mezani kwa DPP zikisubiri kibali cha kupelekwa mahakamani.

Hili ni bandiko la ile jf advantage, be the first to know kuwa baada ya James Rugemalila na Habinder Sing kupandishwa kizimbani, uchunguzi kuhusu kesi nyingine 8 za ufisadi mkubwa zimekamilika hivyo soon kuna Vigogo wengine wakubwa watapandishwa kizimbani.

Source: A reliable tip from deep inside!.

Hata hivyo source hiyo from deep inside haikusema kesi hizo nane ni kesi zipi za ufisadi upi na wala ni vigogo gani hao watakao pandishwa kizimbani, ni kina nani na wamefanya nini!.

Awali kulipandishwa uzi
TAKUKURU kwa sasa wanachunguza kashfa za RICHMOND, EPA na Rada ...
taarifa hii TAKUKURU, inazungumzia uchunguzi, taartifa ya source wangu, inasema uchunguzi umekamilika, kesi ziko mezani kwa DPP, zinasubiri tuu uamuzi wa DPP.

Naomba msiniulize lolote kuhusu hiyo reliable source from deep inside kwa mujibu wa kanuni ya kihabari iitwayo "the confidentiality of the source".

Umuhimu wa tip hii ni kukupatia tuu info wewe mwana jf be the first to know kwa kuwa wa kwanza kujua. Information is power, kitendo cha kujua kuna kesi kubwa 9 za ufisadi mkubwa ni power kubwa ya uthibitisho. kuwa serikali ya Magufuli iko very serious katika vita hii ya ufisadi na haitanii!.
My Take.
Msihamanike sana kudhania sasa ndio ile mikesi yote ya ufisadi mkubwa itaibuliwa. No. Kuna kesi za ufisadi za touchables na za untouchables. Zitakazo fikishwa mahakamani ni only za touchables, zile za untouchables zenyewe haziguswi!.

Pia kupandishwa kwa kesi mahakamani ni one thing thing, kushinda kesi is another na haki kutendeka is quite another thing!.
Mfano hai ni hii kesi ya kwanza kati ya hizo 9 iliyopandishwa mahakamani, serikali tayari imeishashi... kesi hata kabla kesi haijaanza kusikilizwa!.

Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.
Stay tuned.

Paskali
Richmond hii alikujankuifungua Obama hama Richmond nyingine??? Tujiongeze akili kidogo tuuu yaani kiduchu
 
Back
Top Bottom