Tiririka hapa sababu zinazofanya mwanaume/mwanamke achelewe kuoa au kuolewa

Tiririka hapa sababu zinazofanya mwanaume/mwanamke achelewe kuoa au kuolewa

jomasi0002

Member
Joined
Apr 3, 2018
Posts
45
Reaction score
24
Habari za muda huu wanajamii forum. Nia na madhumuni ya Uzi huu kujua au kutambua sababu zinazo pelekea wanawake au wanaume wachelewe kuolewa au kuoa.
Karibuni sana
 
Tukifuata sheria miaka kuanzia miaka 18 kijana anaruhusiwa kuoa au kuolewa
Umri huo unaotaja vijana wengi wanakua wapo katika masomo bado hawajaanza kabisa kujitegemea,

Wazazi pia wamejawa na tamaa wanataka mahali kubwa kuliko nguvu ya kijana anaetaka kuoa, hivyo vijana wengi huogopa kuingia madeni ya ukweni.
Mabinti nao wanataka ndoa za kifahari ya gharama kubwa hivyo kumfanya kijana asogeze tarehe mbele kila akifikilia kuoa.
NB hapa ni vijana wa mijini.

Vijijini hakuna mambo mengi
 
Sija fix umri kwenye ayo maelezo nimesema neno KUANZIA
 
Visa vya mapenzi vinaogopesha wengi kuingia kwenye ndoa,
 
Mimi binafsi ni malengo niliyojiwekea na maisha ninayotaka kuishi kwenye ndoa.

Nilisema
1. Sioi bila kuwa na kwangu
2. Sikai kwenye nyumba ya kupanga, either nizeekee nyumbani kwa wazazi ama niwe na kwangu.
3. Sitaki mtoto wa nje ya ndoa.
4. Sioi nikiwa bado nimeajiriwa.
5. Nikioa ni spend muda mrefu na mzuri na familia yangu badala ya kuamka kila siku kukimbizana kutafuta hela ya kula na kodi.

Hayo ni ma sharti niliyojiwekea yaliyo shape maisha yangu.

Thank God nimetoka kwenye ajira na nina kampuni yangu. Najenga nyumba ya ghorofa na inakaribia kuisha.
Hayo masharti ndiyo yamenisukuma kufika hapa nilipo. Hope kabla ya uchaguzi 2020 nitakuwa ndani ya ndoa.
 
Back
Top Bottom