Tetesi: Tishio la kumuondoa Mufti BAKWATA

uongozi sio elimu tu bali busara, maarifa, hekma na uadalifu, mbona tunaongozwa na madokta lakini utadhani mangumbalu? jitathimini
Ongezea kwamba "ambao wanatumia kichwa cha sifuri brain adab??
 
Shida iko wapi? Wauwache Uislamu waendelee na mambo yao!
 
Mimi sio Muislamu ila yule Hemed Bin Jumaa Bin Hemed alikuwa ananivutia sana jinsi anavyoongea Kiswahili chake. Alikuwa akiongea anamalizia na kibwagio chake, "Dhahir eeh"
 
kundi la viongozi ndani ya baraza hilo wanakula njama za kumuondoa kiongozi wao makini Mufti Zubeir.

Kwa nini unasema "wanakula njama"?

Kwani dhambi kutaka kumng'oa mtu??????????? Lazima iwe negative conspiracy? Yale yale ya Zitto, Kitila, Mbowe na Chadema

Waafrika tatizo hatuwezi kukubali kuwa it's okay kumchoka kiongozi na kufanya mipango ya wazi ya kumwondoa, lazima iwe ni njama! Amezaliwa awe Mufti mpaka afe?

Katiba ya BAKWATA haina "expansion joints" za kuruhusu sauti za wadau kudai mabadiliko ya madaraka bila kuleta mpasuko na bila "kula njama"?
 
Nilikuwa napenda sana kusikiliza hotuba na mawaidha yake. Alikuwa na busara na hekma sana yule Mzee.
 
Acha ujinga wako wewe. Usifikiri unaongea na watoto wenzako hapa, ebwoo!!
 
Nilikuwa napenda sana kusikiliza hotuba na mawaidha yake. Alikuwa na busara na hekma sana yule Mzee.
Kipindi akiwa madarakani tu ilionesha dhahiri kwamba likija kutokea la kutokea juu yake basi ataacha pengo kubwa ambalo litachukua miaka mingi sana kuja kuzibwa. Mpaka sasa hilo pengo bado linaonekana dhahiri.
 
uongozi sio elimu tu bali busara, maarifa, hekma na uadalifu, mbona tunaongozwa na madokta lakini utadhani mangumbalu? jitathimini
Uongozi Ni taaluma kwanza alafu ndo ifuate busara.kama taaluma ya uongozi huna au huijui tegemea kufanya vituko na uharibifu
 
uongozi sio elimu tu bali busara, maarifa, hekma na uadalifu, mbona tunaongozwa na madokta lakini utadhani mangumbalu? jitathimini
Ni kweli ila sasa hayo maelezo mbona hayajanijibu kuhusu Ilmu zao?
 
Mimi napita tu! Ila wewe una uhakika gani kama kilichosemwa ni uongo ama ukweli? Na wewe unaelekea katika mkumbo wa kusingizia kama si kusema uongo.
Mkuu umeghafilika,uislamu unatukataza kusema mabaya ya marehemu hata Kama ni ya kweli.fanya toba mkuu na Allah Ni mwingi wa msamaha
 
Mkuu umeghafilika,uislamu unatukataza kusema mabaya ya marehemu hata Kama ni ya kweli.fanya toba mkuu na Allah Ni mwingi wa msamaha
Yes Uislam unakataza kusema mabaya ya Marehemu, je huyo aliyesema hayo ni Muislam? Lakini hata usipoyasema mabaya yake haiwezi kufuta ukweli kama marehemu alikuwa na mabaya yake au mazuri yake.
 
Uzuri na ubaya wa Uislam ndio huo? Hakuna ukiritimba na hakuna aliyembora zaidi ya mwenzie. Wangemchapa bakora kabla ya kuendelea na mengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…