Titanic inazama je utatoa nafasi yako ili umuokoe mwanamke

Titanic inazama je utatoa nafasi yako ili umuokoe mwanamke

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Mara kadhaa tumekuwa tukipata kusikia kauli mbiu nyingi kuwa wanawake wana nguvu na uwezo mkubwa katika jamii. Ni jambo ambalo sikatai na kulikubali kwani linaongeza chachu ya maendeleo ndani ya jamii zetu.
images - 2025-02-16T131305.317.jpeg


Ila sifa na mapambio yakiwa mengi tena wakati mwingine yakitumia maneno ya kutusi jinsia ya kiume sidhani kama ni sahihi. Unaweza kusifia uzuri wa nyota pasipo kuitusi nuru ya mwezi.
images - 2025-02-16T134048.892.jpeg


Hiki ni kipindi ambacho wanawake wengi wameaminishwa kuwa wapo imara kuliko wanaume, wana akili na utimamu mkubwa na bora kuliko wanaume, wana upendo na mahaba makubwa kuliko jinsia ya kiume na wengine wamefika mbali na kuanza kutumia mifano mibovu sana kuonekana nguvu ya mwanamke.
images - 2025-02-16T131944.527.jpeg


8 March kila mwaka ni siku ya kimataifa ya wanawake sambamba na tarehe November 19 ambayo ni siku ya kimataifa ya wanaume. Ila March 8 ni siku ya ajabu kwa sasa kwani inatumika kuonesha madhaifu ya wanaume.
images - 2025-02-16T133949.767.jpeg


Jumapili ya Pili ya mwezi Mei tunasherehekea sikukuu ya kina Mama, huku jumapili ya tatu ya mwezi Juni tunasherehekea siku ya baba duniani ila utashangaa kuna zygote mmoja inaweka chapisho refu sana kumsifia Mama yake kuwa ni kama Baba, ugonjwa wa akili kabsa. Kuna bumunda moja lenye jinsia ya kiume linasema halimpendi Baba yake kisa alisimuliwa na Mama yake kuwa Mzee alifanya vitu fulani vibaya.

Hatuwezi kusema kuwa Nyama ya Mbuzi ni tamu na yenye afya kiasi kwamba tukamsifia sana Mbuzi kwenye mada inayomhusu Ng'ombe, ni kichaa pekee ndo anaweza kufanya hivyo.

Hili ni swali kwa mwanaume:
Ikitokea ajali baharini au ziwani, chombo chenu kimepoteza matumaini na kinazama, uchache wa life jackets, pamoja na vifaa vya uokozi.

Je unaweza kumpa mwanamke nafasi ya yeye kuishi ilihali mwanzo wa safari alikuwa anakusimulia kuwa yeye ni SUPER WOMAN na hana uhitaji wa mwanaume maisha mwake?
images - 2025-02-16T134028.398.jpeg


TITANIC inazama, Je kama wanawake wa nyakati hizo wangekuwa wanataka usawa 50-50 unadhani Captain Edward John Smith angetoa maelekezo kuwa waanze kuokolewa Wanawake na Watoto?
images - 2025-02-16T131247.756.jpeg


Dunia inazidi kuwafanya wanawake waendelee kuwa delusional kupita maelezo. Kila kukicha ego zao zinaongezeka tena wakati ambao wanaume ndo watu wa msingi kwenye kuendesha dunia.
 
Wanasema wanaume wote ni umbwa lakini nijuavyo mimi mpapai hauzai mapera
 
nyakati hizi ni kila mtu akamate hamsini zake, nyakati hizo mwanaume alikuwa anakamata zake hamsini na za mwanamke hamsini hivyo alikuwa na mzigo mkubwa sana, lakini nyakati hizi huo mzigo tumepunguziwa, nyakati hizi Jack anapambana kivyake na Rose anapambana kivyake
 
Vita ya mwanamme na mwanamke inazidi kupamba moto huku upendo kati yao ukizidi kuwa wa kinafiki
 
kwenye mada hizi sipendi kuongea mengi maana nami nina mtoto wa kike halafu kesho sio mbali toka sasa, sitaki kuja kuhukumiwa na maneno yangu.
 
Skia mkuu najua unapotia kipindi kigumu, matukio na vibwenga vya wanawake vinaweza kukutoa relini. Wote tunajua ukweli mwanamke kamwe hawezi kuwa sawa na mwanaume, hiyo superiority complex ina sababishwa na utandawazi, malezi mabovu, theory za kijinga na kadhalika. Hata rose kwenye titanic alikuwa anaishi kifahari na alimdharau jack, ila baadae baada ya kuona jack yupo na strong masculinity alikuwa submissive to the point ya kumfanya awe kama kichaa.
Ukweli utabaki milele, know who you are, set standard zako, tafuta mwanamke anayekufaa na utaishi vizuri. Goodluck
 
nyakati hizi ni kila mtu akamate hamsini zake, nyakati hizo mwanaume alikuwa anakamata zake hamsini na za mwanamke hamsini hivyo alikuwa na mzigo mkubwa sana, lakini nyakati hizi huo mzigo tumepunguziwa, nyakati hizi Jack anapambana kivyake na Rose anapambana kivyake
Kabisa mkuu kila mtu anapambana saiv.
 
HII VITA IKIFANIKIWA KUMKARIRISHA MWANAUME KWAMBA MWANAMKE NI UCHAFU TU,NAAMINI HAPA KILA MTU ATAJITAMBUA.SIJUI NANI ATASHINDA KIMKAKATI ILA NAAMINI WANAUME WATAENDA KWA WANAWAKE KAMA AMBAVYO HUENDA DUKANI KUNUNUA BIDHAA..
NA HAPA NDIPO MMOJA ATAKUWA KAMA BAKULI AU CHOMBO FULANI CHA KUTUMIA TU.KISHA TUTATAMBUA NANI NI MHIMU NA MKUBWA KWA MWENZIE.WAANZISHA SLOGANI WATAANZISHA NYINGINE KWAMBA WANAWAKE WANACHUKULIWA KAMA WAKAZI WA TARANGIREE PARK AU HATA MANYARA PARK.WAKTI UTATUELEZA.
 
Back
Top Bottom