Tito Magoti na Theodory Giyan wafikishwa Mahakamani, wafunguliwa mashtaka 3 yakiwemo ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha

Tito Magoti na Theodory Giyan wafikishwa Mahakamani, wafunguliwa mashtaka 3 yakiwemo ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
IMG_20191224_131942.jpg

Afisa wa LHRC, Tito Magoti pamoja na mwenzake (kama wanavyoonekana pichani) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana huu

Hata hivyo bado haijafahamika wamefikishwa Mahakamani hapo kwa tuhuma gani

Tito Magoti pamoja na wenzake walitoweka siku 4 zilizopita kabla ya Polisi kujitokeza na kueleza kuwa waliwakamata na kuwashikilia.

====
UPDATE:

F31C5AAB-A064-4019-BF37-6AA7C2B8EECB.jpeg


965A1908-6B2D-4224-8E1C-1AFFF4EBAC9E.jpeg
73710E04-567B-447D-A36B-53AC1F32A012.jpeg

B65178A3-A2BA-4734-B964-86526E404E37.jpeg

Magoti apandishwa kizimbani kwa Uhujumu Uchumi

Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo la kutakatsha pesa shilingi Milioni 17.

Katika shitaka hilo Magoti amejumuishwa na wenzake Mtaalam wa Masuala Mtandao wa LHRC Theodory Giyan, ambao wote mnamo February Mosi na Disemba 17 wanatajwa kumiliki Program za Kompyuta na baadaye kujipatika Milioni 17 ambazo si zao.

Shtaka linamkabili na Magoti na Giyani ni kuwa sehemu ya Mtandao wa kiuhalifu, pamoja na kumiliki Mtandao wa Kompyuta uliotengenzwa kwa ajili ya kufanya uhalifu.

Hakimu anayesimamia Kesi ya Magoti na Wenzake ni Janeth Mtega ambapo kesi hiyo sasa imesogezwa mbele hadi January 7, 2020 huku washtakiwa hao wakirejeshwa rumande kutokana na aina ya makosa wanayoshtakiwa kukosa dhamana.

Magoti alikamatwa Ijumaa la Disemba 20, akiwa maeneo ya Mwenge jijini Dar es salaam huku siku chache baadaye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam akithibitisha kuwa Jeshi hilo kumshikilia Tito Magoti lakini bila kueleza sababu yake.
 
Tito Magoti na mwenzake wamepandishwa kisutu wakikabiliwa na shitaka la uhujumu uchumi ikiwemo kutakatisha fedha Tshs milioni 17.

Aidha pamoja na shitaka hilo pia wanakabiliwa na mashitaka mengine mawili ikiwemo kutengeneza program ya computer kinyume cha sheria ili kujipatia fedha.

Sisi tunaobeti siku tukipanda hapo hatuchomoki maana ni full kutakatisha.
 
Back
Top Bottom