Titus Amigu: Maneno uchawi au mchawi kwa dhana za Kiafrika hayastahili kuwamo kwenye Biblia

Utakuwa hujamuelewa
 
Mbona kaishia upadri tu hajawahi kanyaga hata uaskofu na kujitia ujuaji wote
Kwa hiyo kila Padre mwenye Elimu nzuri awe Askofu?.Hivi kuwaelimisha watu kuhusu mambo muhimu kwenye Biblia ni ujuaji?.
 
Aliishia kupokea sacraments ya upadre na daraja la upadiri ,madaraja ya juu zaidi ya upadri anayasikia kwenye radio tu wenzie wakiyapata

Mbona kaishia upadri tu hajawahi kanyaga hata uaskofu na kujitia ujuaji wote
Mtume Petro alikuwa hajasoma hajui kusoma wala kuandika lakini ndie alikuwa papa wa kwanza wa kanisa

Huyo father Amigu na falsafa yake na midigrii kibao ya falsafa na theolojia kaishia upadri tu
Utaacha lini kushambulia watu badala ya mada au ndio kusema mada imekuzidi uwezo ?.

Shambulia hoja achana na mtoa hoja.
 
Wewe unasumbuliwa na roho ya Ushindani,Kilichoandikwa na Fr.Amigu ni ishu ya Uchawi,badala ya kuleta hoja kuhusu mada yake wewe unaleta ishu zingine.Pole sana mkuu.
 
Kwa hiyo wewe ulitakaje?
 
Fr Amigu anasema mara nyingi Wakristo tumekopa mafundisho mengi juu ya mapepo kutoka dini zingine! Anasema mfano katika Ukristo hakuna fundisho juu ya Jini! Jini ni elimu ya Kiislamu na elimu yao inafundisha viumbe mbalimbali kwa namna yao ila wachungaji wanataja majini, mapepo, mizimu kama kiumbe kimoja.

Sisi Wakristo tunajua habari za malaika waasi ambao ni pepo wabaya/wachafu na hakuna mstari unaotaja jini! Anasisitiza elimu nyingi wanazofundisha wachungaji ni za kukopa na kinyume na mafundisho ya Ukristo.

Mfano mwingine anaosema Padre Amigu ni juu ya wachungaji kufundisha habari za nyota! Anasema hayo si mafundisho ya Kikristo wamekopa dini nyingine! Sisi Wakristo tuna vipawa vya Roho Mtakatifu sio nyota! Dini zingine hazimjui Roho Mtakatifu ndio maana wanasema habari za nyota.

Anasema hata kutabiri wanakofanya manabii siku hizi ni elimu za unajimu za kale! Zilitumika rangi, nyakati n.k kuweza kutabiri ila sio unabii ule wa manabii wa Mungu wala unabii wa agano jipya tunaloishi sasa Yesu akiwa nabii mkuu!

Father ukimsikiliza ana hoja nyingi sana. Wachungaji wanasikiliza na kusoma elimu za mambo ya giza kutoka imani zingine na kuzifundisha kwenye Ukristo! Kujaza watu hofu na kufanya tuogope hadi viumbe vya Mungu kama mijusi!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Aliishia kupokea sacraments ya upadre na daraja la upadiri ,madaraja ya juu zaidi ya upadri anayasikia kwenye radio tu wenzie wakiyapata
Yote aliyopaswa kuyapata, ameyapata.
 
Wewe unasumbuliwa na roho ya Ushindani,Kilichoandikwa na Fr.Amigu ni ishu ya Uchawi,badala ya kuleta hoja kuhusu mada yake wewe unaleta ishu zingine.Pole sana mkuu.
Theology ya discussion yake msingi wake ka vase kwenye African Bible ambayo yeye alihusika kwa sehemu kubwa

Ndio maana nikasimama lwenye hiyo Bibilia ya African Bible waliyotafsiri wenyewe akina Father Amigo kuwa iko wrong tafsiri zao na ndizo zimepelekea waamini uchawi haupo kwa ku base kwenye tafsiri zao wenyewe zilizo wrong
 
Padri Amigu ni chenga sana.

Kwahiyo anataka watu wabaki kwenye boksi dogo la UKRISTO wasipate maarifa mengine nje ya hapo?

Kuna ubaya gani mkristo kujifunza kuhusu majini? Mbona kuna taaluma kabisa inaitwa DEMONOLOGY na inatambulika?

Huyu AMIGU ni MCHAWI tu.
 

We kweli unasoma na kuelewa ?

Nimesema "BIBLIA YA KIAFRIKA kwa kiswahili". Afu siku nyingi nishakueleza ujifunze kujadili HOJA na sio kumjadili mtoa HOJA. Afu Mtoa hoja amezungumzia utafsiriji wa maneno ya kigiriki na kiebrania lugha za asili za biblia kuja lugha yetu ya kiswahili na sio kutoka kingereza kuja lugha yetu ya kiswahili.

Au Ninyi ndio wale manabii na mitume mnaotumia vibaya biblia takatifu kwa kuwajaza watu mafundisho juu ya laana, mapepo, uchawi, ushirikina, majini, kurogwa nk ili muendelee kupiga pesa na kunufaika na UJINGA wa baadhi ya watu (waumini wenu) juu ya hayo mambo ?.
 
Hakuna binadamu anayeogopwa wala anayetishia mwingine

Uchawi upo na mapdre wanalogana sana

Father Amigu anajifanya hajui kuna kulogana huko kwa mapadre wao kwa wao hatari awaulize wenyewe

Wala siri sema nimeongea kistaarabu

Father Amigu mwenyewe alishindwa kupanda madaraja kwa kulogwa na wenzie ndio maana ana elimu.kubwa na ufahamu mkubwa lakini yuko chini tu ohh anasema uchawi haupo wenzie wanamlogs wanapanda juu wanamwacha hapo hapo na ujuaji wake akiwa kalogwa barabara
 
Jargons na many misamiati inaelimisha na kuzindua fikra zilizolala.

Hesabu 23:23
Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
 
Kila andiko lenye pumzi ya Mungu linafaa kwa kuonya kufundisha na kurekebisha mambo.
Biblia iwe imekosewa au haijakosewa lakini Wakristo tunambiwa tuisome kwa muelekeo wan kujenga..mpaka Sasa imetafsiriwa mara nyingi na imethibitishwa kwamba ni sahihi swala la lugha na maana vinabadilika Sana ...kwa tofauti hizo ndogo ndogo nakuthibitiehia UchAwI ,ULOZI ,RAMLI ni vibaya tangu enzi hizo mpaka leo na UChawi wa bongo una madesa mengi mno waulize maustaadh watakuambia vipi vitabu vinauzwa Tena Bei mbaya Sana vinavyotoa Siri hizo Leo Kuna waganga,wanamazingaombwe,. Na watu waaaina nyingi wanaofanya uchawi na KUPATA heshima Kama taaluma ya kawaida..
 
Huyu Fr. Hana Youtube Channel?
 
Dhana ya kupinga kinachoitwa Uchawi au Ushirikina, amekiandika kwenye kitabu chake kinaitwa 'Jinsi ya kuushinda Ulimwengu'. Nlikisoma miaka 13 iliyopita. Ishakuwa kitambo ila nakumbuka vizuri allivyoandika kwenye kitabu chake. wakati huo pia nilisoma kitabu chake kingine kinaitwa ' Maswali wanayobandikwa wakatoliki' Mle kachambua hoja moja baada ya nyingine kuhusu Ukatoliki. Huyu Padre huwa haamini kama kuna uchawi Duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…