Inference gani hii sasađPadri jinga hili, usikute lenyewe ndio CHAWI HASWA.
Ukiona mtu anapinga uchawi ujue ndio CHAWI LENYEWE.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inference gani hii sasađPadri jinga hili, usikute lenyewe ndio CHAWI HASWA.
Ukiona mtu anapinga uchawi ujue ndio CHAWI LENYEWE.
Aliishia kupokea sacraments ya upadre na daraja la upadiri ,madaraja ya juu zaidi ya upadri anayasikia kwenye radio tu wenzie wakiyapataKuna Sakramenti ya Upadre tu, hakuna ya uaskofu.
Utakuwa hujamuelewaMkatiliki mie. Namsikiliza sana Fr. Titus sawa ni mtauhidi mzuri kwa maana ya fani hiyo ndani ya Kanisa Katoliki. Anaelewa lugha mama ya Maandiko Matakatifu. Lakini asisahau kuwa hata Afrika au uswahilini zipo taaluma zote hizo kama za mamajusi, waongea na wafu, mazingaombwe, nk na kuna shule za kujifunza hayo kwa namna rasmi (formal) na isiyo rasmi (informal).
Kusema kwamba hayo mambo yanayoitwa uchawi kwenye Biblia ilikuwa taaluma lakini katika mazingira ya uswahili sio taaluma sio kweli.
Wachawi walikuwepo kwenye biblia na uchawi wao sio less evil ukilinganisha na uchawi kwa dhana ya Kiswahili. Wale wachawi wa Misri hawakubadili fimbo zao kuwa nyoka kwa kutumia ujuzi wa kisayansi ya binadamu, walitumia nguvu ya kipepo. Hayo hufanyika pia katika dhana ya uchawi ya Kiswahili.
Ambacho Pd. Amigu na wengine hukosea sana ni kutokuamini uwepo wa wachawi na uhalisia wao. Wengi wa hawa wanatheologia wasomi hufikiri ni ujinga kusema nimelogwa. Ulozi upo na hayo yote ni kazi za shetani katika madaraja mbalimbali.
Kwa hiyo kila Padre mwenye Elimu nzuri awe Askofu?.Hivi kuwaelimisha watu kuhusu mambo muhimu kwenye Biblia ni ujuaji?.Mbona kaishia upadri tu hajawahi kanyaga hata uaskofu na kujitia ujuaji wote
Aliishia kupokea sacraments ya upadre na daraja la upadiri ,madaraja ya juu zaidi ya upadri anayasikia kwenye radio tu wenzie wakiyapata
Mbona kaishia upadri tu hajawahi kanyaga hata uaskofu na kujitia ujuaji wote
Utaacha lini kushambulia watu badala ya mada au ndio kusema mada imekuzidi uwezo ?.Mtume Petro alikuwa hajasoma hajui kusoma wala kuandika lakini ndie alikuwa papa wa kwanza wa kanisa
Huyo father Amigu na falsafa yake na midigrii kibao ya falsafa na theolojia kaishia upadri tu
Wewe unasumbuliwa na roho ya Ushindani,Kilichoandikwa na Fr.Amigu ni ishu ya Uchawi,badala ya kuleta hoja kuhusu mada yake wewe unaleta ishu zingine.Pole sana mkuu.Katika Biblia yenye makosa mengi na makubwa ni hiyo Biblia ya Kiafrika waliyotafsiri hao akina Padri Amigu
Iko chini ya kiwango ambacho hata mjinga ambaye hajasoma falsafa au theolojia aweza ipinga waziwazi
Kuanzia msitari wa kwanza kabisa wa Biblilia ambao ni wa kitabu cha Mwanzo 1:1 yaani Genesis 1:1
Bibliia ya King James version na Biblia za zamani huo mstari unasomeka hivi "In the begging God created heavens and Earth"
Hiyo tafsiri ya African Bible ya Akina Padri Amigu na kundi lake inasomeka hivi "At first God made Heavens and Earth '
Sasa mimi mfuasi wa mitume na manabii nichambue upotofu wa akina Padri Amigu.kwenye hiyo Biblia yao ya African Bible kwenye huo mstari tu
Biblia za zamani zilitumia neno.God Created heavens and Earth akina Amigu wakatafsiri God made Heavens and Earth
Tofauti iko wapi mtu aweza ulizs.Tofauti
Creating means making something out of Nothing.Kuwa Mungu aliiumba dunia bila kutumia mali ghafi yeyote toka popote.alitamka tu iwepo mbingu ikawepo akatamka iwepo dunia ikawepo hakukuwa na utengeneza dunia na Mbingu kama vile Mungu aliingia kwenye karakana akakusanya materials na kuanza kuchonga mbingu na dunia ndio maana Biblia zilizotangulia zilitambua ukuu wa Mungu wa ku create vitu out of nothing
Twende hiyo Tafsiri ya hiyo Biblia ya African Bible waliyotafsiri Akina Amigu inasema God made heavens and Earth.Tunaelewa wote maana ya Made.Kitu ukiambiwa made ni kuwa kuna materials zimetumika kukitengeneza ndio kikawa hivyo kilivyo hakikuibuka tu yaani hakikuwa created
Sasa tuje kwa nini waliamua huo mstari kutumia God made badala ya God Created?
Hilo kundi lililotafsiri hiyo Biblia la Akina Amigu ni wana theolojia na falsafa wasioamini mambo ya miujiza kabisa
Ndio maana walipofikia kutafsiri palipoandikwa God Created wakasema haiwezekani akaitoa mbingu na dunia into existence bila kutumia materials kutengeneza hiyo dunia na mbingu futa hilo neno Created weka made!!!
Ndio maana Padre Amigu pia haamini kuwa uchawi upo!!! Ndio maana maneno yote ongelea uchawi wakayoondoa kwenye hiyo.African Bible yao waliyotafsiri
Nimetolea mfano wa huo mstari mmoja kifupi hiyo Biblia imejaa makosa mengi mno yasiyoendana na utendaji wa.Mungu ni ya watu wasioamini miujiza ya Mungu.wala uwezo wake au maajabu ya mashetani na malaika waliasi mbinguni na uchawi wao walioleta Duniani
Kwa hiyo wewe ulitakaje?Kuwa msomi wa Biblia hakumaanishi unaijua biblia au maandiko thus pana madhehebu mengi haya yametokana na viongozi wao au waanzilishi wao kutoyajua maandiko.
Padri Titus inamchanganya kutofautisha taaluma ya uchawi, usomaji nyota, uganga, waonaji, nk.
Unaposema nguvu za giza, uchawi ni kijinukta tu katika jumla ya nguvu zote za giza au uwezo usioonekana.
UCHAWI NI NINI
ni nguvu hasi iliyojificha yenye kudhuru mwili, mali, wanyama nk. Mchawi amebase kwenye kudhuru au kuharibu,
Uchawi ni mpana pana aina za uchawi,makundi na vyama vya kichawi.mfano black magic, red magic,white magic,nk.
MGANGA anafanya vyote kudhuru na kuponya kutegemea na matakwa ya mteja, mganga ni mfanyabiashara pesa YAKO ndio uamuru mganga afanye nini. Hata ukitaka kusomea uganga ni lazima usomee uchawi kwanza ukifuzu uchawi ndipo unaanza kozi ya pili ya uganga. Kipo Chuo unasoma uchawi miaka mitano then uganga miaka miwili so mda wa kozi yote ni miaka 7 unakuwa umefuzu.
MAGICIAN mazingaombwe huyu ni mchawi yeye utumia uchawi kufanya miujiza kwenye maonyeaho kwa malipo ya kiingilio, ufanya visivyoonekana kwa macho ya kawaida kwa msaada wa nguvu za mapepo au majini ambayo uwafunika macho watazamaji wasione mchakato mzima jinsi mazingaombwe yanayofanyika.
MAMA JUSI ,WASOMA NYOTA,WANAJIMU ,Wazee wa falaki hawa ni wataalamu wa elimu ya nyota Wana elimu ya kusoma mpangilio wa nyota, mwezi na jua KWA kuhusisha na maisha ya wanadamu.
WATABIRI WAONAJI hawa ni watu wenye uwezo wa kutambua mambo yaliyojificha yasiyoonwa kwa macho ya kawaida wenye kutambua mambo yatakayotea, nk hapa Wanahusika viumbe vya roho mfano majini, malaika, nk.
Kweli wewe ni Bichwa Komwee,ID yako inasadifu kilichojaa kwenye ubongo wako.Padri jinga hili, usikute lenyewe ndio CHAWI HASWA.
Ukiona mtu anapinga uchawi ujue ndio CHAWI LENYEWE.
Yote aliyopaswa kuyapata, ameyapata.Aliishia kupokea sacraments ya upadre na daraja la upadiri ,madaraja ya juu zaidi ya upadri anayasikia kwenye radio tu wenzie wakiyapata
Theology ya discussion yake msingi wake ka vase kwenye African Bible ambayo yeye alihusika kwa sehemu kubwaWewe unasumbuliwa na roho ya Ushindani,Kilichoandikwa na Fr.Amigu ni ishu ya Uchawi,badala ya kuleta hoja kuhusu mada yake wewe unaleta ishu zingine.Pole sana mkuu.
Aidadavue vizuri hoja yake anataka kusema nini.Kwa hiyo wewe ulitakaje?
Biblical inference [emoji847]Inference gani hii sasa[emoji3]
Padri Amigu ni chenga sana.Fr Amigu anasema mara nyingi Wakristo tumekopa mafundisho mengi juu ya mapepo kutoka dini zingine! Anasema mfano katika Ukristo hakuna fundisho juu ya Jini! Jini ni elimu ya Kiislamu na elimu yao inafundisha viumbe mbalimbali kwa namna yao ila wachungaji wanataja majini, mapepo, mizimu kama kiumbe kimoja.
Sisi Wakristo tunajua habari za malaika waasi ambao ni pepo wabaya/wachafu na hakuna mstari unaotaja jini! Anasisitiza elimu nyingi wanazofundisha wachungaji ni za kukopa na kinyume na mafundisho ya Ukristo.
Mfano mwingine anaosema Padre Amigu ni juu ya wachungaji kufundisha habari za nyota! Anasema hayo si mafundisho ya Kikristo wamekopa dini nyingine! Sisi Wakristo tuna vipawa vya Roho Mtakatifu sio nyota! Dini zingine hazimjui Roho Mtakatifu ndio maana wanasema habari za nyota
Theology ya discussion yake msingi wake ka vase kwenye African Bible ambayo yeye alihusika kwa sehemu kubwa
Ndio maana nikasimama lwenye hiyo Bibilia ya African Bible waliyotafsiri wenyewe akina Father Amigo kuwa iko wrong tafsiri zao na ndizo zimepelekea waamini uchawi haupo kwa ku base kwenye tafsiri zao wenyewe zilizo wrong
Katika Biblia yenye makosa mengi na makubwa ni hiyo Biblia ya Kiafrika waliyotafsiri hao akina Padri Amigu
Iko chini ya kiwango ambacho hata mjinga ambaye hajasoma falsafa au theolojia aweza ipinga waziwazi
Kuanzia msitari wa kwanza kabisa wa Biblilia ambao ni wa kitabu cha Mwanzo 1:1 yaani Genesis 1:1
Bibliia ya King James version na Biblia za zamani huo mstari unasomeka hivi "In the begging God created heavens and Earth"
Hiyo tafsiri ya African Bible ya Akina Padri Amigu na kundi lake inasomeka hivi "At first God made Heavens and Earth '
Sasa mimi mfuasi wa mitume na manabii nichambue upotofu wa akina Padri Amigu.kwenye hiyo Biblia yao ya African Bible kwenye huo mstari tu
Biblia za zamani zilitumia neno.God Created heavens and Earth akina Amigu wakatafsiri God made Heavens and Earth
Tofauti iko wapi mtu aweza ulizs.Tofauti
Creating means making something out of Nothing.Kuwa Mungu aliiumba dunia bila kutumia mali ghafi yeyote toka popote.alitamka tu iwepo mbingu ikawepo akatamka iwepo dunia ikawepo hakukuwa na utengeneza dunia na Mbingu kama vile Mungu aliingia kwenye karakana akakusanya materials na kuanza kuchonga mbingu na dunia ndio maana Biblia zilizotangulia zilitambua ukuu wa Mungu wa ku create vitu out of nothing
Twende hiyo Tafsiri ya hiyo Biblia ya African Bible waliyotafsiri Akina Amigu inasema God made heavens and Earth.Tunaelewa wote maana ya Made.Kitu ukiambiwa made ni kuwa kuna materials zimetumika kukitengeneza ndio kikawa hivyo kilivyo hakikuibuka tu yaani hakikuwa created
Sasa tuje kwa nini waliamua huo mstari kutumia God made badala ya God Created?
Hilo kundi lililotafsiri hiyo Biblia la Akina Amigu ni wana theolojia na falsafa wasioamini mambo ya miujiza kabisa
Ndio maana walipofikia kutafsiri palipoandikwa God Created wakasema haiwezekani akaitoa mbingu na dunia into existence bila kutumia materials kutengeneza hiyo dunia na mbingu futa hilo neno Created weka made!!!
Ndio maana Padre Amigu pia haamini kuwa uchawi upo!!! Ndio maana maneno yote ongelea uchawi wakayoondoa kwenye hiyo.African Bible yao waliyotafsiri
Nimetolea mfano wa huo mstari mmoja kifupi hiyo Biblia imejaa makosa mengi mno yasiyoendana na utendaji wa.Mungu ni ya watu wasioamini miujiza ya Mungu.wala uwezo wake au maajabu ya mashetani na malaika waliasi mbinguni na uchawi wao walioleta Duniani
Hakuna binadamu anayeogopwa wala anayetishia mwingineWe kweli unasoma na kuelewa ?
Nimesema "BIBLIA YA KIAFRIKA kwa kiswahili". Afu siku nyingi nishakueleza ujifunze kujadili HOJA na sio kumjadili mtoa HOJA. Afu Mtoa hoja amezungumzia utafsiriji wa maneno ya kigiriki na kiebrania lugha za asili za biblia kuja lugha yetu ya kiswahili na sio kutoka kingereza kuja lugha yetu ya kiswahili.
Au Ninyi ndio wale manabii na mitume mnaotumia vibaya biblia takatifu kwa kuwajaza watu mafundisho juu ya laana, mapepo, uchawi, ushirikina, majini, kurogwa nk ili muendelee kupiga pesa na kunufaika na UJINGA wa baadhi ya watu (waumini wenu) juu ya hayo mambo ?.
Jargons na many misamiati inaelimisha na kuzindua fikra zilizolala.Mkatiliki mie. Namsikiliza sana Fr. Titus sawa ni mtauhidi mzuri kwa maana ya fani hiyo ndani ya Kanisa Katoliki. Anaelewa lugha mama ya Maandiko Matakatifu. Lakini asisahau kuwa hata Afrika au uswahilini zipo taaluma zote hizo kama za mamajusi, waongea na wafu, mazingaombwe, nk na kuna shule za kujifunza hayo kwa namna rasmi (formal) na isiyo rasmi (informal).
Kusema kwamba hayo mambo yanayoitwa uchawi kwenye Biblia ilikuwa taaluma lakini katika mazingira ya uswahili sio taaluma sio kweli.
Wachawi walikuwepo kwenye biblia na uchawi wao sio less evil ukilinganisha na uchawi kwa dhana ya Kiswahili. Wale wachawi wa Misri hawakubadili fimbo zao kuwa nyoka kwa kutumia ujuzi wa kisayansi ya binadamu, walitumia nguvu ya kipepo. Hayo hufanyika pia katika dhana ya uchawi ya Kiswahili.
Ambacho Pd. Amigu na wengine hukosea sana ni kutokuamini uwepo wa wachawi na uhalisia wao. Wengi wa hawa wanatheologia wasomi hufikiri ni ujinga kusema nimelogwa. Ulozi upo na hayo yote ni kazi za shetani katika madaraja mbalimbali.
Huyu Fr. Hana Youtube Channel?Nimekataa uwapo wa uchawi na wachawi kati yetu. Tulionao ni wababaishaji na watu tunaowatuhumu kwa kuwasengenyasengenya tu. Wachawi kiukweli hawapo na bado ninawatafuta. Ninataka wajitokeze na nimesema kama kuna anayewajua awataje, atuitie au atuoneshe
Nisikilizeni vijana na wasomaji wangu. Ni hivi, kwenye Biblia hakuna hata mahali pamoja palipoandikwa kwa Kiswahili neno âMchawiâ au âUchawiâ kwa mastahili. Biblia za Kiswahili zimetutumbukizia maneno hayo pasipo simile.
Maneno hayo yaliyotumbukia humo hayabebi maana na dhana halisi ya kilichosemwa katika lugha asilia za Kiebrania au Kigiriki. Dhana ya Kiafrika juu ya uchawi na wachawi haiingii kwenye Biblia hata kidogo.
Nina hoja. Nadhani mnaweza kukubaliana nami kwamba katika makabila yetu dhana au fasili ya uchawi si nyepesi. Ni dhana mtambuka.
Dhana au fasili yetu ya wachawi ni ya watu wenye nguvu za ajabu za kufanyia mambo ya ajabu kama tunavyosema wenyewe, labda kuruka angani kwa nyungo, fisi, mbweha, pembe au mikeka, kunyesha mvua hata kiangazi, kupiga radi wapendavyo, kuingia majumbani mwa watu kwa kupitia milango na hata madirisha yaliyofungwa, kuroga tokea mbali, kutazama na kudhuru watu kwa macho au kauli, kuwabadili watu wakawa labda mainzi, nyoka au ngedere na kadhalika. Orodha ni ndefu mno. Kwa lugha yenu vijana, âorodha ni ndefu kishenzi!â
Ndipo kwetu sisi âwachawiâ ni watu wenye uwezo wa kuwatoa wafu makaburini na kuwala nyama maiti, wenye uwezo wa kufanya mikutano usiku pasipo watu wengine kuwaona, watu wenye kuwatengeneza na kuwatunza watu kama misukule, watu wenye uwezo wa kuroga wengine kutoka mbali, watu wasioweza kuonekana wanapofanya shughuli zao, watu wenye kutembea usiku uchi wa mnyama, watu wanaoweza wakawatazama watu kwa macho ya aina yake wakadhurika vibaya, watu wanaoweza kuwasemea wenzao maneno ya laana au mikosi wakadhurika na kadhalika.
Naomba maweza mengine muyaongezee wenyewe maana, bila mashaka, kwenu dhana hii ipo nanyi, kama humwamini wenyewe, walau mmesikia habari zake.
Aghalabu, mnajua jinsi tunavyodhuriana katika jamii zetu, kujichonganisha, kupoteza muda na pesa nyingi, kwa shughuli za jamaa kushikana na kwenda kunyoana kwa waganga wa kienyeji, watu kuwaalika akina Lambalamba na kusafisha vijiji vyao, watoto kuwatuhumu na kuwaua wazazi wao, wanavijiji kubomoleana nyumba au kuchomeana moto wakifukuzana kwa ukatili mkubwa.
Watu kuwaua vikongwe na wazee, watu kuwafukuzia watuhumiwa wao kwenye vijiji vya wachawi, watu kuwapiga na kuwachomea wengine nyumba moto au kuwaharibia mazao na mali zao wakidaiwa kuzuia mvua, timu zetu za michezo kutumia pesa nyingi kulipia mabenchi ya ufundi yaani waganga wa kienyeji.
Wachezaji wetu kupewa masharti magumu au kulazwa makaburini kabla ya mechi, watu kuzindika nyumba zao kwa hirizi, watu kuwaua au kuwadhuru albino wakitafuta viungo vyao wapate vyeo na utajiri, watu kutafuta mifupa na mafuvu ya binadamu kwa ajili ya kuboreshea biashara au ajira zao, akina mama kuuawa kwa sababu ya sehemu zao za siri, watu kunyofolewa macho, ndimi na masikio, watu kutafuta, kuchukua na kuvaa hiziri na kadhalika.
Sina mashaka, haya yote mnayajua, imani na vitendo vilivyoipa Tanzania nafasi ya kwanza Afrika katika kuamini uchawi, kwa kadiri ya utafiti wa mwaka 2009 wa PEW Research Centre ya Washington D.C, Marekani.
Lakini habari ngeni kwenu nyote ni hii kwamba Biblia haina dhana hiyo, hata chembe na hakuna panapostahili kutokea neno uchawi au mchawi ndani yake. Maneno hayo yanatokea isivyostahili.
Msishtuke. Ndipo hapo hapo ninapojaribu kulitangaza jambo hili pasipo kusadikika. Wengi wananishangaa sana, lakini si kitu nimeunda jeshi la mtu mmoja! Kumbe, nguvu ya hoja yangu ni lugha asilia zilizotumika kuandikia Biblia. Nawahakikishieni nyote kwamba dhana yetu ya uchawi na wachawi haimo kwenye Biblia maana maneno yote asilia yaliyotumika humo hayana maana zetu.
Msinibishe. Nendeni kwenye lugha asilia Kiebrania (Agano la Kale) na Kigiriki (Agano Jipya). Biblia katika lugha zake asilia hazina maneno yenye maana zetu. Ndiyo maana nakataa kwa nguvu na kwa kujiamini kabisa.
Tafsiri za Kiswahili na Kiingereza zinatupotosha. Kwa bahati njema baadhi ya watafsiri wa nakala za Kiingereza wamejitahidi sana ama kuepuka au kutumia kiusahihi maneno: 'witchcraft', 'sorcery' na 'magic'. Katika Kiswahili tuna maksi ya karibu sefuri.
Tusiandikie mate, wino ungalipo. Hebu tuthubutu kujitengea muda siku fulani tujisomee na kutafakari kwa utulivu sehemu zifuatazo: Mwa 41:8.21, 1Sam 28:7, Kut 7:11.22, 8:7.18.19, 9:11, Law 19:26, Kum 18:10-11, Isa 3:3, 47:9.12, Dan 1:20, 2:2.10.27, Nah 3:4, Mdo 13:6.8, 19:19, Gal 5:20 na Ufu 22:15. Hizi ndizo sehemu maarufu kwa maneno uchawi, mchawi au wachawi. Zatupasa kuzichambua kwa makini. Maneno yametumika kwa kupwaya mno.
Nawahakikishieni tena kwamba tukizitalii sehemu hizi katika lugha zake asilia, hatutapata maana ya wachawi katika dhana ya Kiafrika isipokuwa mojawapo ya maana hizi: mabingwa wa kutumia visivyo utaalamu mbalimbali, wachanganya madawa, wacheza mazingaombwe, watu wenye kuwatinga wenzao kwa utaalamu, wataalamu wa nyota, watabiri, wapiga ramili, waona maono, watu wanaotafuta ushauri wa wafu au mapepo, watafsiri ndoto na kadhalika. Maana hizi ndizo zilipaswa kuchaguliwa vyema na waliotutafsiria Biblia katika Kiswahili zamani zile.
Kumbe, wote waliotajwa hivyo, kwenye Biblia, kwa Wayahudi, walikuwa wataalamu waliokuwa wanajulikana na watu na utaalamu wao uliwekwa kwenye vitabu vyenye kusomeka bayana (rej. Mdo 19:19).
Ndipo, basi, tusidanganyike tukachukua dhana yetu ya uchawi ya Kiafrika tukaiingiza kwenye Biblia takatifu. Tutakuwa waongo na wakufi wa weledi. Narudia na kusisitiza kwamba katika Biblia hicho kinachotafsiriwa kama âuchawiâ kilikuwa aina ya elimu au utaalamu.
Ndiyo maana kulikuwa na vitabu vyake kama nilivyosema sasa hivi (rej. Mdo 19:19) na watu wenye elimu hiyo walikuwa wakijulikana na wengine. Wataalamu wenyewe hawakumwonea mtu yoyote haya na wala hawakujificha. Ndiyo maana waliwahi kuitwa na Farao wakatokea barazani (Kut 7:11) na waliwahi kuitwa na mfalme Nebukadneza huko Babiloni wakajumuika na wataalamu wengine (rej. Dan 2:2). Hali kadhalika tazama jinsi Simeoni âmcheza mazingaombweâ alivyokuwa anajulikana na watu (rej. Mdo 13:6.8).
Tusemeje? Wale waliokuwa wanachuana na Musa wakati ule wa mapigo, hawastahili kuitwa wachawi kwa kadiri ya dhana yetu, isipokuwa âmaprofesa wa mazingaombweâ maana wakati ule kulikuwa na shule ya kufundishia uchezaji mazingaombwe kule Misri.
Ndiyo maana, kama maprofesa wenye elimu yenye kikomo, walishindwa kufanyiza vituko vya mapigo kadhaa. Mwanzoni mwa shughuli zake za kufanyiza miujiza, Yesu alidhaniwa kuwa amesomea katika chuo cha namna hiyo. Kwa ushuhuda, rejea maana ya watu wa Nazareti walivyojikwaa kwake katika Mk 6:1-6. Kifupi, katika tukio hilo la Nazareti, watu wa kijiji chake walikuwa wakihoji Yesu alipataje ada ya kusomea mazingaombwe wakati familia yake ilikuwa na kipato cha maseremala tu.
Hali kadhalika, wale waliokuwa wanaitwa na Mfalme Nekabudneza wamtafsirie ndoto yake wanastahili kutafsiriwa kama âmakuhani watafsiri mamboâ na siyo wachawi kwa kadiri ya dhana yetu. Soma vyema Dan 1:20 na 2:2.
Naendelea kukujuza. Usichoke kusoma. Kama wataalamu, watu tunaowasoma katika Biblia zetu za Kiswahili kama wachawi, walikuwa wanajulikana na watu. Nimesema wala hawakujificha. Zaidi ya hayo, kama wataalamu hawakuwa peke yao.
Ndiyo maana wakati wa matatizo walipokuwa wanaitwa wasaidie walikuwa hawaitwi peke yao isipokuwa pamoja na wataalamu wengine, kama vile, waganga, wenye hekima, mamajusi (tukitaka wanajimu), Wakaldayo (yaani watu wenye akili sana) na kadhalika (rejea tena Kut 7:11 na Dan 2:2).
Kinyume chake, huku kwetu tunasema sema tu majumbani au vijiweni mwetu. Tuseme tunasengenya tu. Huku kwetu nani anawajua âwachawiâ wetu na nani anaweza kutuitia âwachawiâ hao? Wako wapi? Nani anawajua? Hayupo Kwa nini hayupo anayewajua? Kwa sababu dhana yetu ya uchawi na wachawi ni tofauti kabisa na ile ya Biblia.
Katika Biblia unazungumziwa utaalamu sisi tunazungumzia uovu.
Biblia za Kiswahili zinatupotosha kama âHatujiongeziâ. Dhiki ya tafsiri imetufikisha pabaya pasipo kukusudia. Ndugu zanguni au rafiki zangu, maneno yaliyokosewa kutafsiriwa vizuri katika Biblia zetu za Kiswahili hata tukawa na maneno uchawi na mchawi ndanimwe ni haya: katika Kebrania 'artam' na 'artamim', 'oobh' na 'baelath oobh'.
Neno artam lilistahili kutafsiriwa kama kuhani mfasili mambo, au mtafsiri wa ndoto au kuhani msomaji mambo. Baelath oobh maana yake ni mwona maono au mtu anayetafsiri mambo kwa kuwasiliana na wafu.
Katika Kigiriki ni âfarmakeiaâ na âfarmakosâ, âmageiaâ na âmagosâ. Kwa upande wake maneno âfarmakeiaâ lilistahili kutafsiriwa kama âutaalamu wa uchanganyaji madawaâ na hivyo âfarmakosâ kuwa âmchanganya madawaâ. Neno âfarmakeiaâ ndilo lililozaa neno la Kiingereza âpharmacyâ neno tunalotumia sisi na kuliweka katika Kiswahili kama âsehemu ya dawaâ au âduka la madawaâ. Mnanielewa vizuri? Mnaona hapo? Mbona hatuiti âPHARMACYâ âduka la uchawiâ? Na mbona hatumwiti anayehusika na âpharmacyâ mchawi?
Mintarafu neno âmageiaâ linalozaa neno âmagicâ lilistahili kutafsiriwa âutumiaji wa mbinu au elimu fulani kupata matokeo fulaniâ, kwa mfano kutumia ujuzi fulani, dawa fulani, maneno fulani, matamshi au formula fulani. Na mwenye kutumia mbinu hizo ndiye anayeitwa âmagosâ.
Ndipo hapa walipoingia wale wataalamu wa kusoma nyota kutoka mashariki (rejea sikukuu ya Epifania au Tokeo la Bwana). Wataalamu hawa wanaitwa kwa Kiingereza âmagiâ au âastrologersâ nasi Waswahili tunawaita mamajusi au watu wenye hekima na siyo wachawi.
Ndipo hapa Waingereza walipojitengenezea istilahi za âblack magicâ kama utaalamu wa kudhuru watu na âwhite magicâ kama utaalamu wa kufanya maajabu bila kudhuru watu, yaani mazingaombwe ya kawaida.
Kwa vyovyote, watu wanaoujua lugha asilia za Biblia hawawezi kuingia katika wepesi wa kutafsiri maneno âartamâ, âartamimâ, âoobhâ, âbaelath oobhâ, âfarmakeiaâ, âfarmakosâ, âmageiaâ na âmagosâ kama âuchawiâ au âmchawiâ kwa dhana za Kiafrika.
Katika mstari huo huo, tusiwe watu wepesi wa kuchukulia na watumiaji Biblia wanaotusonga siku kwa siku kwa kudai wanajua Biblia. Imani yetu ni ya gharama, jamani. Hivi, tujitahidi sana tusimruhusu mtu yeyote aliyepitisha macho juu juu kwenye Biblia atupotoshe baada ya yeye mwenyewe kupotoshwa na Kiswahili kilichomletea maneno âuchawiâ na âwachawiâ bila tafakari.
Nitaeleza na ninaeleza sasa hivi. Ni hivi, tunachozugwa sisi na Biblia zetu za Kiswahili tukaelewa ni âuchawiâ ulikuwa ni utaalamu au kazi. Utaalamu huo ulikuwa ukitumika kwa ngazi mbalimbali. Aidha, kadiri ya Biblia, utaalamu (au kazi hiyo) unajulikana kwa majina mengi vile vile. Katika ngazi ya juu wanasimama âmamajusiâ na katika ngazi ya chini wanasimama wanaoitwa âwadanganyifuâ. Msihangaike, tutawafahamu hivi punde.
Nimesema katika ngazi ya juu kabisa wanasimama âmamajusiâ, yaani âwataalamu wa mambo ya nyotaâ au âwatu wenye hekimaâ. Hawa ndio waliotajwa katika Mathayo 2 na katika Danieli 1 na 2. Katika kitabu cha Danieli wataalamu hawa huitwa vile vile Walkadayo, yaani watu kutoka Kaldea ambako enzi zile kuliaminika kuwako watu wenye akili sana.
Ndiyo kisa, Danieli alipoonekana kuwa mtaalamu sana aliwekwa kuwa mkuu wa wataalamu wa Babiloni (Kiswahili chetu kikinyoosha husema âmkuu wa wachawiâ tu). Danieli alifanywa mkuu wa wataalamu (âwachawiâ kwa Kiswahili chetu rahisi) kwa sababu âroho ya miungu watakatifu, mwanga na elimu na hekima, kama hekima ya miungu, vilionekana ndani yakeâ. Kwa ushuhuda soma vizuri Dan 5:11.29.
Basi, kama mmenielewa vizuri, sasa tunazungumzia utaalamu na siyo uchawi kwa dhana yetu ya Kiafrika. Nimeshadokeza. Katika ngazi ya chini ya utaalamu huo walikuwa âwadanganyifuâ au âmatapeliâ waliokuwa wanacheza kwa viinimacho vyao kama wacheza mazingaombwe wanavyofanya leo hii kati yetu. Juu ya wadanganyifu hao Paulo anaandika, âWatu waovu na wadanganyifu wanaendelea kuwa wabaya, wakidanganya wengine, na wao wenyewe wakidanganywaâ (2 Tim 3:13).
Katikati ya ngazi hizo mbili, yaani katikati ya mamajusi na wadanganyifu (matapeli) walikuwa watu waliobabaisha wenzao kwa pilikapilika za ulozi, kupiga ramli, kupandisha mapepo na waganga waliokuwa wakijitafutia nguvu za pekee kwa kutamka maneno, kutumia majani na mizizi na madawa mbalimbali. Basi, hivi ndivyo isemavyo Biblia.
Natumaini tupo bado pamoja. Hadi hapa nimeshazinyooshea kidole Biblia za Kiswahili kwa kutokutuletea tafsiri muafaka. Lakini tuwasamehe watafsiri wake. Labda mnaweza kuniliuza, limetokeaje jambo hilo? Nisikilizeni tena. Miaka ile ya 1937, kule Zanzibar, Wazungu waliposimamia zoezi la kutafsiri Biblia katika Kiswahili, hawakuketi na kujaribu kutuletea dhana halisi ya maneno âartamâ, âartamimâ, âoobhâ, âbaelath oobhâ, âfarmakeiaâ, âfarmakosâ, âmageiaâ na âmagosâ. Ndipo kwa kunyoosha mambo wao na wasaidizi wao wakawa wanapachika neno âuchawiâ au âmchawiâ popote pale pasipo simile.
Labda sijaeleweka. Nitawaelewesha kwa mifano. Mfano wa kwanza ni huu wa mtafsiri wa maandishi fulani ambaye atatumia neno âpombeâ kutafsiri maneno kadha wa kadha: divai, bia, whisky, gongo, mbege, ulanzi, tembo, uraka, komoni, chibuku, kangara, wanzuki, gundi ya seremala, âketamineâ, dawa ya panya na chochote chenye nguvu ya kumlewesha mtu.
Ataweza kufanya hivyo lakini hatakuwa sahihi kwa maana divai ni tofauti na komoni, mbege ni tofauti na ulanzi, gongo ni tofauti na wanzuki, gundi ya seremala ni tofauti na whisky, âketamineâ ni tofauti na dawa ya panya na kadhalika. Hapo itabidi msomaji awe na akili ya kujiongeza. La sivyo, atasema vyote hivyo ni sawa tu kwa vile vimetafsiriwa vyote kwa neno moja âpombeâ.
Natoa mfano mwingine. Ni kama mtu anavyopaswa kuwa na akili ya kujiongeza anaposoma misemo kama hii: âBaada ya kufanya vibaya katika Ligi Kuu, timu ya Majimaji inamtafuta mchawiâ, âKaka yangu alikuwa mchawi wa hesabuâ, âNewton alikuwa mchawi wa sayansiâ, âPele alikuwa mchawi wa kabumbuâ, âMaradona alikuwa mchawi wa chengaâ, âBibi Kalembwani alikuwa ananyoa wachawi Mahengeâ, âakina Lambalamba wapo Dodoma kuwashika wachawiâ na kadhalika. Ikiwa msomaji husika ataelewa misemo hiyo yote sawa, basi yeye atakuwa amefeli medani ya lugha.
Kwa hiyo, ni tafsiri kumbakumba ya Zanzibar iliyotuingiza katika kadhia ya kuwa na maneno âuchawiâ na âmchawiâ isivyojuzu kwenye Biblia ya Kiswahili. Maneno mengine yanayopaswa kuwekwa sawa kitaalamu kabisa na pengine kufutwa kabisa ni: YEHOVA, JINI na UZINZI. Siku moja nitawafafanulieni kwa jinsi gani maneno haya yanasikitisha kuonekana katika Biblia zetu za Kiswahili.
Kumbe, natamatisha somo langu, kwa kusisitiza kunena kwamba katika sehemu mbalimbali tunapoona Kiswahili kimetunyooshea tafsiri kwa maneno âuchawiâ au âwachawiâ ni tafsri ya maneno âkuona maonoâ, au âkucheza mazingaombweâ au âkuchanganya madawaâ au âkutumia ujuzi kutafsiri mamboâ na kadhalika.
Kwa mantiki hii, ndugu zanguni, tukirudi kwenye lugha asilia za Biblia, yaani Kiebrania na Kigiriki tutakuwa na fikra mbadala. La sivyo, tutaendelea kukaidiana juu ya dhana yetu ya uchawi, tukiamini Biblia ipo upande wetu.
Haya shime hatujachelewa kuingia kwenye mabadiliko haya ya fikra kwa njia ya lugha asilia za Biblia. Ndiyo, Kiswahili ndiyo hicho, lakini kuna sehemu na maneno ya Biblia fulani fulani ambapo lazima âtujiongezeâ.
Leo nimekuhadithieni maneno âuchawiâ na âmchawiâ. Nimesema hayakustahili kuingizwa katika Biblia kama yalivyoingizwa. Yamekosewa. Matokeo yake, yanawapotosha na kuwatia ubishi watu wengi.
Hali kadhalika, nimedokeza kwamba kuna maneno mengine ya mkasa wa aina hiyo hiyo, hususan maneno YEHOVA na JINI. Ni mambo ya kuelimishana na wala tusione haya kuulizana tunapokwama kuielewa Biblia maana elimu haina mwisho na kusoma sana siyo mwisho wa ujinga.
Yule afisa Mwitheopia aliposhindwa kuelewa maneno ya Nabii Isaya aliyokuwa anayasoma, hakuona haya kujieleza kwa Filipo akisema, âNitawezaje kuelewa bila mtu kuniongoza?â (Mdo 8:31). Filipo alijitolea kumwelewesha naye akaelewa. Natumaini njia ya afisa yule inaweza kuwa njia yetu pia. Tusione haya kuulizana mambo ya Biblia. Karibuni wote!
Credit: Padre Titus Amigu.
Dhana ya kupinga kinachoitwa Uchawi au Ushirikina, amekiandika kwenye kitabu chake kinaitwa 'Jinsi ya kuushinda Ulimwengu'. Nlikisoma miaka 13 iliyopita. Ishakuwa kitambo ila nakumbuka vizuri allivyoandika kwenye kitabu chake. wakati huo pia nilisoma kitabu chake kingine kinaitwa ' Maswali wanayobandikwa wakatoliki' Mle kachambua hoja moja baada ya nyingine kuhusu Ukatoliki. Huyu Padre huwa haamini kama kuna uchawi Duniani.Mkatiliki mie. Namsikiliza sana Fr. Titus sawa ni mtauhidi mzuri kwa maana ya fani hiyo ndani ya Kanisa Katoliki. Anaelewa lugha mama ya Maandiko Matakatifu. Lakini asisahau kuwa hata Afrika au uswahilini zipo taaluma zote hizo kama za mamajusi, waongea na wafu, mazingaombwe, nk na kuna shule za kujifunza hayo kwa namna rasmi (formal) na isiyo rasmi (informal).
Kusema kwamba hayo mambo yanayoitwa uchawi kwenye Biblia ilikuwa taaluma lakini katika mazingira ya uswahili sio taaluma sio kweli.
Wachawi walikuwepo kwenye biblia na uchawi wao sio less evil ukilinganisha na uchawi kwa dhana ya Kiswahili. Wale wachawi wa Misri hawakubadili fimbo zao kuwa nyoka kwa kutumia ujuzi wa kisayansi ya binadamu, walitumia nguvu ya kipepo. Hayo hufanyika pia katika dhana ya uchawi ya Kiswahili.
Ambacho Pd. Amigu na wengine hukosea sana ni kutokuamini uwepo wa wachawi na uhalisia wao. Wengi wa hawa wanatheologia wasomi hufikiri ni ujinga kusema nimelogwa. Ulozi upo na hayo yote ni kazi za shetani katika madaraja mbalimbali.