Tiwa Savage: Mchepuko ulinidanganya, najuta kuvunja ndoa yangu, nampigia magoti mume wangu anisamehe

Tiwa Savage: Mchepuko ulinidanganya, najuta kuvunja ndoa yangu, nampigia magoti mume wangu anisamehe

Aman iwe kwenu akina mama na akina Baba wote wa jamiiforum

Huko kwa wakuitwa TIWA SAVAGE kimeumana

Baada ya mchepuko kumpiga sound naye akajaa leo ndo kaanza kulia Lia na kumkumbuka mume wake wa ndoa

---
Msanii maarufu wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage amesema anajutia kuachana na mume wake, Tunji Balogun maarufu kama Teebillz na kuanzisha uhusiano na mwanaume mwingine.

Msanii huyo amebainisha hayo wakati akifanya mahojiano na jarida la Elle South Africa na kusema hiyo ndio moja ya kosa kubwa ambalo amewahi kufanya.

"Nilimfanya mume wangu asijisikie kuwa mwanaume kwa sababu nilianza kutoka na mwanaume mwingine, bado nampenda na najua nilimkosea lakini nataka kurekebisha mambo na turudiane,” amesema

"Sina uhakika kuwa anaweza kunirudisha tena na sikuwahi kutaka kumpa talaka lakini mwanaume mwingine alinihadaa nimuache mume wangu niwe naye.”

Tiwa ameongeza kuwa sio rahisi mwanamke aliyemwacha mumewe kuolewa na mwanamume mwingine huku akiwasihi wanawake kutofanya alichokifanya.

Mwananchi
Majuto ni mjukuu
 
huyo asahau tu na kumsihi uyo mchepuko wake amuoe.
Unaoaje mwanamke aliemuacha mumewe at first place!!!

Kusoma hujui, hata picha usiione?

Hapo ni kujipigia kisha unapita hivi.
 
Back
Top Bottom