TKZ 2025: HESHIMA kwa Wazazi ni Lazima na Muhimu katika Maisha yako

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Kwa muda mrefu, nimekuwa natafakari juu ya tabia za watu (kama kiburi, uvivu, ulevi, wizi na kila aina ya utovu wa nidhamu) na athari zake katika familia zao na hata kwa Jamii, nikagundua kwamba mtu mwenye mafanikio ni yule anayewaheshimu Wazazi wake. Mtu anayewaheshimu Wazazi wake, haishii hapo, bali anaendeleza heshima hiyo shuleni, kazini, kwenye biashara, kwenye Jamii, nk. Na mtu wa namna hii anaheshimika kila eneo. Ukweli huu unathibitishwa na maandiko mbalimbali katika vitabu vya biblia na quran kama ifuatavyo:

Biblia
Kutoka 20:12
[12]Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

Mithali 13:1
[1]Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;
Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

Mithali 16:18-19
[18]Kiburi hutangulia uangamivu;
Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.

[19]Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini,
Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.

Mithali 26:13-14
[13]Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani,
Simba yuko katika njia kuu.

[14]Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake;
Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.

Yoshua bin Sira 3: 1 - 16
[1] Wanangu sikilizeni mawaidha ya baba yenu. Fanyeni ninayowaambia, nanyi mtawekwa salama,
[2] maana Bwana amewapa kina baba mamlaka juu ya watoto wao, na kuimarisha uwezo wa kina mama juu ya watoto wao.
[3] Anayemheshimu baba yake anajipatia msamaha wa dhambi zake.
[4] Anayemheshimu mama yake anajiwekea hazina kubwa.
[5] Anayemheshimu baba yake atafurahishwa na watoto wake mwenyewe, na atakapomuomba Bwana, atasikilizwa.
[6] Anayemheshimu baba yake atapata maisha marefu, anayempendeza mama yake anamtii Bwana.
[7] Mtoto huyo huwatumikia wazazi wake kama Bwana wake.
[8] Mheshimu baba yako kwa maneno na matendo, ili upate baraka kutoka kwake.
[9] Maana baraka za baba huimarisha nyumba za watoto, hali laana ya mama huing'oa misingi ya nyumba zao.
[10] Usijikuze mwenyewe kwa kumdharau baba yako, maana kumdharau baba yako hakutakuletea faida.
[11] Maana fahari ya baba mtu ni fahari ya huyo mtoto, na watoto wasiomheshimu mama yao ni balaa.
[12] Mwanangu, mtunze baba alipo Mzee wala usimhuzunishe muda wote aishipo.
[13] Hata akipungukiwa akili, umvumilie, usimdharau kwa vile wewe una afya na nguvu
[14] Bwana hatasahau wema wako kwa baba yako, utakusaidia kupata msamaha wa dhambi zako.
[15] Wakati wa taabu Bwana atakumbuka wema wako. Kama umande kwenye jua, dhambi zako zitatoweka.
[16] Anayemkufuru baba yake anamkufuru Mungu; anayemkasurisha mama yake analaaniwa na Bwana.
Waefeso 6:1-3
[1]Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
[2]Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,

[3]Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.

Quran
Hadith Za Mtume (s) Na
Ma Imamu (a) - 700-1710

Kuwahurumia Wazazi.

791. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 15, Uk. 176:

“Furaha ya Allah swt ipo katika furaha ya wazazi wa mtu (kama ndio hivyo ni kweli, basi adhabu na ghadhabu zake pia zipo katika ghadhabu za wazazi wa mtu).”

792. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 85:

“Bora ya matendo ni:
1. Kusali kwa wakati wake,

2. kuwa mwema na mwenye huruma na mwenye mapenzi kwa wazazi wake, na

793. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Safinat-ul-Bihar,J. 2, Uk. 553:

“Iwapo mtu anataka Allah swt ampunguzie makali ya mauti, basi lazima awajali Jama’a na ndugu zake, na awawie wema wazazi wake. Na pale mtu anapofanya hivyo, basi Allah swt atampunguzia makali ya mauti na kamwe hatapata umaskini katika maisha yake.”

794. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Usul-i- Kafi, J. 2, Uk. 349:

“Yeyote yule anayewatazama wazazi wake kwa macho ya ghadhabu, hata kama wao hawakuwa waadilifu kwake, basi Allah swt hatazikubalia ibada za mtu huyo (hadi hapo atakapofanya Tawba).”

795. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 5, Uk. 554:

“Watendee wazazi wako kwa huruma ili na watoto wako waje wakutendee vivyo hivyo; na uwe mcha Allah swt kwa wake wa watu wengine ili wake zako wabakie wacha Allah swt.”

796. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 2, Uk. 162:

“Safari moja mtu alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwuliza namna ya kuwashughulikia wazazi. Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimjibu
1. uwe mwenye huruma kwa mama yako:

2. uwe mwenye huruma kwa mama yako na

3. uwe mwenye huruma kwa mama yako;

4. Uwe mwenye huruma kwa baba yako

5. uwe mwenye huruma kwa baba yako; na

6. uwe mwenye huruma kwa baba yako lakini huruma hiyo uianzie kwa mama yako kabla ya baba yako.”

Hitimisho
Katika Jamii yoyote, ikitokea mtoto anafanya vitendo vibaya, watu huanza kuuliza, huyu ni mtoto wa nani au anatoka familia ipi? Kumbe tabia nzuri au mbaya huanzia nyumbani.

Pamoja na ukweli kwamba ni jukumu la watoto kuwaheshimu Wazazi kama ilivyoelezwa hapo juu, Wazazi au walezi Wana jukumu kubwa la kuwalea, kuwapatia mahitaji na huduma zote za msingi, na kuwafundisha watoto maadili ya kuishi katika familia na Jamii; badala ya kuachia ile kauli ya "Mtoto asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na Ulimwengu" ifanye kazi.

Watu wenye heshima iliyoelezwa katika makala hii, wanaunda Familia Bora, Jamii Bora, na taifa Bora lenye watumishi na viongozi weledi na waadilifu katika sekta na ngazi zote.

© Constantine J.S. Mauki
January 2025
 
Waambie hao wenye shingo ngumu, pengine utawasaidia
 
Mzazi bazazi naye aheshimiwe kwa sababu mzazi tu?

Umeweka logical fallacies za appeal to authority na appeal to tradition.
 
Back
Top Bottom