Uchaguzi 2020 TLP kuwa chama kikuu cha Upinzani maana yake nini? Je, ni mifumo ya nchi haitaki Upinzani wa kukosoa na kuamua kutengeneza upinzani wa kuchonga?

ABC ZA 2025

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2018
Posts
1,299
Reaction score
832
WanaJF salaam,

Nimekuwa kimya kidogo kuwapatia ABC za 2020; hii ni kutokana na majukumu mengi ya Kitaifa.

Najua mnajua kinachoendelea nchini hasa kwa upande wa Upinzani serious ambao ni Chadema na ACT-Wazalendo.

Ukweli ni kwamba dola halifurahishwi na namna Upinzani Tanzania unavyoendeshwa mtakumbuka hata Rais wakati analikihutubia Bunge alisema watakaorudi ni wale wanaovaa kijani ambao ni CCM.

Mpaka sasa chama pekee kilichojitokeza kumuunga mkono Rais Magufuli hadharani ni TLP chini ya Mwenyekiti wake Kachero mbobezi Lyatonga Mrema, kwa msiofahamu Mrema ni Mtu Wa TISS tangu enzi.

TLP kwa sasa imesajili vijana makini sana wanaoendesha Siasa zao Kisasa sana tofauti na ilivyokuwa hapa awali nadhani hili sote tunaliona.

Mkakati nyuma ya haya yote ni kuhakikisha kunakuwa na Wabunge/Madiwani Wa CCM Wa aina mbili.

1. Wabunge/Madiwani Wa CCM kupitia CCM.

2. Wabunge/Madiwani Wa CCM kupitia TLP.

Tafiti zinaonesha CCM itakuwa na Wagombea 4 katika kila kata ya Uchaguzi watakaomnadi Rais Magufuli ambao ni hawa wafuatao;-

1. Wagombea 2 toka CCM ambao ni Mgombea Ubunge na Udiwani.

2. Wagombea wawili toka TLP ambao ni Mgombea Ubunge na Udiwani.

Sasa wapinzani jipimeni nafasi yenu iko wapi kwenye Uchaguzi mkuu huu?

Kuna siku Polepole aliwahi kusema CCM itatawala kwa miaka 100 ijayo kwa mikakati hii naanza kuamini.

Baada ya kura za maoni kumalizika CCM usishangae Wagombea toka CCM ambao hawajafanikiwa kuitetea CCM kupitia CCM halisi watatumia jukwaa la TLP kuitetea CCM yao na wakimaliza kazi utashangaa wakipewa UDC na Ukuu wa Mikoa. Stay tuned.

Ni mimi tu kuwaleteeni habari hizi.
 
Mrema na mbatia na lipumba washaingizwa king CCM ikishinda basi chadema ndo itakuwa main opposition party kwani Magufuli ninani hapa Tz au unadhani watu wanowaogopa police?
 
Huu mwaka kama unataka Ubunge au Udiwani nenda CCM ukishindwa kupenya nenda TLP

Siasa za Bongo ni full unafiki. Hakuna uchaguzi Oct watu watapeana maviti tu
 
Mrema na mbatia na lipumba washaingizwa king ccm ikishinda basi chadema ndo itakuwa main opposition party kwani Magufuli ninani hapa Tz au unadhani watu wanowaogopa police ?




Subutu Chadema hata kiti kimoja hakuna labda ACT Zanzibar
 
Hii aina mpya ya upinzani inayoasisi na hiki chama huenda ikawa bora zaidi katika kulilinda Taifa letu

Kama sio ukibaraka basi Mrema anastahili tuzo kwa hili analolifanya sasa
 
TANZANIA LABOUR PARTY CHAMA KIKUU CHA UPINZANI, KHAAAAA LEO SIANDIKI KITU HAPA ILA UCHAGUZI HUU LOLOTE LAWEZA TOKEA,
 
Sawa tu...maana vyama vingine vya upinzani vimekuwa ni vikaragosi vya mabeberu...Kama ni hivyo Basi mkakati was kufanya TLP kuwa chama kikuu Cha upinzani ni sawa tu...hata hivyo najua pia kuwa habari hii haina ukweli wowote..
 
Kama huu mpango ni kweli basi naweza sema tuna TISS dhaifu kuliko zote duniani.

Nchi yeyote ikitaka upinzani moderate basi wanachukua vijana makini wa TISS na kuwapandikiza hadi wafikie level ya maamuzi kwenye vyama yaani kamati kuu. Ssa hapo wanafumua kila kitu kuanzia sera mpaka itikadi mbona simple tu.

Kajifunzeni kwa museveni wote tunajua kinara wa upinzani pale alipandikizwa kitambo ili siku akikataliwa na wananchi basi ashinde mtu wa kabila lake yaani Besigye/Mbabazi!!

Ila hii ya kulazimisha chama fulani kuwa ndio upinzani ili tu kiwe moderate kwa serikali bila kuweka misingi ya kuaminika kwa wananchi haitozaa matunda. Nadhani mnaona ilivyofeli huko visiwani kwa kina Hamad Rashid
 
Magufuli anatambua mshindi ni yule anayetangazwa na tume ya uchaguzi, siyo anayeshinda kwa kura. Hutaki nanda mahakamani ukakutane na ccm nyingine kule, hutaki fanya fujo ukutane na jeshi la ccm utakiona cha moto.
We all know all governments organs belong to ccm, sasa kwanini isiwe hivyo?!
 





NAOMBENI KADI YA TLP NA NAWEZAJE KUGOMBEA UDIWANI KUPITIA TLP HAPA MAFINGA MJINI?
 
Anaepata faida ni nani? mwananchi mnyonge au Mnyika au Mbowe aliyevuna 2Bilioni tokea awe mwanasiasa? au anaekomolewa ni nani? wananchi mnyonge au Mbowe? au neno CHADEMA?
WaTanzania siku akili ikiwakaa sawa mtajua kua mnyonyaji mkubwa wa nchi hii ni katiba yetu.

Chukulia kua viongozi wote wa CHADEMA wakaamua kujiunga na ccm au TLP je hiyo ccm itaanza kupambana na wananchi wanyonge au itakaa kimya?
 
Pumba tupu,eti TLP ina Vijana makini na wanaendesha siasa kisasa,pytuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…