Uchaguzi 2020 TLP Updates: Fahamu Mambo matano (5) kati ya ishirini na moja (21) yanayoisukuma zaidi TLP kumuunga Mkono Mhe Dkt. John Magufuli kuelekea Okt 2020

Ninavyokujua najua umeunga mkono bila hata kusoma. Kitendo cha kuona tu TLP, na neno Magufuli, huku ukijua TLP ni mchepuko wa ccm m, usingejisumbua kusoma zaidi ya kuunga mkono hoja.
tindo Tlp wamedadavua vizuri sana. Na ndio ukweli unaofanya JPM akubalike.
 
tindo Tlp wamedadavua vizuri sana. Na ndio ukweli unaofanya JPM akubalike.

Hata wazungu wa Afrika kusini walikuwa na wadadavuzi wazuri kuliko TLP, lakini hilo halikufanya weusi wasidai haki zao. Tunataka tume huru ya uchaguzi, kila mtu apate haki yake stahiki toka kwa wapiga kura. Sio hiyo tume inayotii utashi wa rais aliye madarakani.
 
Hicho ni kisingizio cha wapinzani baada ya kujua mmeshashindwa. Tume ipo huru ndio maana taratibu zote huwa zinafuatwa ikiwemo kubandika matokeo na kuweka mawakala kila kituo na ngazi zote husika.
 
Ile ya mwenyekiti board ya parole Ni point ngapi?
 
Hicho ni kisingizio cha wapinzani baada ya kujua mmeshashindwa. Tume ipo huru ndio maana taratibu zote huwa zinafuatwa ikiwemo kubandika matokeo na kuweka mawakala kila kituo na ngazi zote husika.

Sibahatishi ninachokuambia boss. Hiyo tume ni sehemu ya kuchezea matokeo.
 
Sio kweli unachofanya ni kuhalalisha uongo.

Tulishaamka boss muda mrefu. Hizo siasa za rais kutumia madaraka yake kunajisi uchaguzi tulishatoka huko. Haya majibu hata uniamishe usiku wa manane, siwezi kuyabadili.
 
Tulishaamka boss muda mrefu. Hizo siasa za rais kutumia madaraka yake kunajisi uchaguzi tulishatoka huko. Haya majibu hata uniamishe usiku wa manane, siwezi kuyabadili.
Siasa za kiaswahili.
 
Hapa ndiyo WATOTO wa Mjini niliwasikia wakisonya "Upinzani huo kwioooo"
 
Hii nimeipenda kumbe kwa sasa katika kila kituo kimoja cha kutolea huduma za afya (Hospitality,Zahanati,Kituo cha afya...)kama watanzania wote 55M tutaugua kwa siku moja basi kila kituo kitahudumia wagonjwa 17 tu ,


#Tano tena kwa JPM,
Did you factor in uwepo wa wataalamu na vifaa? Au majengo ndio service? Pia proximity ya vituo ipoje?
 

Kama ni taarifa rasmi ya TLP ni vema kuweka kwenye pdf alafu isainiwe ili tujue kama kweli
Ila sasa inawezekana hata msemaji wa chama akawa hakuna ndio maana mnaficha utambulisho wenu.
pili ni vema kwenda kwa Msajili mkaombe usajili wenu ufutwe tu maana nyie mmesajiliwa kufanya kazi ya siasa,kwa kueneza falsafa na itikadi yenu,kama.hakuna hiyo basi nyie ni wafu na hakuna haja ya kujaza daftari la msajili wakati mmekufa!

Nikishajua kama ni taarifa rasmi basi ntawajibu kwa facta
 
Ingependeza mngeingia kabisa huko ccm

Ova
 
TLP viongozi hamuungwi mkono hata na familia zenu Chama hakina hata mbunge mmoja wa kuchaguliwa na wananchi! Munamuunga mkono kwa sababu 2 kubwa.

1. Mupate fadhila za uteuzi
2. Kuficha aibu ya kupata kura 2000 Tanzania nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…