TLS inaweza kukata rufaa Mahakama ya Rufaa dhidi ya ushindi wa Mwambukusi kabla ya uchaguzi? Je, uchaguzi utasimamishwa kusubiri rufaa au utaendelea?

TLS inaweza kukata rufaa Mahakama ya Rufaa dhidi ya ushindi wa Mwambukusi kabla ya uchaguzi? Je, uchaguzi utasimamishwa kusubiri rufaa au utaendelea?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kwa huku iliyotolewa leo tarehe 26/07/2024 je TLS na Serikali wanaweza kukata Rufaa? Endapo watakata rufaa uchaguzi utaendelea au utasogezwa mbele kusubiri maamuzi?

Hongera Mwambukusi kura yangu unayo baada ya kusikia matamanio yako ya utekelezaji s. 4.

Nimefurahi pia kwamba umekubali kuwa unaopambana nao siyo wale wajumbe wa kamati wanaoonekana bali ni vivuli vilivyo nyuma ya mfumo. Je, ukiingia ofisini utapambana na hao waliotangaza wewe kuenguliwa au utapambana na mfumo?

Kumbuka wanachama wako wa TLS wana chama kingine cha serikali na ndicho kinachopambana na TLS ili kiwe na nguvu TLS ife. Mawakili waliopo kwenye vyama viwili hivi vya kitaaluma unawaambiaje?
 
Sidhani kama TLS wataka rufaa, hofu waliyokuwa nayo mwanzo kumhusu Adv. Mwabukusi iliyowafanya wakate jina lake, ilikuja kuondolewa na wale waliokuwa wakipigania jina la Adv. Mwabukusi lirudishwe kwenye orodha ya wagombea.

Naandika hivyo kwasababu, wakati wakina Kibatala na wenzake wakitaka Adv. Mwabukusi arudishwe kugombea, at the same time walisema wazi hawatampigia kura, hiki kitendo kikitosha kuiondoa hofu serikali na TLS.

Nasema kiliwaondoa hofu kwasababu naamini watawala walijua, kumbe yule wanayemtilia shaka hana ushawishi sana miongoni mwa wapigakura kama walivyokuwa wakidhania.

Sijui huko TLS kura sio siri huwa zinapigwa wazi? kama ni siri, kwanini wakina Adv. Kibatala wakatamka wazi hawatampigia kura Adv. Mwabukusi? kwa hii hatua yao hawakuvunja kanuni zozote za uchaguzi huko TLS? kama walivunja, adhabu yao ni ipi?
 
Sidhani kama TLS wataka rufaa, hofu waliyokuwa nayo mwanzo kumhusu Adv. Mwabukusi iliyowafanya wakate jina lake, ilikuja kuondolewa na wale waliokuwa wakipigania jina la Adv. Mwabukusi lirudishwe kwenye orodha ya wagombea.
Yani Mwambukusi na Lissu watakuwa walizaliwa tumbo moja ni wabishi sana halafu wamenyooka!
 
Huyu mwabukusi kura ndizo zitatoa majibu, kwann tunampa kisa kama yy ndio mpanga matokeo
 
Back
Top Bottom