Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
(FULL VIDEO IPO CHINI)
Leo tarehe 5 Oktoba 2024, mawakili wote wa Tanzania bara, hasa wa jijini Dar es Salaam, wanakutana katika jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, ili kujadili suala la utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania. Tukio hili la kitaifa linaandaliwa na Tanganyika Law Society (TLS) na limehudhuriwa na wanachama wa TLS pamoja na wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.

Lengo kuu la kongamano hili ni kujadili hatua za kisheria, historia ya matukio haya, na mikakati ya kuzuia na kuwajibisha wahusika, sambamba na kuangalia namna ya kuwasaidia waathirika na familia zao.
Tukio hili ni la umuhimu mkubwa katika kulinda haki za binadamu na kupambana na vitendo vya upoteaji wa raia nchini.
Kongamano linaanza rasmi saa 03:00 asubuhi na litakuwa mubashara kupitia uzi huu pamoja na Wakili TV kwenye YouTube kwa wale ambao hawawezi kuhudhuria.

MATUKIO
Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Bi Mariam Othman akifanya ufunguzi na kuwakaribusha wageni waalikwa katika kongamano la kujadili "Matukio ya kupotea kwa Raia Nchini Tanzania"
“Hatutakiwi kufanya uchaguzi tukiwa tumebeba bunduki, tunatakiwa kubeba ilani na karatasi ya kupigia kura”.- Raisi wa TLS, Wakili Boniphace Mwabukusi afanya ufunguzi wa mjadala juu ya Matukio ya Kupotea kwa Raia.
“Kila tarehe 30 August ni siku ya Kimataifa ya kukumbuka wahanga waliopotezwa kwa nguvu. Tatizo hili sio la Tanzania tu bali ni Dunia nzima, ila wenzetu wamekubali tatizo lipo na wanatoa rekodi kila mwaka za watu waliopotezwa kwa nguvu. Tafiti za mwaka 2021 zimeonyesha Afrika kesi nyingi zipo nchi za Algeria (3,253), Egypt (289), Burundi (250), Sudan (177), Morocco (153) na Ethiopia(113). Kwa Tanzania hakuna taarifa rasmi za watu kupotezwa kwa nguvu lakini TLS imepokea orodha isiyo rasmi matukio 84 ya watu kupotezwa Tanzania”.
“Tunashauri kila mwaka tarehe 30 Agosti hapa Tanzania kuwepo na maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kukumbuka wahanga waliopotezwa kwa nguvu ili tukumbushane kwamba hili ni tatizo na tukubali kwamba tatizo lipo na tulitafutie majawabu” - Jaji mstaafu Makaramba
“Sheria ya ugaidi inampa haki askari kukamata bila kuwa na hati ya kukamatia, hivyo kuongeza matukio ya utekaji” - Shekhe Ponda.
“Katika kuchunguza masuala ya watu kupotea, tumekuwa tukipendekeza mara nyingi kuwa watu wanaotuhumiwa kuhusika na matukio hayo wasichunguze matukio hayo, maana mtu anayetuhumiwa ni rahisi sana kujipendelea wakati wa uchunguzi, inatakiwa kuundwa kamati huru ambayo itachunguza matukio hayo kwa uhuru bila kupendelea"
"Masuala ya uchunguzi ya kesi za watu kupotea zinatakiwa kuwa wazi kwenye hatua zote na hii inaweza kuwa njia nzuri ya ufuatiliaji wa matukio haya.” - Wakili Paul Kisabo, kutoka mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

“Moja ya jukumu la Jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama kwa watu, na Sec. 5(2) ya Tanzania Police Service Act inatoa jukumu la uchunguzi pale watu wanapopotea”.
“Kwa rekodi ya polisi watu 37 waliokumbwa na kadhia ya kutekwa tangu 2018 uchunguzi ulikamilika ikiwepo kufikishwa mahakamani kwa watuhumiwa na wengine walikutwa wamekufa”. - Kamanda Muliro

#WakoWapi #TLSSymposium #UtekwajiNaUpoteaji