(LIVE VIDEO IPO CHINI)
Leo tarehe 5 Oktoba 2024, mawakili wote wa Tanzania bara, hasa wa jijini Dar es Salaam, wanakutana katika jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, ili kujadili suala la utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania. Tukio hili la kitaifa linaandaliwa na Tanganyika Law Society (TLS) na limehudhuriwa na wanachama wa TLS pamoja na wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.
Lengo kuu la kongamano hili ni kujadili hatua za kisheria, historia ya matukio haya, na mikakati ya kuzuia na kuwajibisha wahusika, sambamba na kuangalia namna ya kuwasaidia waathirika na familia zao.
View attachment 3115940
Tukio hili ni la umuhimu mkubwa katika kulinda haki za binadamu na kupambana na vitendo vya upoteaji wa raia nchini.
View attachment 3115938
Kongamano linaanza rasmi saa 03:00 asubuhi na litakuwa mubashara kupitia uzi huu pamoja na Wakili TV kwenye YouTube kwa wale ambao hawawezi kuhudhuria.
Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Bi Mariam Othman akifanya ufunguzi na kuwakaribusha wageni waalikwa katika kongamano la kujadili "Matukio ya kupotea kwa Raia Nchini Tanzania"
View attachment 3115943
“Hatutakiwi kufanya uchaguzi tukiwa tumebeba bunduki, tunatakiwa kubeba ilani na karatasi ya kupigia kura”.-
Raisi wa TLS, Wakili Boniphace Mwabukusi afanya ufunguzi wa mjadala juu ya Matukio ya Kupotea kwa Raia.
#WakoWapi #TLSSymposium #UtekwajiNaUpoteaji