Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Tanganyika Law Society (TLS) imeandaa kongamano la kitaifa litakalojadili ongezeko la matukio ya watu kupotea na kutekwa nchini Tanzania. Kongamano hili litafanyika tarehe 5 Oktoba 2024 saa 3:00 asubuhi maenoe ya Wakili House, Chato Street, Mikocheni A, Dar es Salaam.
View: https://youtu.be/sYFFLcEP-T4?si=tPzpuqhhwg17pvev
Uamuzi wa kuandaa kongamano hili umechochewa na kuongezeka kwa ripoti za raia wanaotekwa au kupotea bila maelezo ya kutosha kutoka kwa vyombo vya dola kama Polisi na Bunge. Hali hii imeibua maswali mengi kuhusu usalama wa raia na utendaji wa mamlaka husika katika kutafuta na kutoa haki.
Mwanasheria Adv. Salha Rashid, ambaye ni mmoja wa waandaaji wa kongamano hili, anasema kuwa lengo ni kuwaleta pamoja wanasheria, wanaharakati wa haki za binadamu, wawakilishi wa serikali, na wananchi kwa ujumla kujadili na kutafuta suluhisho la tatizo hili linalozidi kuleta hofu miongoni mwa wananchi. Kongamano hili linatarajiwa kutoa mapendekezo ya sera na sheria ili kukabiliana na hali hii na kuongeza uwajibikaji wa vyombo vya dola.
Tukio hili litarushwa mubashara kupitia uzi wa “LIVE: TLS-kongamano la kitaifa kujadili matukio ya utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania”
Kwa maelezo zaidi au kushiriki, unaweza kuwasiliana na Adv. Salha Rashid kupitia barua pepe srashid@tls.or.tz
View: https://youtu.be/9cwvlPAHDbA?feature=shared

PIA SOMA: