TLS kuandaa kongamano la Kitaifa kuhusu matukio ya kutekwa na kupotea kwa raia nchini Tanzania

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318

Tanganyika Law Society (TLS) imeandaa kongamano la kitaifa litakalojadili ongezeko la matukio ya watu kupotea na kutekwa nchini Tanzania. Kongamano hili litafanyika tarehe 5 Oktoba 2024 saa 3:00 asubuhi maenoe ya Wakili House, Chato Street, Mikocheni A, Dar es Salaam.

View: https://youtu.be/sYFFLcEP-T4?si=tPzpuqhhwg17pvev
Uamuzi wa kuandaa kongamano hili umechochewa na kuongezeka kwa ripoti za raia wanaotekwa au kupotea bila maelezo ya kutosha kutoka kwa vyombo vya dola kama Polisi na Bunge. Hali hii imeibua maswali mengi kuhusu usalama wa raia na utendaji wa mamlaka husika katika kutafuta na kutoa haki.

Mwanasheria Adv. Salha Rashid, ambaye ni mmoja wa waandaaji wa kongamano hili, anasema kuwa lengo ni kuwaleta pamoja wanasheria, wanaharakati wa haki za binadamu, wawakilishi wa serikali, na wananchi kwa ujumla kujadili na kutafuta suluhisho la tatizo hili linalozidi kuleta hofu miongoni mwa wananchi. Kongamano hili linatarajiwa kutoa mapendekezo ya sera na sheria ili kukabiliana na hali hii na kuongeza uwajibikaji wa vyombo vya dola.

Tukio hili litarushwa mubashara kupitia uzi wa “LIVE: TLS-kongamano la kitaifa kujadili matukio ya utekwaji na upoteaji wa raia nchini Tanzania”

Kwa maelezo zaidi au kushiriki, unaweza kuwasiliana na Adv. Salha Rashid kupitia barua pepe srashid@tls.or.tz



View: https://youtu.be/9cwvlPAHDbA?feature=shared

PIA SOMA:
 
Heko Mwabukusi kwa uongozi bora TLS haya ndio mambo watanzania wanataka.
 
Ngoja inyeshe tuone panapovuja
Tungekuwa mbali sema Mialimu ya hii nchi inaturudisha nyuma kazi kuiba kura tu.

Yakute sasa mtaan yakishastaafu yanavolia njaa na kikokotoo.

Lakn bado hayakomi yanaiba tena kura mmq
 
Kuna mtu humu aliwahi kuliza kam TLS chini ya mwabukusi ni chama cha wanasheria au chama cha kiharakati kwa mambo ya siasa na cjui alikuwa anamanisha nini
 
Bro tupe views za upande wako, wewe unaonaje mkuu?​
Kwakweli mmi kuna muda ananichanganya kuna wakati TLS inaendeshwa kiharakati, kuna mda ana ongea fact, pia kuna mda naiona kama chama cha siasa ….. generaly naweza sema TLS ya mwabukusi ni motoooooo
 
Kwa jinsi ninavyoijua nchi hii, 'Watekaji' watalipiga vita kali kongamano hili mpaka lishindwe kufanyika. Ngoja tuone!
 
Kwakweli mmi kuna muda ananichanganya kuna wakati TLS inaendeshwa kiharakati, kuna mda ana ongea fact, pia kuna mda naiona kama chama cha siasa ….. generaly naweza sema TLS ya mwabukusi ni motoooooo
😂Mimi nakuelewa kwanini unaona ivyo. Unajua nini, Mwabukusi yeye alisema TLS chini yake itakua katika msingi wa Section 4 (Yani kifungu cha 4) cha sheria iliyoanzisha TLS. Sasa kifungu hicho kinaeleza majukumu na malengo ya TLS,

sitaki kukirejea kifungu hicho ila ukipata wasaa wa kukipitia utagundua majukumu ya TLS yanagusa nyanja zote ikiwemo masuala ya kisiasa, uharakati na menginenyo kwa maslahi ya umma kwani ni kama jeshi la kisheria linalolinda maslahi ya wanachama wake na umma kiujumla katika masuala ya kisheria​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…