TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Kama kiapo hakikaimishwi...maana yake viongozi wote walioapa kwa rais aliyepita wataapa tena?,au ni kwa mawaziri tu kiapo ndo hakikaimishwi?
Ni kwa mawaziri tu sababu rais asipokuwepo waziri mkuu cheo chake kinakoma na pia Baraza la mawaziri.
Ndio maana term ya pili ya JPM aliwaruhusu wateule wengine waendelee ila alichagua waziri mkuu na Baraza jipya la mawaziri na kuwaapisha
 
TLS ni wapumbavu sana wanawapotosha majuha humu ndani. Katiba inasema kabisa baada Rais kufa au kuondoka madarakani kwasbbu yote ile basi makamu wa Rais atamalizia kipindi kilichobaki bila uchaguzi kufanyika. Meaning hapo hakuna Serikali mpya anaendelea alipoishia mtangulizi wake.

Wala haikusema pia Rais akifa na Serikali yake inakufa inabidi iundwe upya. Very simple logic lakini humu wamejaa mazumbukuku wanapelekeshwa tu.
 
Joined Yesterday ! wewe ni mchanga sana kupambana na sisi wakubwa wako , hebu pata uzoefu kwanza halafu urudi tena
Mkuu ni mambo tu mkuu!! Ni kweli I'd hiyo ni juzi lkn huwenda nipo hapa miaka mingi kulikoni wewe mkuu,
 
Kufuatia sheria za nchi zinavyotueleza kutokana na katiba ya JMT Je itamlazimu Rais wa Kuapishwa kuvunja baraza lote?
Vipi kuhusu Mwanasheria Mkuu wa.serikali itabidi amchague mwingine je KMK itabidi amchague mwingine au inakuwaje? Nakama leo kaongea na baraza la mawaziri inamaanisha atavunja baraza kama katiba inavyomuelekeza??Je kama kiapo akirisishwi vipi maDC na RC watatakiwa kuapa upya kumbuka hili nitukio la kwanza kufariki kiongozi wa nchi akiwa madarakani!

Je atateua tena wabunge 10 kama katiba inavyoeleza?toa maoni kwangu naona tunahitaji katiba mpya.

Hebu tuwasikilize wataalamu washeria nchini wanasemaje!
 

Nina wasiwasi sana na ukweli wa tafsiri hii ya TLS; imejikita katika mazingira yanayohusu rais wa kuchaguliwa kuliko mazingira ya rais anayechukua madaraka baada ya kifo cha rais aliyekuwa amechaguliwa. Nikiangalia Serikali ya Marekani baada ya Kennedy kuuwawa na makamu wake Johnson kuchukua madaraka ya kuongoza serikali kwa kipindi kilichobaki, hakukuwa na mabadiliko ya baraza la mawaziri zaidi tu ya mabadiliko ya Rais na Makamu wa Rais.

Katiba yetu pia inatoa mwongozo kuwa rais akifariki, basi nafasi ya rais itachukuliwa na aliyekuwa Makamu wa rais halafu yeye kwa kushirikiana na chama chate watapendekeza mtu wa kujaza nafasi ya makamu wa rais ambaye atahibitishwa na bunge halafu serikali itaendelea kama mwanzo. Sasa hawa wanasheria wanatoa tafasiri inayoaminisha watu kuwa rais akifariki, basi inakuwa kama kumefanyika uchaguzi mpya kabisa na aliyekuwa makamu wa rais ameshinda uchaguzi huo automatically jambo ambalo si kweli.

Of course rais yeyote aliyeko madarakani ana mamlaka ya kubadili baraza la mawaziri wakati wowote, na hivyo Mama Samia Suluhu Hassan anaweza kubadili baraza lote na mwaziri hadi waziri mkuu kutokana na madaraka yake aliyo nayo kikatiba, lakini mabadiliko hayo siyo automatic kuwa baada ya rais kufariki basi serikali inakuwa ombwe, kama inavyotokea baada ya uchaguzi.

Wataalamu wetu hawa sheria wakati mwingine wanasema vitu vya ajabu sana, mostly wanasoma katiba wakiwa na mindset fulani. Ni aibu sana kwa body ya sheria kutoa tafsiri ya katiba ambayo iko twisted na shallow namna hiyo.
 
Wako sahihi, rais Samia anapaswa teua mpaka mwanashera mkuu wa serikali upya, bila kusahau katibu mkuu kiongozi...
Kw
Hiki cha leo ni kama kikao cha kupiga stori tu maana as long as the PM is not legit basi hakuna baraza la mawaziri
Hawa TLS wanaaibisha taaluma yao! Tukiwachekea watatuingiza kwenye mgogoro wa kikatiba!!
 
Mawazo yako ni kama yangu jirani.

Mama Samia alikuwa makamu wa Rais wa serikali hii hii. Umakamu wake huo wa Rais ulikuwa na maana gani kama si continuity of government endapo Rais aliyekuwepo hatokuwepo tena?

Na ndo maana atamalizia muhula wa Rais aliyekuwepo madarakani.

Sasa kama kwenye muhula anaanzia pale ambapo Magufuli kaishia, kwa nini sehemu zingine za serikali zisiendelee na kazi kama kawaida? Manake hatokuwa Rais kwa miaka 5 kamili. Atakuwa Rais kwa takriban miaka 4.5.

Huo uchambuzi wa TLS haujanishawishi kabisa.

Ku complicate mambo pasipo na sababu.
 
Nini kazi ya TISS ni ku contro sio ku controliwa sasa ianze upya yenyewe yaani duu mpaka iliye mchuja anaijua na kuianika adharani hata kutoa siri za mchakato ni aibu kubwa
Kisheria hata kolokoloni(bawaba)anambinu za kulinda nyumba ya tajiri mpaka uchawi anatumia lakini tajiri hapaswi kujua na haimuhusu
 
Nadhani hizi ni tafsiri endelevu..

Kichwa cha treni kikifa ukileta Kipya na mabehewa yote yanabadilishwa...

Mwingine no mabehewa yaleyale haina shida....

Ni ok kuamini watabadilishwa...
Na ni ok kuamini hawatabadilishwa... haiji serikali mpya.. ila kiongozi wa juu anakuwa crowned...

Hakuna kiapo serikalini kinasema kumtii Magufuli Bali kumtii Raisi...

Tusije ambiwa hata wakuu wa mikoa na wilaya wataapishwa upya...
Mimi naona katiba yetu inakanganya sana..!, sasa kama hivi ndivyo mbona Rais leo alikuwa na kikao na hilo baraza la mawaziri?? Litaitwaje baraza la mawaziri na automatically wanapaswa kiteuliwa upya na kuapa ndio kuwe na mawaziri??
 
Hao jamaa wanadhani kuwa kwa vile wao ni wanasheria basi wanaweza kutudanganya kirahisi rahisi
 
Kwa maana hiyo hata hawa kina Pole pole walioteuliwa kuwa wabunge na rais Magufuli nao inatakiwa wasiwe wabunge tena?

Hapa hawa TLS inaonekana nao hawana wanachojua
Pumbafu wewe rudia Tls walicho sema ni mwongozo wa ushauri tena wameambatanisha na katiba siyo lazima kama wewe pangu pakavu tia mchuzi una
Sawa.

Lakini hakuna mahali panaposema waziwazi kuwa rais mpya akila kiapo basi baraza zima la mawaziri nalo linavunjika, siyo?

Umenielewa?
Vipi wewe ndugu unaona mkia wa Ngombe unauliza kinyeo kiko wapi?

Tumia ufahamu kidogo mnauita lojiki
 
Hiki cha leo ni kama kikao cha kupiga stori tu maana as long as the PM is not legit basi hakuna baraza la mawaziri
Siyo kweli, hawa TLS nadhani wanaandaa mazingira ya kubahatisha jamaa zao kuingia kwenye baraza la mawazi. Tusiwape nafasi, ili mradi wamechemsha mwanzoni itatusaidia huko mbele, vinginevyo watasumbua na kuyumbisha Sana!
Ukweli ni kwamba mazingira ya urais kama huu, katiba inamtaja makamu wa Rais tu kukumbwa na mabadiliko yanayodaiwa na katiba: 1. Makamu wa Rais kuapishwa na kuwa Rais kwa kipindi kilichobaki kwenye miaka mitano. 2. Rais kuteua jina akishirikiana na Chama chake ili baada ya kuthibitishwa na binge awe makamu wa Rais.
Katiba haijasema chochote kuhusu nafasi zingine. Maana yake ni kuwa Rais mpya ameachiwa maamuzi yake mwenyewe! Akiamua kuuvunja baraza lote kwa mamlaka yake kama Rais na kuliunda upya ni sawa! Akiamua kubadilisha baadhi ya mawaziri hata viongozi wengine waandamizi ni sawa pia. Akiamua kuendelea na baraza lile lile kwa sasa ni sawa pia!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…