TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Kinachonifanya niamini kwamba mama Samia Suluhu ataliunganisha taifa ni kitendo chake cha kwenda Nairobi (kwa uamuzi wake binafsi) kumuona Tundu Lissu kipindi aliposhambuliwa na "watu wasiojulikana" mchaba kweupe jijini Dodoma. Kuna taarifa kwamba baada ya uamuzi huo wa kijasiri alilaumiwa sana na wenzake ndani ya serikali kwa "usaliti" lakini alisimama imara bila kutetereka.
 
Mawazo yako ni kama yangu jirani.

Mama Samia alikuwa makamu wa Rais wa serikali hii hii. Umakamu wake huo wa Rais ulikuwa na maana gani kama si continuity of government endapo Rais aliyekuwepo hatokuwepo tena?....
Nyani Ngabu Mimi Nadhani Serikali haijavunjika kumetokea mabadiliko ya nafasi ya Rais kutokana na matakwa ya kikatiba.

Mama Samia sio "President Elect" au Rais Mteule, ni Makamu aliepata Urais kwa kifo cha Rais Mtangulizi.

Rais Mteule hupatikana baada ya uchaguzi.Hapo ndio ungebidi kuunda upya.

Kwa sasa Hakuna haja ya kiapo kipya. Ni Serikali Inaendelea.
 
Hizi loopholes kwenye katiba zimekaa kimkakati, kimakusudi ama bahati mbaya?

Ni mitego ya hatari na rahisi sana kutumika/kutafsirika kwa mujibu wowote na ‘wahusika!’

Naendelea kujifunza....
 
Aisee.
Kumbe Kina Makonda wanaweza kurudi kivingine.

Hata wapinzani kama Mbowe, Mbatia au Lisu nao wanaweza kuwa wabunge wa kuteuliwa na Rais mpya kisha nchi ikawa shwaaaaaari.
 
Wanasheria mmeitendea haki taaluma yenu. Safi sana.

Sio watu wa afya wanaambiwa kuwa Corona inaisha kwa kujifukiza, nao wanaishiwa mapozi.
 
Huu ni upotoshaji uliolenga kitu fulani.

1. Eti rais anapofariki au anaposhindwa kumudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili, baraza la mawaziri linakuwa limevunjika na hivyo makamu wa rais baada ya kuapishwa kuwa rais anawajibika kuunda baraza la mawaziri jipya!

Hii ni kinyume kabisa na katiba. Rais akifariki baraza la mawaziri ambalo alikuwa akiliongoza halivunjiki bali linashikamana zaidi. Makamu wa rais ni miongoni mwa baraza hilo na ataapishwa kwa mjibu wa katiba kuchukua nafasi hiyo ya kuliongoza baraza hilo kwa kipindi kilichobakia.

Rais anaposhindwa kumudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili baraza la mawaziri halivunjiki bali linashikamana zaidi na ndilo linaanzisha mchakato wa makamu wa rais kupewa kiti hicho kwa kumuarifu jaji mkuu ili aunde jopo la madaktari kuthibitisha lililomtokea rais ili hatimaye makamu wa rais aapishwe kumalizia kipindi kilichobakia.

Hivyo katiba iko wazi kabisa kwamba makamu wa rais ataapishwa kuwa rais kumalizia kipindi kilichobakia. Kipindi kilichobakia kinaweza kuwa cha siku chake au miezi fulani au miaka fulani. Ni kipindi kilichobakia kwenye awamu hiyo. Hatuanzishi awamu nyingine. Kuna wengine wanafikiri kwamba sasa tunaanza awamu ya sita, si kweli hata kidogo. Bado tunaendelea na awamu ya tano ya hapa kazi tu hadi 2025.

2. Tusichanganye na masuala ya rais kuondolewa madarakani kwa impeachment au kujiuzuru. Haya utaratibu wake wa kikatiba nao uko wazi. Hapa ndipo bunge lote pamoja na baraza la mawaziri linavunjika. Kinachofuata ni uchaguzi mkuu mpya kupata serikali mpya na bunge jipya.

3. TLS kutoa miongozo kwa serikali, haya madaraka wameyatoa wapi? Halafu miongozo yenyewe kwa serikali inatolewa hadharani. Hapa kunatia wasi wasi wa alichokipandikiza Tundu Lissu pale TLS.

TLS kama tasisi zingine zinaruhusiwa kutoa ushauri kwa serikali kuhusiana na mambo mbali yanayohusu taifa letu. Lakini kwa kawaida ushauri makini huwa una utaratibu wake wa namna ya kuutoa kwa serikali, na kwa kawida huwa umeombwa.
 
Mama samia ukitaka ufanye kazi, kwakuwa Baraza linavunjika basi huna budi ya kuteua Baraza la mawaziri litakalokusaidia ili ufike mbali zaidi, ukianza na waziri wa katiba na Sheria, wa madini, hata waziri mkuu tumekosa imani naye, anatudanganya ndani ya nyumba ya ibada kwamba rais ni mzima na anachapa kazi, kumbe rais alishafariki kitambo!
 
Nimesoma mwongozo wa chama cha mawakili wa Tanganyika na majibu ya waziri wa katiba na sheria na kuona pasipo na shaka kuwa nyuma yake kuna viashiria vya kuliipa kisasi kwa serikali iliyokuwa inaongozwa na JPM. Aidha wanaona kuingia kwa mama Samia ni fursa kwao kulipa kisasi kwa baadhi ya watu ambao kwa maoni yao hawakuwapenda, hawapendi na wangetamani kuwaona wanatoka kwenye utendaji wa serikali.

Watanzania tunaumizawa na sheria nyingi ambazo wao wamekuwa hawatolei mwongozo na imeshangaza kidogo uharaka katika hili la waziri mkuu na baraza la mawaziri.

Walichofanya ni matumizi mabaya ya taakuma kwa maslahi binafsi
 
Ni wajibu wao kutoa ushauri kwa viongozi wa nchi na kutafsiri vifungu vya sheria kulingana na katiba ya nchi.

Kama kuna mahali wameeleza kinyume na katiba sema hapa tujue wote.

Otherwise wewe ni mwendawazimu.
 
Rais mteule? Samia alikuwa Rais mteule? Seriously?
Labda kwa concept ya kwamba wanakuwa voted kwa pamoja na rais wakati wa uchaguzi, ingawa bado inaleta ukakasi pia.

Kwa maoni yangu nadhani katiba ingetamka kuwa ikitokea sababu yoyote inayofanya kiti cha urais kuwa wazi kabla ya kumaliza muhula wake, tume ya taifa ya uchaguzi ingekuwa inamtangaza kwanza VP kama 'President elect' kabla ya kula kiapo.

All in all, jambo hili na mengine mengi ambayo yamekuwa yakizua sintofahamu na migogoro ya kikatiba ni justification tosha kuwa tunahitaji katiba mpya kwa kweli kama tunataka kujenga jamii iliyo staarabika kwa maana ya 'Good Governance'.
 
Kuna watu ambao ushauri unawagusa wanakuja kujihami kivingine,"hoja hujibiwa kwa hoja"!
 
Rais nikiongozi mwenye mamlaka kamili hakuna nguvu hatamoja alionayo kikatiba kwasabu ile au hii iliyopunguzwa sasa Natamani kujuwa rais aliofariki aliteuwa wabunge je nawasasa anaweza teuwa wengine nawale walioteuliwa inakuaje iwapo itaonekana anyohaki yakuteuwa naomba nijibiwe kwa mujibu wa katiba
 
TLS ni kiungo muhimu sana kwa ustawi wa Taifa letu, haswa ukizingatia kwa nyakati kama hizi ambapo bunge letu limekuwa 'bubu'.

Nawaombea afya njema na baraka tele kutoka kwa Mungu Mwenye Enzi, daima msitetereke.
Pia Limekuwa BUTU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…