Na Gerson Msigwa alisema dhahiri Rais ataongoza kikao cha viongozi waandamizi bila kutaja waandamizi wa nini.Kile kilikuwa kikao cha washauri siyo baraza la mawaziri, kule ndani nilimuona Dr. Abbas, Dotto na wengine
Wewe siyo tu unafuatilia,ila unataka kusoma/kusikia kile unachotaka wewe,uhuru wa mawazo haupo kichwani mwako hata chembeMjadala huu mtamu sana watu wanauliza vifungu kwenye katiba vinavyosema kuhusu waziri mkuu Rais aliye madarakani anapo fariki!
TLS hoja zao zinazua maswali sana na ni assumptions tuu!
Maana kuna maana kubwa kama kwenye muktadha husika katiba inaponyamaza kuhusu waziri mkuu!
Mbona kwa Vice iko wazi kabisa? Hata kama katiba yetu ina mapungufu wasingeliweza sahau swala la PM kama kweli linahitaji kwenye muktadha tulionao!
Kuna maana kubwa sana katiba kutosema chochote kuhusu PM!
Mimi niko hapa nafatilia uzi huu nipewe vifungu.
Ni kweli. Pengine huyu mama atasikiliza kilio cha katiba mpya na uchaguzi ujao tutakuwa nayo. Mradi tu asikubali kusikiliza ''makombo ya Magufuli'' yaliyobaki. Na aanze kuifumua TISS yote. Ni aibu sana kumwacha rais kufa kwa covid wakati ishara zilikuwa wazi kabisa baada ya wasaidizi wake wa karibu kufa. Magufuli alikuwa mjeuri lakini ni nini kazi ya TISS?
Wametajwa kikatiba
Lala tu,umeandika ujinga tena!!Law interpretation ya ajabu kabisa hii. Utasemaje hakuna Baraza la Mawaziri wakati halijavunjwa? Halafu kifungu mlichoquote kina husiana na kuunda Baraza likiwa limevunjwa. Someni vizuri Katiba na kuitafasiri vizuri.
Umeambiwa na Nani Kara na COVID-19. Hivi nyie Nani ataweza kuwaongoza Kama kila kitu mnajua.
Kwahiyo wote walioapa mbele ya rais wanapaswa kutoka kwenye nafasi zao sasa?TLS hawajui sheria au katiba ni mbovu, wao TLS wameweka vifungu vya sheria ndani ya katiba, ww unawapinga kwa hisia za uzalendo uchwara na mifano irrelevant. Hao akina Polepole huo ubunge wameapa mbele ya rais au kwa spika? Siasa za kutegemea madaraka ya rais bila kufuata katiba ndio yanawatesa. Halafu mkiambiwa katiba ina mapungufu ifanyiwe mabadiliko, hamtaki mnaona mtatoka madarakani!
We katiba ishasema baraza la mawaziri linavunjika pale raisi mpya anapokula kiapo.Well, hiyo katiba inasema waziwazi kuwa endapo Rais aliyepo madarakani anaacha kuwa Rais kwa sababu yoyote ile, ikiwemo kifo, basi baraza la mawaziri nalo linavunjika?
Manake kama haisemi waziwazi, inaacha mwanya wa kutafsirika ki namna mbalimbali.
Mambo kama hayo inapaswa yatamkwe waziwazi na katiba pasipo kuacha mwanya au mianya ya tafsiri.
Kwahio ummejikubali kuwa ninyi ni mataga??Kwanini usiweke kifungu kilichovunjwa?
Na kwanini unasubiri kigogo awaze badala yako?
Mataga hawamini kitu gani?
Kwamfano hebu weka kifungu walichoweka TLS na kwamba kimekiukwa
Ngoja niisome taratibu!
Nilichoelewa ni kwamba hadi sasa hatuna baraza la mawaziri kwa sababu hawa akina Mwigullu Nchemba waliapishwa na Rais Magufuli ambaye ni marehemu kwa sasa!
Lakini, kwa mkutadha huu, nikwamba. Mawaziri wanapaswa kuapa kwa rais aliyeko madarakani! Sasa hawa waliapa kwa rais Magufuli!! hivi wakula kiapo cha utii kwa nani? si rais aliyeko madarakani.
Wanasheria wako sawa!!
Ndio maana wameambatanisha vifungu vingi. Kumbuka hata mwenyekiti wa tume ya uchanguzi, wakati anamtangaza Magufuli, alitumia vifungu zaidi ya kimoja kuharalisha hio mamlaka yake!!
Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Hiyo katiba ni so outdated hilo halina mjadala, hata hivyo kwenye hiyo katiba hao viongozi uliowataja wamepewa hayo majukumu kikatiba, au ni utaratibu umefanyika sasa kutokana na kutokufahamu katiba? kumbuka hapa hatuongelei viongozi wa juu, bali ni rais kufariki akiwa madarakani. Hao mawaziri watoke ofisini kwa mujibu wa katiba, ili wasimuwekee mama Kiwingu wakati wa kuunda baraza jipya la mawaziri. Kama ni kuingia kwenye hizo kamati za mazishi, waingie kama watu maalum na sio kama mawaziri.
Kikao kile kwa mujibu wa katiba ni batili, ifahamike hali hii ni mara ya kwanza kutokea kwenye nchi hii, na uzoefu unaonyesha watu wengi ikiwemo viongozi, huwa hawajui katiba inasemaje bali huendesha nchi kwa mazoea. Kumbuka hata rais Samia juzi alitangaza maombolezo ni siku 14, wakati kikatiba ni siku 21, na leo amerekebisha kosa lile.
Jambo baya kupita yote hata Muhimili wa mahakama haujui mambo haya, na huwa mahakama inasubiri viongozi waseme na wao ndio watekeleze. Kama jambo haliwauzi viongozi, basi mahakama hutekeleza kwa kufuata utashi wa viongozi.
Hapo hao wanasheria wameweka kifungu chochote kwamba rais akifa na balaza la mawaziri linakufa kweli? Kipo hicho kifungu?Mfano wa kitu gani, nirudie kilichowekwa na wanasheria? Hujaelewa kipi kilichowekwa na vifungu vya katiba mpaka mimi nirudie? Ww endelea na uzalendo uchwara wa kusikiliza viongozi wapika data wanaosema rais ni mzima na anachapa kazi, kwakuwa sisi tunalishwa matango pori na kigogo.