TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Ni jambo geni lakini mwanasheria wa Serikali alipaswa kulijua. Shida bado watu wana ule uoga na hofu waliyojengewa kwa miaka mitano bado upo, wanaogopa hata kutoa ushauri
 
Napinga mwongozo huu uliotolewa na TLS, ingawa mimi si mwanasheria nahisi wameisoma hiyo katiba kwa kuharakisha, na wana bias.
  1. Kwanza si jukumu, wajibu wala haki ya TLS kutoa mwongozo kama huo. Kwa mujibu wa hiyo TLS Act aliyonukuu Rais wa TLS, jukumu (role) la TLS ni kutoa ushauri (advice), sio mwongozo (guidance).
  2. Wajibu (responsibility) wa kutoa mwongozo kama huo ni wa mwanasheria mkuu wa serikali, ndio maana kila inapoingia serikali mpya madarakani mtu wa kwanza kuteuliwa kabla ya wengine wote ni mwanasheria mkuu wa serikali.
  3. Katiba haijamwelekeza rais aliyepata madaraka kwa mtindo huu aliopata Mhe Samia kuteua waziri mkuu mpya wala kuvunja baraza la mawaziri. Wala katiba haisemi kuwa kifo cha rais kinasababisha automatic cessation ya uwepo wa baraza la mawaziri. Rais mpya anayo haki ya kuvunja baraza la mawaziri na kuliunda upya, lakini halazimiki kufanya hivyo, katiba haisemi hivyo.
  4. Leo mojawapo ya kazi alizofanya Rais Mama Samia ni kuongoza kikao cha baraza la mawaziri. TLS inataka kutuambia kuwa Mh Rais ameongoza baraza "hewa"?
  5. Nimemuona na kumsikia Rais wa TLS hapo kwenye video akisema kuwa kiapo hakirithiwi, kwamba kila aliyeapa kwa rais aliyepita kiapo chake hakihusiki kwa rais mpya. Sikubaliani naye. Anamaanisha viongozi kuanzia ngazi ya kitaifa (mawaziri, makatibu wakuu) hadi halmashauri (DEDs) walioteuliwa na kuapa kwa JPM, eti inawapasa kurudia viapo vyao sasa kwa Samia kwa kuwa JPM hayupo?
  6. Nawaomba TLS watofautishe kati ya kuunda serikali mpya baada ya uchaguzi ambapo viongozi wa kuchaguliwa wanakuwa wamemaliza muda wao, na kupokea serikali iliyokwishaundwa tayari. Hapo kiongozi mpya anayelazimika kuteuliwa kikatiba ni makamu wa rais tu, wengine rais anaweza kuwabadilisha katika utaratibu wa kawaida wa mabadiliko kama ambayo mtangulizi wake angefanya, na kila anayebadilishwa ndiye anayepaswa kuapa upya kwa nafasi mpya.
Haya, nimejilipua kubishana na wanasheria, nitupieni mawe!
 
Kile kilikuwa kikao cha washauri siyo baraza la mawaziri, kule ndani nilimuona Dr. Abbas, Dotto na wengine
Na Gerson Msigwa alisema dhahiri Rais ataongoza kikao cha viongozi waandamizi bila kutaja waandamizi wa nini.
 
Mjadala huu mtamu sana watu wanauliza vifungu kwenye katiba vinavyosema kuhusu waziri mkuu Rais aliye madarakani anapo fariki!

TLS hoja zao zinazua maswali sana na ni assumptions tuu!
Maana kuna maana kubwa kama kwenye muktadha husika katiba inaponyamaza kuhusu waziri mkuu!

Mbona kwa Vice iko wazi kabisa? Hata kama katiba yetu ina mapungufu wasingeliweza sahau swala la PM kama kweli linahitaji kwenye muktadha tulionao!

Kuna maana kubwa sana katiba kutosema chochote kuhusu PM!

Mimi niko hapa nafatilia uzi huu nipewe vifungu.
Wewe siyo tu unafuatilia,ila unataka kusoma/kusikia kile unachotaka wewe,uhuru wa mawazo haupo kichwani mwako hata chembe
 
Ni kweli. Pengine huyu mama atasikiliza kilio cha katiba mpya na uchaguzi ujao tutakuwa nayo. Mradi tu asikubali kusikiliza ''makombo ya Magufuli'' yaliyobaki. Na aanze kuifumua TISS yote. Ni aibu sana kumwacha rais kufa kwa covid wakati ishara zilikuwa wazi kabisa baada ya wasaidizi wake wa karibu kufa. Magufuli alikuwa mjeuri lakini ni nini kazi ya TISS?

Umeambiwa na Nani Kara na COVID-19. Hivi nyie Nani ataweza kuwaongoza Kama kila kitu mnajua.
 
Wametajwa kikatiba

Nitajie kifungu kinachoonyesha hayo majukumu inapotokea rais aliyeko madarakani akiwa amefariki. Watu wa TLS mje mtoe ufafanuzi wa hili suala la huyu Mheshimiwa.
 
Law interpretation ya ajabu kabisa hii. Utasemaje hakuna Baraza la Mawaziri wakati halijavunjwa? Halafu kifungu mlichoquote kina husiana na kuunda Baraza likiwa limevunjwa. Someni vizuri Katiba na kuitafasiri vizuri.
Lala tu,umeandika ujinga tena!!
 
Nanai amevunja Baraza likilokuwepo la mawaziri? Katiba inasemaje kuhusu kuvunjwa kwa Baraza la mawaziri
 
Umeambiwa na Nani Kara na COVID-19. Hivi nyie Nani ataweza kuwaongoza Kama kila kitu mnajua.

Wanaotakiwa kusema ukweli ndio hao wanasema rais ni mzima anachapa kazi, mwingine anatokea anasema hizo siku rais alikuwa anaumwa! Wakati huo huo mitandaoni inasemekana rais kashakufa, baada ya mashinikizo ndio serikali inakiri rais kafariki. Kwanini watu wasiendelee kuamini yasemwayo mitandaoni badala ya kusikiliza hekaya za wenye mamlaka?
 
TLS hawajui sheria au katiba ni mbovu, wao TLS wameweka vifungu vya sheria ndani ya katiba, ww unawapinga kwa hisia za uzalendo uchwara na mifano irrelevant. Hao akina Polepole huo ubunge wameapa mbele ya rais au kwa spika? Siasa za kutegemea madaraka ya rais bila kufuata katiba ndio yanawatesa. Halafu mkiambiwa katiba ina mapungufu ifanyiwe mabadiliko, hamtaki mnaona mtatoka madarakani!
Kwahiyo wote walioapa mbele ya rais wanapaswa kutoka kwenye nafasi zao sasa?
 
Well, hiyo katiba inasema waziwazi kuwa endapo Rais aliyepo madarakani anaacha kuwa Rais kwa sababu yoyote ile, ikiwemo kifo, basi baraza la mawaziri nalo linavunjika?

Manake kama haisemi waziwazi, inaacha mwanya wa kutafsirika ki namna mbalimbali.

Mambo kama hayo inapaswa yatamkwe waziwazi na katiba pasipo kuacha mwanya au mianya ya tafsiri.
We katiba ishasema baraza la mawaziri linavunjika pale raisi mpya anapokula kiapo.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Kwamfano hebu weka kifungu walichoweka TLS na kwamba kimekiukwa

Mfano wa kitu gani, nirudie kilichowekwa na wanasheria? Hujaelewa kipi kilichowekwa na vifungu vya katiba mpaka mimi nirudie? Ww endelea na uzalendo uchwara wa kusikiliza viongozi wapika data wanaosema rais ni mzima na anachapa kazi, kwakuwa sisi tunalishwa matango pori na kigogo.
 
Akiamua kuendana na team yake aliyonayo sasa kitakachifuata ni kuwatangaza upya na kuwaapisha...
Ngoja niisome taratibu!

Nilichoelewa ni kwamba hadi sasa hatuna baraza la mawaziri kwa sababu hawa akina Mwigullu Nchemba waliapishwa na Rais Magufuli ambaye ni marehemu kwa sasa!
 
Lakini, kwa mkutadha huu, nikwamba. Mawaziri wanapaswa kuapa kwa rais aliyeko madarakani! Sasa hawa waliapa kwa rais Magufuli!! hivi wakula kiapo cha utii kwa nani? si rais aliyeko madarakani.
Wanasheria wako sawa!!

Ndio maana wameambatanisha vifungu vingi. Kumbuka hata mwenyekiti wa tume ya uchanguzi, wakati anamtangaza Magufuli, alitumia vifungu zaidi ya kimoja kuharalisha hio mamlaka yake!!

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app

Hapa unaongelewa muktadha wa Rais aliye madarakani anapofariki .....!

Hivi unafikiri kwanini katiba haijasema chochote kuhusu waziri mkuu? Msiweke tafsiri ambayo haijaainishwa bali mseme vifungu
 
Hiyo katiba ni so outdated hilo halina mjadala, hata hivyo kwenye hiyo katiba hao viongozi uliowataja wamepewa hayo majukumu kikatiba, au ni utaratibu umefanyika sasa kutokana na kutokufahamu katiba? kumbuka hapa hatuongelei viongozi wa juu, bali ni rais kufariki akiwa madarakani. Hao mawaziri watoke ofisini kwa mujibu wa katiba, ili wasimuwekee mama Kiwingu wakati wa kuunda baraza jipya la mawaziri. Kama ni kuingia kwenye hizo kamati za mazishi, waingie kama watu maalum na sio kama mawaziri.

Hebu twambia katiba imesema wapi kuhusu hao mawaziri unaosema watoke? Hebu tueleze vifungu kabisa
 
Kikao kile kwa mujibu wa katiba ni batili, ifahamike hali hii ni mara ya kwanza kutokea kwenye nchi hii, na uzoefu unaonyesha watu wengi ikiwemo viongozi, huwa hawajui katiba inasemaje bali huendesha nchi kwa mazoea. Kumbuka hata rais Samia juzi alitangaza maombolezo ni siku 14, wakati kikatiba ni siku 21, na leo amerekebisha kosa lile.

Jambo baya kupita yote hata Muhimili wa mahakama haujui mambo haya, na huwa mahakama inasubiri viongozi waseme na wao ndio watekeleze. Kama jambo haliwauzi viongozi, basi mahakama hutekeleza kwa kufuata utashi wa viongozi.

Weka vifungu vya katiba vilivyo vunjwa tafadhali
 
Mfano wa kitu gani, nirudie kilichowekwa na wanasheria? Hujaelewa kipi kilichowekwa na vifungu vya katiba mpaka mimi nirudie? Ww endelea na uzalendo uchwara wa kusikiliza viongozi wapika data wanaosema rais ni mzima na anachapa kazi, kwakuwa sisi tunalishwa matango pori na kigogo.
Hapo hao wanasheria wameweka kifungu chochote kwamba rais akifa na balaza la mawaziri linakufa kweli? Kipo hicho kifungu?

Alafu kwa nini umepanic sana? Haya ni maisha tu hata nyie chadema mkijipanga iko siku mtashika madaraka labda 2300 huko
 
Back
Top Bottom