TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

11. Usomaji wa pamoja wa ibara ya 51(2) na ibara ya 57(2)(e) unatufanya tuseme, kwa kujiamini kabisa, kuwa mara tu baada ya Raisi kuapishwa kuwa Raisi anatakiwa kumteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14 tokea kuwa kwake Raisi. Waziri Mkuu aliyepo wadhifani anahesabika kutokuwa Waziri Mkuu na hivyo Baraza la Mawaziri linakuwa limevunjika kutokana na Waziri Mkuu kutokuwepo “kwa sababu nyingine yoyote”. Sababu nyingine yoyote ni “kufariki kwa Raisi aliyemteua na kusimikwa Raisi mpya ambaye siye aliyemchagua.”
pakaywatek , hilo ndio hitimisho la TLS. Unakubaliana nalo?
 
Nikafikiri unaweka vifungu kumbe unaleta ngonjera.

Mna shida sana nyie watu

Nikuwekee kifungu kwani mimi ni Jebra Kambole au Jaji Mkuu? Ungeweka kifungu ww nione utetezi wako uliojikita kwenye vifungu. Wataalamu wa sheria ni nafasi yao kutaja vifungu, mimi nadeal na fani nyingine huo muda wa kujua katiba kila kifungu kwa kichwa nautoa wapi?

Kama makamu wa rais alitangaza hapo mwanzo kuwa maombolezo ya rais ni siku 14, lakini leo kabidili kuwa siku 21 kuendana na katiba baada ya kuambiwa na wanasheria, ndio itakuwa mimi na vifungu vya katiba?
 
Kwanini hivyo vipengele mnavyotaka vitumike ni kwa mawaziri tu wakati kuna wengi tu wameteuliwa na rais na kuapa mbele yake?
Bado unauliza maswali yako ya kipimbi? Kwa hiyo kama kuna wengi wameteuliwa na rais ndio ndio unahalalisha baraza la mawaziri? Mods hebu pigeni life ban hii pimbi inatuchefua tu hapa.
 
Utawala wa Huyu Rais haujakamilika kwa sababu hana makamu wa Rais ndiyo maana katiba inamtaka ndani ya siku 14 hawe ameteua makamu wa Rais. Hawezi vunja baraza kwa ssbabu inatakiwa ashauriane na makamu wake kuhusu waziri mkuu mpya hivyo baraza bado ni halali.
Havunji, linavunjika tu kwa PM kupoteza wadhifa wake. Kama nimewaelewa TLS
 
Nikuwekee kifungu kwani mimi ni Jebra Kambole au Jaji Mkuu? Ungeweka kifungu ww nione utetezi wako uliojikita kwenye vifungu. Wataalamu wa sheria ni nafasi yao kutaja vifungu, mimi nadeal na fani nyingine huo muda wa kujua katiba kila kifungu kwa kichwa nautoa wapi? Kama makamu wa rais alitangaza hapo mwanzo kuwa maombolezo ya rais ni siku 14, lakini leo kabidili kuwa siku 21 kuendana na katiba baada ya kuambiwa na wanasheria, ndio itakuwa mimi na vifungu vya katiba?
Achana na hiyo pimbi itakuchosha bure.
 
We umezungumzia kiapo wanachoapa.

Ni wapi kwenye katiba ambapo panasema Rais aliyepo madarakani akikoma kuwa Rais basi baraza la mawaziri nalo linavunjika automatically?
Baadhi ya sheria huwa zinasomwa kwa pamoja ili ziweze kufafanua jambo.
Katiba haiwezi andika na kufafanua Kila kitu ndio maana Kuna mahakama.
 
Kwa mujibu wa Katiba yetu kuapishwa kwa Rais Mpya kunamfanya Waziri Mkuu kupoteza wadhifa wake na pamoja naye Baraza zima la Mawaziri. Kwa sasa mchakato unatakiwa kufuata ni kwanza kumpata Makamu Mpya Rais, na akiisha apishwa Rais na Makamu wake wanakubaliana juu ya Waziri Mkuu. Ikumbukwe katika mazingira ya kawaida Rais na Makamu wake wanaingia pamoja.

Jambo la pili ni kuwa Mawaziri wote wanatumikia kwa ridhaa ya Rais (at the pleasure of the President). Sasa Rais aliyewapa ridhaa hayupo. Na hivyo ridhaa haipo. Hii ingekuwa hivyohivyo kama Magufuli angejiuzulu au angeondolewa na Bunge.
Hivyo:

1. Hakuna Waziri Mkuu Wala Mawaziri. Vyeo vyao vilikoma Rais Samia Hassan alipoapishwa tu. Wizara zote zinaongozwa na Najaribu Wakuu kama anapoapishwa Rais baada ya Uchaguzi. Kama hawana uhakika basi Rais atatangaza kuvunja Baraza la Mawaziri (siyo lazima kwani technically halipo)

2. Kilichofañyika leo ni Rais Mpya kukaa na kupeana pole na Mawaziri waliopita na labda kuwapa matarajio yake.

3. Mchakato wa kumpata Makamu wa Rais ndio unafanyika. Akipatikana taratibu zinafuatwa

4. Waziri Mkuu Mpya kutafutwa na Jina lake kutangazwa Bungeni baadaye kuapishwa mbele ya Rais. Majaliwa hajaapa mbele ya Samia kiapo Cha utii. Ni kweli kwa Mawaziri wote wengine.

5. Akishapatikana Waziri Mkuu (anaweza kuwa Majaliwa) ndio anashauriana na Rais kuunda Baraza la Mawaziri. Viapo vinafuata. Teuzi nyingine zinafanywa baadaye.

Hii Ina maana wateuliwa wote ambao nafasi zao ni kwa ridhaa ya Rais hadi dada zimeota mbawa isipokuwa Rais atoe agizo la kuwathibitisha hadi vinginevyo.

Urais wa Mzalendo Magufuli umekoma; Mhula wake wa pili ndio haujakoma. Imeanza awamu ya sita na Rais ni wa sita.
 

Mkuu kwanza nikupongeze wangalau kwa kuleta hata hii evidence. Hata hivyo hivyo vipande vya sheria vimebase kwenye viongozi wa kitaifa, nataka sehemu specific ya kamati za mazishi ya kitaifa ya rais aliyeko madarakani. Sibezi jitihada zako maana nimeona kabisa umekuja na kitu, japo bado hakijalenga vizuri kwenye mada inayobishaniwa. Big up sana.
 
Mwana K siku 14 hazijaisha. Ndio kwanza kaapishwa leo tutegemee makamu wa raisi na badae PM.
Kitu cha kujua hapa ni kwamba PM ni yule yule ndio maana Ndugai kaita wabunge Dodoma na mpaka sasa wabunge wapo Dodoma wanakula posho kusubiria kuwaidhinisha DP na PM.
 
Mkuu kwanza nikupongeze wangalau kwa kuleta hata hii evidence. Hata hivyo hivyo vipande vya sheria vimebase kwenye viongozi wa kitaifa, nataka sehemu specific ya kamati za mazishi ya kitaifa ya rais aliyeko madarakani. Sibezi jitihada zako maana nimeona kabisa umekuja na kitu, japo bado hakijalenga vizuri kwenye mada inayobishaniwa. Big up sana.
Kwa hiyo unataka niibebe yote nikupe? nipe mda nakuletea sehemu yote inayoongelea mazishi ya viongozi.
 
Well, hiyo katiba inasema waziwazi kuwa endapo Rais aliyepo madarakani anaacha kuwa Rais kwa sababu yoyote ile, ikiwemo kifo, basi baraza la mawaziri nalo linavunjika?

Manake kama haisemi waziwazi, inaacha mwanya wa kutafsirika ki namna mbalimbali.

Mambo kama hayo inapaswa yatamkwe waziwazi na katiba pasipo kuacha mwanya au mianya ya tafsiri.
Mkuu Nyani Ngabu,

Kuna ambayo yameandikwa na yasiyoandikwa.
Sasa kwa kuwa yasiyoandikwa yanatutatiza, busara inatuelekeza tufuate yaliyoandikwa;
Baada ya Raisi kuchukua madaraka atafanya ..........
Swali la kujiuliza, je ni kweli Rais wa Tanzania, mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan amechukua madaraka?
Kama ndiyo, basi na atende kama katiba aliyoapa kuilinda inavyomuongoza.
 
Back
Top Bottom