TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS kwa mara ya kwanza nimeona mmetekeleza wajibu wenu wa kisheria kwenye nchi hii. Mawaziri wote ikiwemo waziri Mkuu inabidi waambiwe, na wasiendelee kutokea kwenye nafasi zao kwani kwa sasa hakuna baraza la mawaziri. Nimemuona Majaliwa akiendelea kutambulishwa kama waziri Mkuu, wakati kikatiba hana uhalali huo. Tungekuwa na vyombo vya habari vinavyotekeleza wajibu wao walipaswa kulitangaza hili wazi wazi kuwa kwa sasa hakuna baraza la mawaziri, na waziri yoyote aliyekuwa kwenye baraza lililopita asiendelee kuingia ofisini au kutumia mali za ofisi kama gari nk, wakati hana uhalali huo.
Tatizo MaCCM yamejimililisha nchi, nakuifanya ya chama kimoja.
Wanajifanyia mambo kinyume na katiba.
 
Mkuu kwanza nikupongeze wangalau kwa kuleta hata hii evidence. Hata hivyo hivyo vipande vya sheria vimebase kwenye viongozi wa kitaifa, nataka sehemu specific ya kamati za mazishi ya kitaifa ya rais aliyeko madarakani. Sibezi jitihada zako maana nimeona kabisa umekuja na kitu, japo bado hakijalenga vizuri kwenye mada inayobishaniwa. Big up sana.
Kwa hoja hii TLS wapo sahihi pia hawapo sahihi kwa sababu wameegemea upande wa uundaji wa baraza la mawaziri wakaacha ukamilishaji wa taasisi ya urais kwanza.
 
Kwa hiyo unataka niibebe yote nikupe? nipe mda nakuletea sehemu yote inayoongelea mazishi ya viongozi.

Mkuu nimesema naheshimu mchango wako kwenye hili, na wala sibezi uwezo wako kwenye hili, ila vifungu ulivyoweka bado sio kwa suala lililoko mezani la kifo cha rais aliye madarakani. Kimsingi sibishani na ww, ila bado majibu hayajitoshelezi, ukiweza kuleta hicho kifungu/vifungu utakata mzizi wa fitina. Ila kama muda hautoshi, nimeheshimu mchango wako kwenye mada hii.
 
Kwahiyo hata wakuu wa mikoa wote aout? Mpaka rais awateue tena?

Kwa maana nyingine wateule wote walioapa mbele ya JPM wanapoteza nafasi zao hadi rais Samia ateue na kuwaapisha tena?
 
Kwa mantiki ya kawaida kabisa rais anapoapishwa anaunda serikali yake, na serikali ni mawaziri kwanza. Hao wengine anaendelea nao kadiri muda unavyoenda. Hata Magufuli alipoapishwa alianza kuteua mawaziri kwanza, kisha ndio alikuja kubadili katibu Mkuu Kiongozi, jaji Mkuu, IGP, CDF, wakuu wa mikoa, wilaya nk.

Hili halihitaji kujua sheria bali ni akili timamu na kuweza kupambanua mambo. Sasa ww unaleta ubishani ambao wala haukubebi bali unaonekana juha tu. Achana na hangover za siasa za uzalendo uchwara, hizi ni zama mpya na zina kitabu chake, unakwama wapi?
Hao TLS wametumia kifungu ambacho hakihusiana na Rais akifariki ama kushindwa kutekeleza majukumu ya urais. Vifungu walivyotumia ni vile vya Rais anayechukua madaraka kwa kufuata utaratibu wa kawaida. Tatizo la Baraza la TLS ni unaharakati ndiyo unawapotosha walipashwa kuisoma vizuri Katiba kwa umakini na burasa.
 
Mtabwatuka kila neno safari hii !
Ninachojua, wewe na wengine wengi, bado mtaendelea kuwa wapinzani msio na faida, au kunakitu unang'oja utakipata kwenye utawala huu mpya mkuu, ingawa na Mimi ni rasimi sasa natarajia kung'atuka huku niliko kwani kilichokuwa kinanifanya niendelee kuwako Ndo hivo tena, ushabiki wa mtu NAO unatabu yake

Nilikuwa mshabiki wa JPM pekee na si chama
 
Law interpretation ya ajabu kabisa hii. Utasemaje hakuna Baraza la Mawaziri wakati halijavunjwa? Halafu kifungu mlichoquote kina husiana na kuunda Baraza likiwa limevunjwa. Someni vizuri Katiba na kuitafasiri vizuri.
Rais anateua Mawaziri ili wamsaidie. Kama Rais aliyewateua hayupo ina maana nao hawana mtu wa kumsadia unless huyo aljaye awahitaji na awateue rasmi.
 
Hiyo imekaa sawa kwa hiyo wametimuliwa kikatiba angalia hao wengine waliotajwa tajwa wasirudi kabisaa wabaki bungeni kupiga makofi maana hakuna mradi wataweza kukagua hao...
 
Hao TLS wametumia kifungu ambacho hakihusiana na Rais akifariki ama kushindwa kutekeleza majukumu ya urais. Vifungu walivyotumia ni vile vya Rais anayechukua madaraka kwa kufuata utaratibu wa kawaida. Tatizo la Baraza la TLS ni unaharakati ndiyo unawapotosha walipashwa kuisoma vizuri Katiba kwa umakini na burasa.

Kwa mara ya kwanza leo umechangia nikakuelewa. Sasa usichoke, unaweza kuweka vifungu specific kuhusu utaratibu ukoje iwapo rais aliye madarakani anafariki? Hao TLS kama ni wanaharakati ama la hiyo ni mada nyingine. Hebu tutoe kwenye hili kwanza kisha hasira zako dhidi ya TLS utazionyesha tu.
 
Ninachojua, wewe na wengine wengi, bado mtaendelea kuwa wapinzani msio na faida, au kunakitu unang'oja utakipata kwenye utawala huu mpya mkuu, ingawa na Mimi ni rasimi sasa natarajia kung'atuka huku niliko kwani kilichokuwa kinanifanya niendelee kuwako Ndo hivo tena, ushabiki wa mtu NAO unatabu yake

Nilikuwa mshabiki wa JPM pekee na si chama
Joined Yesterday ! wewe ni mchanga sana kupambana na sisi wakubwa wako , hebu pata uzoefu kwanza halafu urudi tena
 
Rais anateua Mawaziri ili wamsaidie. Kama Rais aliyewateua hayupo ina maana nao hawana mtu wa kumsadia unless huyo aljaye awahitaji na awateue rasmi.
Raisi anateua mawaziri tu? Kwa hoja yako hiyo unamaanisha wateule wote wa raisi Kama wakuu wa mikoa, wilaya, Das,Ras nao wateuliwe upya?
 
Rais anateua Mawaziri ili wamsaidie. Kama Rais aliyewateua hayupo ina maana nao hawana mtu wa kumsadia unless huyo aljaye awahitaji na awateue rasmi.
Wanateuliwa kwa mujibu wa sheria na Baraza la Mawaziri linavunjwa kwa mujibu wa sheria lakini siyo kama hao Baraza la TLS wanavyotaka kutuaminisha.
 
Mkuu nimesema naheshimu mchango wako kwenye hili, na wala sibezi uwezo wako kwenye hili, ila vifungu ulivyoweka bado sio kwa suala lililoko mezani la kifo cha rais aliye madarakani. Kimsingi sibishani na ww, ila bado majibu hayajitoshelezi, ukiweza kuleta hicho kifungu/vifungu utakata mzizi wa fitina. Ila kama muda hautoshi, nimeheshimu mchango wako kwenye mada hii.
Chukua na hichi kipande uone waziri mkuu wadhifa wake unaisha lini
Screenshot_20210319-235938.jpg
 
Kama kiapo hakikaimishwi...maana yake viongozi wote walioapa kwa rais aliyepita wataapa tena?,au ni kwa mawaziri tu kiapo ndo hakikaimishwi?
Ngoja niisome taratibu!

Nilichoelewa ni kwamba hadi sasa hatuna baraza la mawaziri kwa sababu hawa akina Mwigullu Nchemba waliapishwa na Rais Magufuli ambaye ni marehemu kwa sasa!
 
Back
Top Bottom