TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Ukishasema hii ni serikali ya awamu ya 6 ina maana kuna mabadiliko ya serikali uliyoikuta. Ukirndeleza serikali ileile bila kuivunja inaonekana bado una kaimu Nafasi ya urais uliyemkuta....
Kama ni hivyo alitakiwa akae nao kabla hajaapishwa, ni lini uliona rais anayeondoka madarakani anaitisha kikao cha baraza la mawaziri baada ya uchaguzi kuisha?
 
Inatakiwa twende hivi kwa kila jambo la kisheria au kikatiba. tusizibe watu midomo
 
Hakika jambo hili litekelezwe kikamilifu, hongereni TLS kwa kuelekeza matakwa ya kikatiba kwamba yafuatwe, ni wajibu mh Rais kuheshimu katiba ambayo ameapa kwayo.
 
Hawa TLS mbona wanakuja kwa kasi hivyo, ama kweli jemedari ameumaliza mwendo
 
Lakini kwa kutizama mantiki tu. Kama PM akijiuzuru kunatosha kuvunjika kwa baraza la mawaziri, itakuwa kifo cha Rais?
 
Afadhali wizara ya afya ipate waziri
Wizara ya afya tuna majembe ya nguvu! Mabeberu walitaka kutulisha matango mwitu kwa kujibanza kwenye corona wakagonga mwamba!! Mama wa Afya songa mbele!! Walio wengi tunakuelewa na naibu wako tunamwelewa!!
 
Wamempoteza mama etu ...

Kavunja katiba x2

_kutangaza siku 14
_kuongea na baraza feki la wachumia tumbo
 
Hawa TLS mbona wanakuja kwa kasi hivyo, ama kweli jemedari ameumaliza mwendo
Hawa TLS tumewashtukia, wanataka kuifanya nchi yetu kuwa kama shamba la bibi! Wanaona sasa kila kitu kiko wazi watu waanze mishe mishe za kujichukulia nafasi.
 
Mawazo yako ni kama yangu jirani.

Mama Samia alikuwa makamu wa Rais wa serikali hii hii. Umakamu wake huo wa Rais ulikuwa na maana gani kama si continuity of government endapo Rais aliyekuwepo hatokuwepo tena?

Na ndo maana atamalizia muhula wa Rais aliyekuwepo madarakani.

Sasa kama kwenye muhula anaanzia pale ambapo Magufuli kaishia, kwa nini sehemu zingine za serikali zisiendelee na kazi kama kawaida? Manake hatokuwa Rais kwa miaka 5 kamili. Atakuwa Rais kwa takriban miaka 4.5.

Huo uchambuzi wa TLS haujanishawishi kabisa.

Ku complicate mambo pasipo na sababu.
Kiapo cha VP siyo kiapo cha President, ni viapo viwili tofauti kabisa

Katiba ibara ya 51(3)(a) inatamka wazi kuwa Waziri mkuu ataendelea kuwa waziri mkuu mpaka pale raisi mteule atakapokula kiapo chake cha urais.

Sasa aliyekuwa rais mteule baada ya kifo cha rais aliyeko madarakani jana kala kiapo, hii maana yake nafasi ya PM iko wazi and hence baraza zima la mawaziri halipo kwa sababu za kikatiba zinazosema kuwa pasipokuwepo na waziri mkuu basi hakuna baraza la mawaziri
 
Mzee umeongea haya kwa kutumia vifungu gani vya katiba na muktadha gani?
 
Kufuatia sheria za nchi zinavyotueleza kutokana na katiba ya JMT Je itamlazimu Rais wa Kuapishwa kuvunja baraza lote?
Vipi kuhusu Mwanasheria Mkuu wa.serikali itabidi amchague mwingine je KMK itabidi amchague mwingine au inakuwaje? Nakama leo kaongea na baraza la mawaziri inamaanisha atavunja baraza kama katiba inavyomuelekeza??Je kama kiapo akirisishwi vipi maDC na RC watatakiwa kuapa upya kumbuka hili nitukio la kwanza kufariki kiongozi wa nchi akiwa madarakani!

Je atateua tena wabunge 10 kama katiba inavyoeleza?toa maoni kwangu naona tunahitaji katiba mpya.

Hebu tuwasikilize wataalamu washeria nchini wanasemaje!View attachment 1729761View attachment 1729762View attachment 1729763
Hawa TLS naona hawakupata muda wa kutafakari. Wanadai kiapo akiamishiki, basi kama akiamishiki hata wao wengi wao mbona waliapishwa na baadhi ya majaji wakuu walioisha tangulia mbele za haki. Hivyo walitakiwa wale kiapo upya?
Kwa maelezo yao, Jaji mkuu, Mwanasheria Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu wote, ma RC na mabalozi wote, na wengineo wanaokula kiapo mbele ya Rais hawafai kwendelea na nafasi zao kama kiapo hakiamishiki kwa mujibu wa TLS.
TLS wanadai kuwa eti mbona waziri akibadilishwa wizara uapa tena. Kweli TLS wamekurupuka. Kiapo uapishwa kwa shughuli au kazi ambayo mteuliwa uenda kuifanya kwa mujibu wa sheria. Mfano waziri wa Mifugo uapishwa kama waziri wa mifugo. Akibadilishwa kuwa waziri wa Utalii ataapishwa kama waziri wa Utalii. Hivyo kiapo ulenga kazi halisi ndo maana uapishwa tena.
Katiba imeeleza wazi kuwa Makamu wa Rais ataapa kuwa Rais ni kwa sababu kiapo chake cha mwanzo aliapa kama Makamu wa Rais. Ndo maana uapishwa na kukagua gwaride la heshima akiwa Rais rasmi.
Anaposhika madaraka ya urais ni kuendeleza awamu ya serikali ili kumaliza kipindi cha miaka mitano. Huu si uchaguzi mpya.
Hata hivyo Rais anauwezo wa kuteua mawaziri au waziri mkuu kadri atavyoona inafaa. Yakiwa ni mabadiliko ya kawaida yanavyofanyika. Katiba haisemi kuwa baraza la mawaziri mara Rais anapokufa linavunjika la hasha.
Bali katiba imeeleza wazi ni mwendelezo wa serikali kumalizia miaka mitano ya serikali iliyochaguliwa.
Nasikitika TLS upande wa maelezo ya waziri mkuu wamenukuu ibara za katiba zinazoongelea uteuzi baada ya uchaguzi mkuu.
Hivyo si ukweli kuwa kiapo akiamishiki. Kama umeapa kwa minajiri ya kazi husika kwa kipindi husika kiapo hudumu mpaka pale muda wa kazi hiyo utakapokuwa umetenguliwa kwa mujibu wa sheria. Ndipo kiapo chaweza apishwa tena.
Balaza la mawaziri lipo kwa mujibu wa katiba. Mpaka hapo Rais kwa utashi wake atakapo amua kufanya mabadiliko ya kawaida ya baraza.
TLS mmechemsha. Mmetafsiri katiba kwa utashi wenu si kwa kutazama katiba na tafsiri yake. Huu si uchaguzi mpya. Ni awamu ya Serikali ile ile isipokuwa Makamu wa Rais kapanda cheo na kuwa Rais. Anaendeleza awamu ile ile kumalizia miaka mitano. Tafadhali TLS msipotoshe.
 
Back
Top Bottom