TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14

Kiapo cha VP siyo kiapo cha President, ni viapo viwili tofauti kabisa

Katiba ibara ya 51(3)(a) inatamka wazi kuwa Waziri mkuu ataendelea kuwa waziri mkuu mpaka pale raisi mteule atakapokula kiapo chake cha urais.

Sasa aliyekuwa rais mteule baada ya kifo cha rais aliyeko madarakani jana kala kiapo, hii maana yake nafasi ya PM iko wazi and hence baraza zima la mawaziri halipo kwa sababu za kikatiba zinazosema kuwa pasipokuwepo na waziri mkuu basi hakuna baraza la mawaziri
Nani kakudanganya kuwa Mama SSH alikuwa Rais Mteule baada ya Kifo cha Rais? Unajua maana ya Rais Mteule au President Elect?

SSH alikuwa ni Makamu wa Rais naBaada ya Kifo alikaimu Kiti Cha Urais, Kukaimu siyo kuwa Rais Mteule
 
TLS wanaipotosha jamii na ni kwa makusudi. Wanakuwa ni taasisi yenye kuitia aibu tasnia nzima ya sheria.

Mama Samia hana ulazima wa kuvunja baraza kwani mazingira sio yale ya baada ya uchaguzi kuwa umemalizika bali ni mazingira ya kifo na yeye kulazimika kuvaa viatu vya rais.

Hahitaji hata kuvunja baraza lake ni suala la kuangalia waziri gani anayeshindwa kutimiza malengo aliyopewa na kuchagua mwingine.

Wanasheria wetu wanawafanyia kazi watu fulani fulani wenye nia zao za miaka mingi tu.
 
Sifa mojawapo ya uhai wa baraza la mawaziri kufikia kikomo ni pale mtu mwingine anapoapishwa kuwa rais wa nchi including mwanasheria mkuu wa serikali. Hakika hatuna baraza la mawaziri wala mwanasheria mkuu wa serikali. Alitakiwa ateuwe mwanasheria mkuu the same day baada ya kiapo.
 
Tuwekeeni humu picha za viongozi wa TLS...wanatumiwa tu hawa na power mongers
 
Raisi mama Samia Suluhu anaenda kuongoza serikali ya awamu ya tano.Kwa nini haihojiwi kwa nini anairithi awamu ya tano?Nawauliza wenye hoja za mambo ya kurithi...

Raisi anaenda kulirithi bunge la awamu ya tano ambalo lilifunguliwa na Raisi aliyefariki.Watu wa mambo ya kurithi tunaomba mtwambie ni kwa nini huu urithi ukubaliwe na huo wa baraza la mawaziri uonekane una maana kubwa?

Kwenye tawala za mikoa na serikali za mitaa Raisi aliyetangulia ameteua wakuu wa mikoa,wilaya,wakurugenzi etc.Hawa wanaenda kurithiwa na Raisi mpya wa sasa.Kwa nini wabobezi wa mambo ya kurithi hawataji hili kuwa miongoni mwa mambo waliyoyabaini kutofaa kurithiwa?

Kuna wabunge wa viti maalumu wa aina zote, wapo hapo ama kwa kuzingatia idadi ya kura alizopata Rais aliyefariki au kwa uteuzi wa moja kwa moja kwenye nafasi kumi za Raisi aliyefariki .Hawa wanabakiaje kuwa wabunge wakati sababu ya wao kuwa wabunge inakuwa ni ya kurithi?Kwani Hili halihojiwi sambamba na hayo mengine yanayoonekana hayatakiwi kurithiwa?

Mama Samia mwenyewe,mpaka amekuwa VC ni kwa sababu alikuwa mgombea mwenza wa Raisi aliyefariki.Sasa kwa nini nchi imrithi VC ambaye sasa ni Raisi wakati uteuzi wake kwanza ulimuhusisha kwa kiasi kikubwa Raisi aliyetangulia.Kwa nini TLS wanakubali huu urithi na mwingine wanaupinga?

Hoja ya kurithi haina mashiko.Hii ni serikali ya awamu ya tano na Samia anaongoza serikali ya awamu ya tano.Tayari mtangulizi wake alishaisimika serikali ya awamu tano.Haina tena haja ya kuisimika upya serikali ya awamu ya tano.Haina haja ya kuapisha upya viongozi.Mambo yote ambayo TLS wanarejea yana apply katika mazingira ya kubadili serikali moja kwenda nyingine kwa njia ya uchaguzi mkuu. Kwa sasa bado tupo kwenye serikali ileile ya awamu ya tano ambayo tuliichagua mwaka jana...anauhuru wa kuendelea na watu walewale au kuwateua wengine.Halazimishwi...
 
Pale chama cha wanasheria kinaposhindwa kutafsiri Sheria. Kwaio kama baraza la mawaziri lilioachwa na raisi Magufuli ni batili vipi kuhusu mwanasheria mkuu wa serikali, jaji mkuu na viongozi wengine wa serikali walioteuliwa na mheshimiwa wakati wa uhai wake Je na wao wateuliwe wengine.
Wakati mwingine tunapata mashaka juu ya vyama hivi vya kisomi ni kweli vina manufaa kwa nchi kama mnashindwa kutafsiri hata jambo dogo hilo
 
Mkuu Safi sana, kwa wajibu mzuri uliyo tuofanya kutuonyesha, kimsingi saivi tufuate utaratubu wa kisheria kuliongoza Taifa.
Ninacho jifunza kwamba hizi nafasi ZA kuteuliwa Azina garatii sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo aliyesaini ile barua ya TLS jana alipewa shule na wasomi wabobezi wa sheria akaishia kuwa mdogo kama kidonge cha piliton.
 
Pale chama cha wanasheria kinaposhindwa kutafsiri Sheria. Kwaio kama baraza la mawaziri lilioachwa na raisi Magufuli ni batili vipi kuhusu mwanasheria mkuu wa serikali, jaji mkuu na viongozi wengine wa serikali walioteuliwa na mheshimiwa wakati wa uhai wake Je na wao wateuliwe wengine.
Wakati mwingine tunapata mashaka juu ya vyama hivi vya kisomi ni kweli vina manufaa kwa nchi kama mnashindwa kutafsiri hata jambo dogo hilo
Kwani raisi anashindwa kuteua wote wapya?
Kikubwa asiwe na papara,, lakini hata mi naona ateue wapya kwani hawa wengine watamsumbua kwakuwa hawakuwai kuwa mipango yake.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Sifa mojawapo ya uhai wa baraza la mawaziri kufikia kikomo ni pale mtu mwingine anapoapishwa kuwa rais wa nchi including mwanasheria mkuu wa serikali. Hakika hatuna baraza la mawaziri wala mwanasheria mkuu wa serikali. Alitakiwa ateuwe mwanasheria mkuu the same day baada ya kiapo.
Na wewe rudi uwani ukamalize mambo ya gesi ya tumboni huko kabla hujaingia kwenya umma!
 
Na wewe ni mmojawapo wa wanachama wa TLS waliosoma sheria lakini wasiojua kutafsiri na kuelewa sheria! Primary School Lawyers!!!
Mimi siyo mwanasheria lakini nafahamu huwezi kuwa na baraza la mawaziri bila Rais.

Saa na dakika aliyofariki Rais Magufuli na Baraza la mawaziri lilivunjika muda ule ule.

Huwezi kusema huyu mtu kafa lakini mkono wake utaendelea kuishi!
 
Back
Top Bottom