Kwaiyo.....?
Usipepese,nenda straight Kwenye pointi..! Kwani unataka kusemaje?
TLS (
Tanganyika Law Society) ni Chama cha Mawakili cha Tanzania Bara(ambayo ndiyo iliyokuwa Tanganyika). Hii ni taasisi iliyoanzishwa kisheria mnamo mwaka 1954 kwa sheria ya kikoloni ya Sheria ya Chama cha Mawakili wa Tanganyika, Sura Nambari 307 ya Sheria za Tanzania. Sheria hii iliundwa na Bunge la Kiingereza.Pamoja na mabadiliko ya hapa na pale yaliyofanywa kwenye Sheria hii, Mawakili wetu wamerithishwa Sheria hii-inawaongoza hadi leo. Ifahamike kuwa Chama hiki cha Mawakili hakihusishi na kila Mwanasheria. Uanachama wake umeelezwa vyema chini ya kifungu cha 6 cha sheria husika. Pia kuna Sheria ya Mawakili, Sura ya 341 ya Sheria za Tanzania, pamoja na sheria ndogo na kanuni zilizoundwa kwayo, ambazo nazo zatumika pamoja katika kuwaongoza Mawakili hapa Tanzania.
Chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Chama cha Mawakili, chama kimepewa malengo tisa. Haya ndiyo hapayobeba maana halisi ya uwepo wa taasisi hii, nguvu zake na zaidi sana umuhimu wake. Malengo manne kati ya hayo yanagusa mojakwamoja wadau wa sheria au umma kwa ujumla.
(1)Chama kina lengo la kuendeleza na kuimarisha viwango vya utendaji na mafunzo ya kada ya sheria.
(2) Kuwezesha upatikanaji wa uelewa wa kisheria kwa wanachama wake na wengineo.
(3) Kuisaidia serikali na mahakama kwenye masuala yote yahusuyo Sheria za Bunge, utawala na utendaji wa sheria Tanzania.
(4) Kuulinda na kuusaidia umma wa Tanzania katika masuala yote yahusuyo sheria.
Naunga mkono hoja kuwa TLS siyo mahali pa kufanya HARAKATI kama ambavyo Boniface Mwabukusi anavyotarajia. Tupa kule Mwabukusi