Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 778
- 1,592
Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society – TLS) kimetoa taarifa rasmi leo tarehe 30 Juni 2025 kuhusu tukio la kuuawa kwa mmoja wa wanachama wake, Wakili Joseph Masanja (Roll No. 7664), lililotokea tarehe 23 Desemba 2024 katika bwalo la Jeshi la Magereza, Babati – Manyara.
PIA SOMA: Tanganyika Law Society (TLS) yalaani vikali tukio la mauaji ya wakili Joseph Masanja. Yataka serikali iingilie kati
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchunguzi wa TLS kupitia kamati maalum iliyoundwa na Baraza la Uongozi, umebaini kuwa chanzo cha kifo cha Wakili Masanja ni kushambuliwa na askari wa Jeshi la Magereza katika eneo la bwalo hilo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Baraza la Uongozi la TLS liliwasilisha ripoti kamili kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, na kumjulisha kutoridhishwa kwao na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watuhumiwa. Kwa mujibu wa TLS, Kamishna Jenerali wa Magereza alieleza kuwa hatua za kiutawala tayari zilichukuliwa dhidi ya baadhi ya askari waliotajwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba Jeshi lake litaendelea kushirikiana na vyombo vya uchunguzi.
TLS pia imeeleza kuwa imeandika barua zaidi ya mara moja kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuwasilisha rasmi taarifa hiyo na kueleza kutoridhishwa kwake na namna Jeshi la Polisi lilivyoshughulikia uchunguzi wa tukio hilo. Hadi leo, TLS haijapokea majibu kutoka kwa Waziri husika.
Chama hicho kimesisitiza kuwa haki ya kuishi ni haki ya msingi ya kikatiba kwa kila mtu, na kwamba haki hiyo haiwezi kutolewa wala kuondolewa na chombo chochote cha dola. Kwa msingi huo, TLS imetoa wito kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha wote waliohusika na mauaji ya Wakili Masanja wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Baraza la Uongozi la TLS imesema itahakikisha kuwa itaendelea kufuatilia suala hili kwa karibu na halitasita kuchukua hatua za ziada za kisheria au kiidara kwa mujibu wa mamlaka yake ili kuhakikisha haki inatendeka.
Ikumbukwe pia kuwa tukio hili linakuja miezi michache tu baada ya tukio lingine lililoripotiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mnamo tarehe 01 Aprili 2025, kuhusu kuuawa kwa kijana Emmanuel Lucas mwenye umri wa miaka 18 katika Wilaya ya Serengeti, mkoa wa Mara, kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Magereza kutoka Gereza la Tabora B
LHRC ilieleza kuwa watuhumiwa walikamatwa, lakini hadi sasa bado kuna wasiwasi juu ya kasi na mwelekeo wa hatua za kisheria dhidi yao.
SOMA: LHRC: Tukio la Emmanuel Lucas kuuawa kwa kupigwa risasi na Askari Magereza (Mara), uchunguzi ufanyike na Haki ipatikane
Mfululizo wa matukio haya mawili, ambayo yote yanawahusisha askari wa Jeshi la Magereza, yanazidi kuibua mjadala mpana juu ya nafasi ya taasisi za usalama katika kuheshimu, kulinda na kudumisha haki ya kuishi, haki ya msingi ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeiweka wazi isiguswe.