TMA: Hali ya El Nino inaweza kuendelea hadi mwaka 2027

TMA: Hali ya El Nino inaweza kuendelea hadi mwaka 2027

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Hahaaa hii inaitwa force kingi hadi mtaelewa tu, nani kakaona kekundu, narudia tena ukiweka hapa na hapa unaliwa kekundu haka hapa. 😎😎😎😎
=============
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema hali ya El Niño inaweza kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2027, huku akiwataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu ailinde Tanzania.

Akizungumza na AyoTV, Dkt. Chang’a amesema hali hiyo inaendelea kuimarika na kuelekea katika hatua ya kukomaa, jambo linaloweza kusababisha athari mbalimbali zinazohusiana na hali ya hewa.

Amesisitiza kuwa Mamlaka inaendelea kushirikiana na Wataalamu wa Sekta mbalimbali pamoja na viongozi wa Serikali katika kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa na maelekezo sahihi ya kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza.

HUcMGIrXcAAKKkS.jpg
 
Watulie tu maana hawana tofauti na waganga wa kienyeji. Wameshatabiri inatosha, watulie tuone wanafaa kuaminika kwa kiwango gani. Mvua itanyesha , lakini sio kwa muda waliosema wao, wala sio lazima inyeshe kwa kiwango walichosema wao.
 
Tuendelee kusubiri mkuu, tuliambiwa tununue chakula cha kutosha mwezi wa September tusingeweza kutoka nje kimeisha usiache tena kununua cha disemba mkuu.
ni muhimu sana kuhakikisha tahadhari zote zinazingatiwa,
maana,
kwa uzoefu,
masaa mawili tu ya mvua za El nino yanatosha kusababisha uharibifu mkubwa na maafa makubwa na mabaya sana :NoGodNo:

​

 
dharau kama hizo zilikua chamtoto kipindi cha Nuhu gentleman, ila wenye kiburi walikiona cha moto in minutes :NoGodNo:
Hii inaitwa aibu utaona ww. Walisema mwisho wa September na mwanzoni mwa October. Hadi sasa utabiri hola. Mvua itanyesha, ila sio kama utabiri wa hao matapeli walivyotaka tuamini.
 
Back
Top Bottom