Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Mamlaka ya hali ya hewa kanda ya Magharibi- Tabora imesema hali ya ukavu iliyojitokeza kwa wiki mbili katika mkoa wa Tabora ni mabadiliko ya kawaida ya hali ya hewa ambayo hutokea katikati ya msimu wa masika. Akizungumza na CG FM Menena wa mamlaka ya hali ya hewa kanda ya Magharibi Tabora, Waziri Omary amesema hali ya ukavu imesababishwa na migandamizo mikubwa ya hewa kutoka kusini mwa dunia iliyokua ikizuia ukanda wa mvua katika maeneo ya Tabora. Waziri amesema mifumo hiyo inatarajiwa kudhoofika kidogo katika siku kumi zijazo kuanzia Desemba 11 na kwamba mvua zitanyesha katika mkoa wa Tabora. Aidha Waziri amesema kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa uliotolewa hivi karibuni msimu huu Tabora itapata mvua kwa wastani na chini ya wastani na kushuhudia vipindi virefu vya ukavu.