TMA siku zingine kama hamna uhakika na Hali ya Hewa bora mnyamaze tu kwani mmenichania Mkeka wangu

TMA siku zingine kama hamna uhakika na Hali ya Hewa bora mnyamaze tu kwani mmenichania Mkeka wangu

Nilibeti sehemu kutokana na Tabiri zenu juu ya Kimbunga Jobo kuwa Mkoa wote wa Dar es Salaam utazama Bahari ya Hindi na Watu wengi tutakufa cha Kushangaza Mimi nipo Hai hadi sasa hivi, Mkoa wa Dar es Salaam mkavu, Watu wanaenda Kuogelea Baharini na Anga la Dar es Salaam liko shwari tu.

TMA mmenikera mno na Kunikosesha Tsh 500,000/= kwa Utabiri wenu wa Bahati Nasibu ambao niliingia chaka na Kuwaamini. Labda Azam FC Usiku leo watanirejesha katika Furaha yangu pale watakaponifungia Wapuuzi fulani hivi wa Kariakoo.
Ndio maana unaitwa utabiri wa hali ya hewa mkuu,unapotabiri kuna mawili kupata au kukosa, wangekaa kimya mgelalamika, wametoa tahadhari napo mnalalamika,waulize wavuvi wa Kilwa walichokiona juzi.
 
Umeshaambiwa Tanganyika ilishawahi pigwa na cyclone mwaka 1952,Acha ubishi babu weye.
TMA wasanii tu,sijafikiria hata kidogo kama tutakumbwa na kimbunga ,jaribuni kusoma alama za nyakati na majira ya nukta ,TZ hatujawahi kupatwa na cyclon
 
Back
Top Bottom