Toa maoni yako juu ya pambano kati ya Mwakinyo dhidi ya Mfilipino

Toa maoni yako juu ya pambano kati ya Mwakinyo dhidi ya Mfilipino

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Jana usiku muda wa saa nne kulikuwa na pambano ya ngumi kati ya Mwakinyo na Mfilipino.

Mimi niliushuhudia pambano hilo tangu mwanzo mpaka mwisho. Kwa maoni yangu bila kupepesa macho Mwakinyo alishindwa kwa pointi.

Ushindi aliopewa kwa maoni yangu ni ushindi wa upendeleo. Toa na wewe maoni yako na wewe.
 
Tanga mnasifika kwa michezo yenu ile ila sio ya ngumi. Mwakinyo kama utaendelea na ngumi basi muombe sana Mungu ufikishe hata miaka 45 ukiwa hauna tatizo lolote maana una defence sana kuliko ku attack
 
Daaaa midia zote zilikua zinampa kiki sijaona la maana bora Twaha Kiduku yuko vizuri.
 
Kuna dogo mmoja wa Tabata anaitwa kinyogoli kama sikosei, huyu dogo kakosa wadhamini, Ila ni Bondia mzuri Sana.
Mtu angejitokeza kumdhamini hakika hatojutia.
 
hakupiga power punch hata moja licha ya mfilipino kumuachia uso muda wote. Mfilipino alistahili kushinda kwa point plus ile knockdown ila sikuzote ndio hivyo ushindi wa point huwa unaleta utata
 
Ngoja watetezi waje kumtetea hapa, yeye mwenyewe japo alitangazwa kushinda ila furaha yake hata robo haikufika.
 
Tanga mnasifika kwa michezo yenu ile ila sio ya ngumi.mwakinyo kama utaendelea na ngumi basi muombe sana Mungu ufikishe hata miaka 45 ukiwa hauna tatizo lolote maana una defence sana kuliko ku attack
...una defence$#@&?? sana
 
Bora uangalie mieleka kuliko ndondi. Matokeo yanategemea majaji wa pambano
 
Ukiwa mwenyeji wa mchezo unakuwa na goli moja mbele.... Au hamjui hilo?
 
Baada ya kurudia kuangalia hizi highlights nimejiridhisha pasi na shaka kwamba Mwakinyo ameshinda, kapiga point nyingi kuliko mpinzani wake japo kwa jicho la mtu asiyejua sheria za ngumi na how to score points ni ngumu kumuaminisha hilo kutokana na style aliyoitumia Mwakinyo (defensive), hiyo ni style ambayo Mayweather alikuwa akipenda kuitumia pindi alipokutana na bondia anayeattack sana japo watazamaji wengi hatuipendi (inapoteza ladha ya pambano), ni kama kwenye mpira timu inapopaki basi na kusubiri ushindi wa kuvizia, lakini mwisho wa siku ushindi ni ushindi. Hongera Mwakinyo japo nilitegemea utafanya zaidi ya hapo, huyo uliyepigana naye sio bondia wa kiwango cha juu na hatambuliki kabisa kwenye boxing world, kule boxrec ni no192 kwenye uzito wako duniani[emoji3][emoji3] ila umepigana naye kwa uoga sana, vipi ukikutana na kina Jermell Charlo utavuka hata round?[emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom