Tobo:
Ni uwazi uliopo kwenye kitu ambao umesababiswa na kupenyezwa kitu kingine kwenye kitu husika mf. mtu anapotoga sikio hutengeneza tobo kwenye sikio. Kwa ujumla tobo liko wazi pande zote. Pia tobo lazima liwe kuna kitu kilichosababisha kwa makusudi.
Tundu:
Ni tobo linalotokana na uchakavu wa kitu husika, kwa mfano nguo ikichakaa hupata matundu. Pia tundu huwa wazi pande zote.
Shimo:
Ni tobo linalotengenezwa kwenye kitu fulani lakini halitokezi upande wa pili. Hivyo basi shimo ni tobo au tundu lililoziba upande mmoja.
Kwa hiyo yote ni MATOBO

Hapo nimejaribu kueleza kwa jinsi nielewavyo mimi... Nashukuru kwa masahihisho.kama yanatofauti kwanini utumie neno tobo kwenye tafsiri..? tumia neno uwazi ingeleta maana zaid
Tobo:
Ni uwazi uliopo kwenye kitu ambao umesababiswa na kupenyezwa kitu kingine kwenye kitu husika mf. mtu anapotoga sikio hutengeneza tobo kwenye sikio. Kwa ujumla tobo liko wazi pande zote. Pia tobo lazima liwe kuna kitu kilichosababisha kwa makusudi.
Tundu:
Ni tobo linalotokana na uchakavu wa kitu husika, kwa mfano nguo ikichakaa hupata matundu. Pia tundu huwa wazi pande zote.
Shimo:
Ni tobo linalotengenezwa kwenye kitu fulani lakini halitokezi upande wa pili. Hivyo basi shimo ni tobo au tundu lililoziba upande mmoja.
umesema vizuri katika tobo na tundu; kimsingi tofauti kubwa kati ya tobo na tundu ni hiyo uliyoonesha tobo hutokea kwa kusababishwa na kitu kingine cha nje, tundu laweza kusababishwa na kitu cha nje au kitu cha asili (natural). Lakini vile vile tundu na tobo vinategemea ukubwa. Tundu ni tobo kubwa!! Hivyo kutegemea na matumizi huwezi kujikuta mtu anatumia maneno hayo kwa kubadilishana.
Hata hivyo, kwenye shimo umesema vizuri kidogo. Kwa ufupi, shimo ni sehemu ya ardhi iliyochimbwa kwa kina na kuachwa wazi bila kufukiwa. Ni kwa sababu hiyo shimo SIYO tundu wala tobo (kwa sababu tobo na tundu vinahitaji kuwa wazi upande wa pili ili vitu viweze kupenya).
Na vile vile shimo haliwezi kuwa kwenye nguo, gari, au kitu kingine isipokuwa kwenye ardhi.
Lakini vile vile tundu na tobo vinategemea ukubwa. Tundu ni tobo kubwa!! Hivyo kutegemea na matumizi huwezi kujikuta mtu anatumia maneno hayo kwa kubadilishana.
QUOTE]
Mkuu, sasa mbona mahala fulani kwenye kile kitabu cha Biblia wanasema ...ngamia kupenya katika tundu la sindano. Kama tundu ni tobo kubwa na tunajua sindano mpenyo wake ni mdogo kwa nini wasiseme ngamia kupenya katika tobo la sindano?
Jana jioni nilisikia Radio Clouds, wakiuliza tofauti baina ya maneno: tundu, tobo na shimo. Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kusikia majibu ya wasikilizaji yalikuwaje. Nimeona si vibaya nikauleta hapa mjadala huu hapa jamvini ili tupate michango zaidi.
Karibuni.
Tobo .. Tundu ..na shimo .. naona kama ni kitu kile kile
shimotundu, tobo na shimo.