Tobo, tundu au shimo?

Tobo, tundu au shimo?

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Posts
9,613
Reaction score
7,889
Jana jioni nilisikia Radio Clouds, wakiuliza tofauti baina ya maneno: tundu, tobo na shimo. Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kusikia majibu ya wasikilizaji yalikuwaje. Nimeona si vibaya nikauleta hapa mjadala huu hapa jamvini ili tupate michango zaidi.

Karibuni.
 
Tobo:
Ni uwazi uliopo kwenye kitu ambao umesababiswa na kupenyezwa kitu kingine kwenye kitu husika mf. mtu anapotoga sikio hutengeneza tobo kwenye sikio. Kwa ujumla tobo liko wazi pande zote. Pia tobo lazima liwe kuna kitu kilichosababisha kwa makusudi.

Tundu:
Ni tobo linalotokana na uchakavu wa kitu husika, kwa mfano nguo ikichakaa hupata matundu. Pia tundu huwa wazi pande zote.

Shimo:
Ni tobo linalotengenezwa kwenye kitu fulani lakini halitokezi upande wa pili. Hivyo basi shimo ni tobo au tundu lililoziba upande mmoja.
 
Kwa hiyo yote ni MATOBO
 
Hapo kwenye tundu nadhani ni zaidi ya uchakavu. Kwa mfano nimekuwa nikisikia wazungumzaji wa kiswahili wakisema " Usichezee shilingi katika tundu la choo".
 
Kwa mfano chandarua au nyavu, tunaweza kusema ina 'matundu' au ina 'matobo'?
 
Chandarua huwa na matobo, nakumbuka pale Forodhani kuna darasa la vidudu la matobotobo. Ila chandarua ikichanika hupata matundu.
 
Tobo:
Ni uwazi uliopo kwenye kitu ambao umesababiswa na kupenyezwa kitu kingine kwenye kitu husika mf. mtu anapotoga sikio hutengeneza tobo kwenye sikio. Kwa ujumla tobo liko wazi pande zote. Pia tobo lazima liwe kuna kitu kilichosababisha kwa makusudi.

Tundu:
Ni tobo linalotokana na uchakavu wa kitu husika, kwa mfano nguo ikichakaa hupata matundu. Pia tundu huwa wazi pande zote.

Shimo:
Ni tobo linalotengenezwa kwenye kitu fulani lakini halitokezi upande wa pili. Hivyo basi shimo ni tobo au tundu lililoziba upande mmoja.

kama yanatofauti kwanini utumie neno tobo kwenye tafsiri..? tumia neno uwazi ingeleta maana zaid
 
Hapo nimejaribu kueleza kwa jinsi nielewavyo mimi... Nashukuru kwa masahihisho.
 
Tobo .. Tundu ..na shimo .. naona kama ni kitu kile kile
 
Shimo ni uwazi uliotumbukia ardhini unapimika kwa urefu, upana na kina.

Tundu ni upenyo

Tobo hakuna neno kama hilo. Labda ni uwazi na tundu unaotokana na kutobolewa
 
Samahanini hii ni nje kidogo ya mada husika. Je nini tafsiri ya "Domestic Violence" kwa kiswahili? Inshallah nitashukuru nikipata kiswahili fasaha cha maneno hayo ya Kiingereza.
 
Tobo:
Ni uwazi uliopo kwenye kitu ambao umesababiswa na kupenyezwa kitu kingine kwenye kitu husika mf. mtu anapotoga sikio hutengeneza tobo kwenye sikio. Kwa ujumla tobo liko wazi pande zote. Pia tobo lazima liwe kuna kitu kilichosababisha kwa makusudi.

Tundu:
Ni tobo linalotokana na uchakavu wa kitu husika, kwa mfano nguo ikichakaa hupata matundu. Pia tundu huwa wazi pande zote.

Shimo:
Ni tobo linalotengenezwa kwenye kitu fulani lakini halitokezi upande wa pili. Hivyo basi shimo ni tobo au tundu lililoziba upande mmoja.

umesema vizuri katika tobo na tundu; kimsingi tofauti kubwa kati ya tobo na tundu ni hiyo uliyoonesha tobo hutokea kwa kusababishwa na kitu kingine cha nje, tundu laweza kusababishwa na kitu cha nje au kitu cha asili (natural). Lakini vile vile tundu na tobo vinategemea ukubwa. Tundu ni tobo kubwa!! Hivyo kutegemea na matumizi huwezi kujikuta mtu anatumia maneno hayo kwa kubadilishana.

Hata hivyo, kwenye shimo umesema vizuri kidogo. Kwa ufupi, shimo ni sehemu ya ardhi iliyochimbwa kwa kina na kuachwa wazi bila kufukiwa. Ni kwa sababu hiyo shimo SIYO tundu wala tobo (kwa sababu tobo na tundu vinahitaji kuwa wazi upande wa pili ili vitu viweze kupenya).

Na vile vile shimo haliwezi kuwa kwenye nguo, gari, au kitu kingine isipokuwa kwenye ardhi.
 
Hapo kidogo mnateleza, shimo si lazima liwe ardhini, shimo linaweza kutokea hata mwilini au kwenye mbao, ili mradi liwe limeziba upande mmoja, lina kipenyo na kina.

Tobo linakuwa na kipenyo pekee.

Tundu ni uwazi wenye kipenyo na kina ila pande zote ziko wazi, mfano ni tundu la pua, sikio, ushu$ nk.
 
Lakini vile vile tundu na tobo vinategemea ukubwa. Tundu ni tobo kubwa!! Hivyo kutegemea na matumizi huwezi kujikuta mtu anatumia maneno hayo kwa kubadilishana.
QUOTE]

Mkuu, sasa mbona mahala fulani kwenye kile kitabu cha Biblia wanasema ...ngamia kupenya katika tundu la sindano. Kama tundu ni tobo kubwa na tunajua sindano mpenyo wake ni mdogo kwa nini wasiseme ngamia kupenya katika tobo la sindano?
 
Jana jioni nilisikia Radio Clouds, wakiuliza tofauti baina ya maneno: tundu, tobo na shimo. Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kusikia majibu ya wasikilizaji yalikuwaje. Nimeona si vibaya nikauleta hapa mjadala huu hapa jamvini ili tupate michango zaidi.

Karibuni.

kiingereza tungesema synonyms. same meaning. kwa wale waliotazama prison break, T-BAG akiwa mdogo baba yake alimwambi, "give me 10 synonyms of the word destroy. dogo akaanza-kill, lynch, maim, mutilate, eradicate, crush, extinguish.... so unaona maana ya neno ilivyo na maneno mengi.
 
Tobo .. Tundu ..na shimo .. naona kama ni kitu kile kile

Hata mimi bado naona ni kitu kile kile. Kwa mfano nywele ni zile zile ila hubadilika jina kutokana na mahali zilipo kwa mfano

Kichwani zinaitwa nywele,
Kwenye kidevu zinaitwa ndevu na wengine wanaongezea kama za Osama
Na kule ndani zinaitwaje sijui ah nimesahau mnikumbushe
 
Back
Top Bottom