umesema vizuri katika tobo na tundu; kimsingi tofauti kubwa kati ya tobo na tundu ni hiyo uliyoonesha tobo hutokea kwa kusababishwa na kitu kingine cha nje, tundu laweza kusababishwa na kitu cha nje au kitu cha asili (natural). Lakini vile vile tundu na tobo vinategemea ukubwa. Tundu ni tobo kubwa!! Hivyo kutegemea na matumizi huwezi kujikuta mtu anatumia maneno hayo kwa kubadilishana.
Hata hivyo, kwenye shimo umesema vizuri kidogo. Kwa ufupi, shimo ni sehemu ya ardhi iliyochimbwa kwa kina na kuachwa wazi bila kufukiwa. Ni kwa sababu hiyo shimo SIYO tundu wala tobo (kwa sababu tobo na tundu vinahitaji kuwa wazi upande wa pili ili vitu viweze kupenya).
Na vile vile shimo haliwezi kuwa kwenye nguo, gari, au kitu kingine isipokuwa kwenye ardhi.