Duh! We jamaa mbona kila post ni issue za Vevo tu! Hivi uliambiwa what's so special huko Vevo?!
Jibu fupi ni kwamba, kwa mjanja mtafuta pesa hawezi kuwa Vevo kwa sababu mgawanyo wa mapato kupitia Vevo ni mkubwa ukilinganisha na YouTube!
Na hapa ningependa kusisitiza kwamba zile za akina Kiba zinazoonekana hadi Kariakoo ni Vevo Mirror Accounts ambazo zipo YouTube na sio Vevo!
Sio kwamba hawana ORIGINAL Vevo accounts bali kupitia original Vevo accounts walikuwa hawafikishi hata Views 1000 kwa sababu Vevo original ilikuwa inapatikana mbele peke yake! Kwa Afrika kama kuna nchi zilikuwa unaweza ku-access Vevo basi hata 5 hazifiki… na kati ya hizo hakuna hata moja kutoka East Africa!
Mond ni msaka pesa… hawezi kufanya jambo kwa sifa eti yupo Vevo wakati anajua akiwa YouTube anapiga pesa kubwa kuliko kupitia Vevo!
Na labda tu nikujuze kwamba hata hao Vevo wenyewe wameshafungasha virago vyao na focus yao yote ipo YouTube!
Kiba hata kama alitaka kutoka Vevo (na-assume na yeye angekuwa mjanja kama Mond) ingekuwa ngumu kwa sababu moja ya wamiliki wa Vevo ni Sony! Ingawaje hata UMG nao ni wamiliki wa Vevo, lakini mkataba wa Mond na Kiba kwa hizi multinational companies ipo tofauti!