Tofauti kati ya Crown Athlete, Majesta na Royal saloon

Tofauti kati ya Crown Athlete, Majesta na Royal saloon

Morg

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
1,301
Reaction score
1,788
Hizi ni Gari Aina tatu tofauti lkn mm nimeshindwa kuelewa utofauti wake labda naweza kutofautisha kwa muonekano lakini sio kuwa ubora ukubwa wa engine na uimara wa hizo Gari.

Mwenye uelewa naomba anijuze mm najichanga inshallah nivute athletes Crown ya cc 3000 ingawa nimewahi skia kuna Majesta lakini sijawahi kuijua kiundani naomba msaada wenu
 
Toyota Crown za hivi karibuni ni Executive (luxury) saloon kwa soko la Japan. Zimegawanyika katika makundi makuu wamili.
  1. Crown Midsize Executive saloon na
  2. Crown Full size Executive Saloon.
Toyota Crown Midsize Executive Saloon
Hizi ni four door saloon za size ya kati (ni kubwa kuliko kina Brevis, Altezza etc) Hapa ndio kuna Royal Saloon na Athlete. Hizi ni basically same car, zinashare karibu kila kitu, isipokuwa vitu vichache kulingana na zilivyokuwa tuned.
Royal Saloon - comfort oriented.​
So hapa utakuta suspension ni soft, side-walls za tairi ni nene kidogo ili linese vizuri, roundish bumpers and grille. Rangi za ndani za kuvutia vutia, kuna vitu kama wood trims etc​
Athlete - sporty oriented.
Suspension ni ngumu kidogo for better handling, hasa ukitumia ile sport button. Gari liko chini kidogo kuliko Royal Saloon, tairi ni low profile, bumpers na grille ziko aggressive kidogo, unaweza kuta ina ka spoiler ka kizusi, taa za nyuma ziko sporty kidogo na iko kama ina body kit vile. Rangi za ndani ni aggressive vile vile nyeusi nyeusi hivi, na seats zake hasa za mbele ni sporty, zina support ya mabega na mapaja, zinakushika vizuri hata gari likikata kona kwa kasi hauyumbi saana.​
Ila mwisho wa siku ni basically gari moja tu, engine option ni same kabisa.​
Toyota Crown Full Size Exective Saloon
Hii sasa tunasema ni Premium Executive Saloon. Yaani luxury ya luxury. Hii ina karibu vitu vyote vilivyo kwenye hao wadogo zake na vimeboreshwa zaidi, lakini pia ina vitu vyake vingine. Cha kwanza ni body size.

Hii ni bodi lake ni kubwa kulinganisha hao kina Athlete, meaning ukikaa ndani unakuwa comfortable zaidi, na engine zake ni kubwa pia. Kwa muonekano japo kwa mbali zinaendana na Athlete na Royal lakini ni tofauti kidogo. Luxury features nyingi zinakuwa standard kwenye hizi gari, tofauti na hizo za mwanzo.

Kama nikifananisha na Mercedes benz,
Crown Majesta = S Class
Crown Royal Saloon = E Class
Crown Athlete = E Class sport package.
 
Toyota Crown za hivi karibuni ni Executive (luxury) saloon kwa soko la Japan. Zimegawanyika katika makundi makuu wamili.
  1. Crown Midsize Executive saloon na
  2. Crown Full size Executive Saloon...
  1. Big up mkuu umenifungua macho kwa mbali naanza kuona mwangaza kwa kutofautisha hizo Gari Aina tatu kubwa hapo ni Majesta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toyota Crown za hivi karibuni ni Executive (luxury) saloon kwa soko la Japan. Zimegawanyika katika makundi makuu wamili.
  1. Crown Midsize Executive saloon na
  2. Crown Full size Executive Saloon...
  1. Bonge moja la analysis. Big up

Sent from my SM-A205F using Tapatalk
 
Vp haswa hapo kwenye ukubwa wa Engine zao ni tofauti au zinashabiana pamoja na Majesta

Sent using Jamii Forums mobile app
Majesta nyingi used zina engine ya V8 3UZ, ambayo ni cc4300. Ila kuna chache zenye V6 3GR ya cc3000. Hiyo 3GR ipo kwenye Althlete na Royal Saloon pia.

Kwa hizi Crown zilizozagaa siku hizi za kuanzia 2004 zina GR engines za V6 ambazo zinarange kuanzia cc2500 mpaka cc3500.
 
Back
Top Bottom