Toyota Crown za hivi karibuni ni Executive (luxury) saloon kwa soko la Japan. Zimegawanyika katika makundi makuu wamili.
- Crown Midsize Executive saloon na
- Crown Full size Executive Saloon.
Toyota Crown Midsize Executive Saloon
Hizi ni four door saloon za size ya kati (ni kubwa kuliko kina Brevis, Altezza etc) Hapa ndio kuna Royal Saloon na Athlete. Hizi ni basically same car, zinashare karibu kila kitu, isipokuwa vitu vichache kulingana na zilivyokuwa tuned.
Royal Saloon - comfort oriented.
So hapa utakuta suspension ni soft, side-walls za tairi ni nene kidogo ili linese vizuri, roundish bumpers and grille. Rangi za ndani za kuvutia vutia, kuna vitu kama wood trims etc
Athlete - sporty oriented.
Suspension ni ngumu kidogo for better handling, hasa ukitumia ile sport button. Gari liko chini kidogo kuliko Royal Saloon, tairi ni low profile, bumpers na grille ziko aggressive kidogo, unaweza kuta ina ka spoiler ka kizusi, taa za nyuma ziko sporty kidogo na iko kama ina body kit vile. Rangi za ndani ni aggressive vile vile nyeusi nyeusi hivi, na seats zake hasa za mbele ni sporty, zina support ya mabega na mapaja, zinakushika vizuri hata gari likikata kona kwa kasi hauyumbi saana.
Ila mwisho wa siku ni basically gari moja tu, engine option ni same kabisa.
Toyota Crown Full Size Exective Saloon
Hii sasa tunasema ni Premium Executive Saloon. Yaani luxury ya luxury. Hii ina karibu vitu vyote vilivyo kwenye hao wadogo zake na vimeboreshwa zaidi, lakini pia ina vitu vyake vingine. Cha kwanza ni body size.
Hii ni bodi lake ni kubwa kulinganisha hao kina Athlete, meaning ukikaa ndani unakuwa comfortable zaidi, na engine zake ni kubwa pia. Kwa muonekano japo kwa mbali zinaendana na Athlete na Royal lakini ni tofauti kidogo. Luxury features nyingi zinakuwa standard kwenye hizi gari, tofauti na hizo za mwanzo.
Kama nikifananisha na Mercedes benz,
Crown Majesta = S Class
Crown Royal Saloon = E Class
Crown Athlete = E Class sport package.