Tofauti kati ya malipo kabla na malipo baada kutoka makampuni ya simu

Tofauti kati ya malipo kabla na malipo baada kutoka makampuni ya simu

aceroty

Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
52
Reaction score
30
Habari,

Wengi wenu wiki zilizopita mlipokea message kutoka tigo kwamba mmechaguliwa kuingia kwenye kundi muhimu la wateja wa malipo ya baada. Na kwamba mtembelee maduka ya tigo muunganishwe au mpige namba zilizoandikwa kwenye hizo message. Si ndiyo?

Lengo kuu la hii post ni kuwaelezea maana ya hiyo message na kwamba, hakuna kitu cha bure ,kama wengi wa mliopiga simu mnavyofikiria.Ukiwa unataka kununua vocha ili upate huduma lazima utoe pesa yako mfukoni ili uweze kufanya mawasiliano. Hiyo ni inaitwa malipo kabla.

Malipo kabla ni huduma zote kama mini kabang,kabang,bundle za siku,wiki,na mwezi.Ni kwa watu ambao hawaoni shida kununua vocha Mara kwa Mara,watu ambao hawapigi simu nyingi kila siku. Kwa ufupi, mtu ambaye hana matumizi makubwa ya simu.

Lakini kuna jamii nyingine ya watu, mfano kampuni zinazotoa huduma za kukusanya madeni(wanasheria Mara nyingi wanatoa hizi huduma).Simu zao muda mwingi huwa ziko busy kuwapigia simu wateja kuwakumbusha kulipa madeni wanayodaiwa. Hawa watu simu zao lazima muda wote ziwe na vocha.

Wengi wao huwa wanaamua kujiunga na huduma ya malipo ya baada-kwamba unapewa bundle(kifurushi cha mawasiliano) chenye muda wa maongezi, meseji, na GB. Ambacho wewe unakilipia baada ya muda wa siku 30. Ni sawa na vifurushi vya kawaida sema unalipa baada ya mwezi au siku 30(inategemea na mwezi).

Lakini wakati unajiunga kwenye hii huduma(malipo baada) lazima uweke kianzio. Amana. Security deposit. Ni kama bondi hivi. Ni sawa na unapotaka kuchukua mkopo Benki. Lazima uweke bondi, ili utakaposhindwa kulipia madeni yako,ile bondi itatumika kama fidia. Sio bure.

Wewe kama sio mtumiaji mkubwa wa simu nikimaanisha kwamba, muda mwingi hulazimiki kwenda kupiga simu ili ufanye biashara, au labda wewe sio mtu unayesafiri mara nyingi kwenda mikoani kwenye sehemu ambazo hakuna maduka ya vocha,usipoteze muda wako kujiunga. Hii huduma ni kwa watu wenye matumizi MAKUBWA ya simu na wale ambao hawapendi KERO za kuishiwa na vocha Mara kwa Mara.

Lakini kama matumizi yako(ununuaji wako wa vocha) ni wa kawaida(tshs 1000-2000 kwa siku),usipoteze muda wako kujiunga. Tigopesa yako itakidhi mahitaji yako yote.

Naitwa Ian niko tigo. Kama una maswali yeyote kuhusiana na hii hizi huduma mbili. Usisite kuuliza.
 
Mimi nilitumiwa pia lakini sikujua tofauti kea kweli anayejua atujuze.
 
Malipo baada ni kama unapewa mkopo wa kupata huduma unakuja kulipa baadaye.
Ila huo mkopo unalimit ya kiwango. Huwezi kutumia forever.
Kama ulikuwa mtumiaji mzuri wa tigo lazima watakuwa na average matumizi ya huduma zao.
Kama kwa mwezi ulikuwa unatumia 10,000 basi utapewa the maximum amount ya 10,000.
 
aceroty kwahiyo ni mtu mwenye average ya matumizi ya sh ngapi kwa siku ni advisable kujiunga na huduma ya postpaid?
 
Last edited by a moderator:
Ndalama Mara nyingi huwa ni watu wenye matumizi kuanzia tshs 1000 na kuendelea.
Lakini inategemea na necha ya kazi yako. Kama kazi yako haikufanyi ununue sana vocha sio lazima ujiunge.
 
Back
Top Bottom