Tofauti kati ya mwanaume na mwanamke

Tofauti kati ya mwanaume na mwanamke

Lamzettttt

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2020
Posts
1,218
Reaction score
3,481
Mwana saikolojia wa kimarekani, Profesa Reek amechapisha matokeo ya utafiti wake juu ya mwanaume na mwanamke katika kitabu kikubwa. Anasema: Ulimwengu wa mwanaume ni tofauti kabisa na ule wa mwanamke. Ikiwa mwanamke hawezi kufikiri au kufanya mambo kama mwanaume, ni kwa sababu wanaishi katika dunia mbili tofauti.

Ameendelea kusema kuwa; “Kwa mujibu wa Agano la Kale, mwanaume na mwanamke wametokana na mwili mmoja. Hivyo ni kweli lakini ingawa wametokana na mwili mmoja, wana miili miwili tofauti, ambayo haifanani kabisa katika maumbile yake.

Hawana hisia za aina moja na hawaonyeshi mwitikio wa aina moja katika matukio na ajali mbali mbali. Wako kama sayari mbili zinazozunguka katika njia mbili tofauti. Wanaweza kuelewana na wanaweza kukamilishana, lakini sio kitu kimoja (sawa). Hii ndio sababu wanaweza kukaa pamoja, kupendana na wanaweza wasichokane.

Profesa Reek analinganisha roho ya mwanaume na mwanamke na anagundua tofauti nyingi. Anasema; “Inakinaisha (chosha) kwa mwanaume kukaa na mwanamke anayempenda muda wote. Lakini hakuna kitu kizuri kwa mwanamke kuwa karibu na mwanaume anayempenda.

Mwanaume mara zote anataka kubaki vile vile. Lakini mwanamke anataka kuamka akiwa tofauti na mpya kila siku.

Sentensi bora kabisa ambayo mwanaume anaweza kumwambia mwanamke ni kuwa ‘Mpenzi wangu, nakupenda.’ Sentensi nzuri kabisa ambayo mwanamke hupenda kumwambia mwanaume ni, ‘Naona fahari kuwa na wewe.’

Mwanaume aliyepata kuwa na wanawake wengi katika maisha yake huwavutia sana wanawake wengine. Lakini wanaume hawapendi wanawake waliopata kuwa na wanaume wengine huko nyuma.

Wanaume wanapokuwa wazee hukosa furaha kwa sababu wanapoteza kazi walizokuwa wanazitegemea. Wanawake wazee huwa na furaha kwa sababu, kwa mtazamo wao huwa wameweza kumiliki vitu bora kabisa ambavyo mtu anaweza kutamani, nyumba na wajukuu wachache.

Bahati nzuri kwa mwanaume ni kujipatia nafasi inayoheshimika katika jamii. Lakini kwa mwanamke bahati ni kuuteka moyo wa mwanaume na kubaki nao katika maisha yake yote.

Mwanaume mara zote hutaka kumbadilisha mwanamke wa chaguo lake ili afuate dini na utaifa wake.

Kwa mwanamke ni rahisi kubadilisha dini yake na uraia kwa ajili ya mwanaume aliyempenda ikiwa ni pamoja na kubadilisha ubini wake baada ya kuolewa.
 
Wanawake wanapenda sana kujichukulia points za bure kutoka kwa Wanaume kwa kauli kama ''Nyuma ya mwanaume yeyote aliyefanikiwa kuna mwanamke'' bila hata kuwa na mchango wa maana kwa huyo mwanaume.

Zamani hawa akina Delila walikuwa wanasema "TUNAWEZA TUKIWEZESHWA", na Muwezeshaji ni nani?jibu unalo. Hii kauli inasadifu kabisa Imani niliyonayo kuwa "NYUMA YA MAFANIKIO YA MWANAMKE KUNA MWANAUME" Ila baada ya sisi Wanaume kuwawezesha hawa wanawake, sasa wamekufa na kauli ya "TUNAWEZA HATA BILA KUWEZESHWA!" Hii ni kuonyesha dharau kwa Wanaume waliowawezesha miaka yote.

Kwa upande mwingine siwalaumu sana Wanawake. Hiyo kauli ya "Nyuma ya Mwanaume yeyote aliyefanikiwa kuna mwanamke'' haikuanzishwa na Wanawake wenyewe bali Wanaume fulani wenye ajenda za siri; wengi wao wakiwa 'Machoko' kutoka ughaibuni, na Wanaume wasomi uchwara walio brainwashed. Na mwisho wa siku wanaelekea kuipindua dunia kwa kuwadhoofisha Wanaume halisi, na nguvu za kuitawala dunia kuhamia kwa Mwanamke na Wanaume mashoga.
 
Back
Top Bottom