Tofauti ya msingi kati ya wanahabari na mashushushu ni katika baadhi ya mbinu za msingi za ukusanyaji habari, ambapo kwa asilimia kubwa mashushushu hukusanya habari kwa njia za siri ambapo mara nyingi wanahabari hukusanya habari kwa uwazi. Kingine kinachotofautisha fani hizo mbili ni matumizi yake, ambapo kwa mashushushu baada ya kupata habari husika huzichambua na kuwasilisha uchambuzi wao mahala husika, ilhali kwa wanahabari, wakishakusanya habari lengo kuu ni kuiweka wazi kwa wasomaji, wasikilizaji au watazamaji wa vyombo vyao vya habari.
Sasa, kwa vile wanahabari ni watu muhimu katika ukusanyaji wa habari, na kimsingi baadhi yao huwa "watoa habari‟ (sources) wa mashushushu, kuna nyakati mashushushu hulazimika kuwaambia ukweli wanahabari wanaowahitaji kwa ajili ya ushirikiano wa kikazi. Mfano halisi ni kama huu: shushushu anamzoea mwanahabari, na kutokana na mazoea hayo shushushu huyo anafanikiwa kupata habari mbalimbali.
Inafika mahali, shushushu anabaini kuwa mwanahabari huyo ni chanzo muhimu, au pengine chanzo chenye "access‟ na taarifa nyeti. Ikumbukwe kuwa ni rahisi kwa mtu kukusimulia habari mbalimbali akiamini kuwa anayepewa habari hizo anazisikiliza tu na hazitumii kwa mahitaji mengine. Kadhalika, katika mazingira ya kawaida tu, unapomsimulia mtu habari, kisha akaonyesha udadisi wa aina flani, waweza kuanza kumhisi tofauti.‟
Lakini pia yawezekana kuwa shushushu anahitaji taarifa flani muhimu ambayo njia rahisi au pekee ya kuipata ni kupitia kwa mwanahabari husika. Katika mazingira aya aina hiyo, inaweza kumlazimu shushushu "kujiweka wazi‟ kwa mwanahabari huyo, hususan kama taarifa inayohitajika ni ya dharura. Hata hivyo, kuwa karibu kimaongezi hata kama ni mara kwa mara hakumaanishi kuwa mwanahabari huyo ni mtu wa kuaminika. Kwahiyo, uamuzi wa kujiweka wazi kwake unaweza kuwa na madhara.
Shushushu anaweza kutumia mbinu mbalimbali kupima uaminifu wa mwanahabari (ambazo nitazielezea kwa kirefu katika sura zijazo) lakini mbinu hizo hazitoi uhakika wa asilimia 100 kuwa mwanahabari huyo ni mtu wa kuaminika. Tatizo jingine hapo ni kwamba kama ilivyo kwenye tafiti za "kuchunguza watu‟ (observational studies), binadamu wana tabia ya kufanya vitu "kiasili‟ wanapoamini kuwa hawachunguzwi.
Wakihisi tu kuwa wanachunguzwa, wanaweza "kuongeza chumvi‟ au kuficha ukweli. Kwahiyo, wakati mwanahabari anaweza kuwa na manufaa anapodhani kuwa anayefanya maongezi naye sio shushushu, kujua ukweli kwaweza kubadili tabia yake, na pengine kumkwepa kabisa. Na hapa ndipo hisia ya sita inapohitajika mno ili kutambua kuwa mbinu zilizotumika kumweka sawa‟ mwanahabari huyo zimefanikiwa au la, maana mtu kukubali kitu kwa mdomo hakumaanishi mara zote kuwa amekubali pia rohoni.
Na mtoa habari mzuri ni yule anayetoa taarifa za kweli bila „kuongeza chumvi,‟ kuficha vitu au kuelezea mawazo yake badala ya ukweli. Hisia ya sita ikimtuma shushushu kuwa mwanahabari huyo anaaminika, hapo inaweza kumpelekea kumwambia ukweli kuwa yeye anafanya kazi gani, na anahitaji kitu gani kutoka kwa mwanahabari huyo. Ni kama kucheza kamari vile, kwa sababu hata hiyo hisia ya sita sio kitu chenye uhakika wa asilimia 100.