Tofauti kati ya tabia za maskini na tajiri

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
NGUVU YA TABIA

Tofauti Kati Ya Tabia Za Maskini Na Tajiri.

Tajiri ni mtu ambaye yuko serious katika maswala ya utafutaji wa pesa na nidhamu ya pesa kwa ujumla.

~Tajiri Yuko serious katika utafutaji wa pesa, yani anatafufa pesa kwa nguvu zote mpaka muda wake wa kulala ni mdogo sana, muda mwingi anafanya kazi.
Kupenda usingizi ni moja ya tabia inayokemewa na Mungu kwenye maandiko, kwa sababu kulala sana ni ishara kwamba HUNA KAZI YA KUFANYA.

Maskini wengi hufanya kazi kwa muda mchache sana na wanatumia muda mwingi kulala au kufanya vitu visivyo na msingi wowote.
Hebu jitafakari kwa kutumia kanuni hii.. 8:8:8

Ukichukua masaa 24 ukagawa kwa 3 unapata masaa 8
Tuchukulie unaingia kazini saa 2 n kutoka saa 10, hapo umetumia masaa 8, Ukilala kitaalamu kabisa utalala masaa 8... swali linakuja masaa 8 yaliyobaki huwa unafanya nini?

Ukiwaza kwa undani zaidi utagundua kwamba Walioajiriwa wengi kama wanatumia masaa 8 kazini, na 8 kulala, Je masaa 8 huwa wanayapeleka wapi?

Wanafunzi wa vyuo mara nyingi ukikuta vipindi vimebana siku hiyo watatumia masaa 8 vipindi vinne vyenye masaa 2
Kama mwanafunzi huyu wa chuo atalala masaa 8, mana yake anabakiwa na masaa 8 YA KUPOTEZA.

Tafiti zinaonesha kwamba hayo masaa 8, ndiyo yanayotengeneza MASKINI WENGI.
Na hayo masaa ndiyo yanatengeneza MATAJIRI WENGI.

Waajiriwa waliofunguka akili, hutumia muda wao wa ziada kufanya kazi mbadala za kuwaongezea KIPATO. Mfano: Kuna mtu namfahamu alikuwa anaingiza Millioni 30M Kila mwezi ndani ya kampuni ya fulani kwa kufanya network marketing, na bado ameajiriwa na anatumia muda wake wa ziada.

Nawafahamu wanafunzi wengi wa vyuo wanaofanya kazi za kujiongezea kipato kwa muda wao wa ziada.
Leo katika uzi huu, jiulize je huwa unatumiaje masaa yako 8?....

Tukutane kwenye nyuzi zingine, Tukiendelea kipengele cha nidhamu ya fedha.
----------------------------------
 
Nyie motivation speaker mnatufanya watu tuwe na hangover za usingizi,mi ukinikamata usingizi nauchapa hasa .Kutafuta kupo ,nmeshashiba nitafute Hela nipeleke wapi badala ya kulala,na uhakika wa kupiga k vant big ninao.
 
Kitabu Cha rich dady na poor dady kina madini muhimu Sana kwanini matajiri wanakuwa matajiri na masikini kuwa masikini.

Hongera Sana mkuu kwa uzi huu umejaa madini ya almasi
 
Watu wengi uwa tunakosea pale tunapoleta vitu vya kufikirika kwenye uhalisia.
Sisemi kwamba vitu haviwezekani ila inabidi tuwe tunawaza kwa uhalisia sana.
 
Maneno tu hayo,kuna tajiri maarufu hapa bongo akiingia ofisini anafanya kazi mpaka saa sita,akishakula analala mpaka saa kumi jioni,akitoka kazini jioni anaenda kula mirungi mpaka asubuhi.
Au labda kama huu uzi wako unazitaka zile m-tano za Mello hapo sawa.
 
Hahahah dah noma kweli aisee
Nyie motivation speaker mnatufanya watu tuwe na hangover za usingizi,mi ukinikamata usingizi nauchapa hasa .Kutafuta kupo ,nmeshashiba nitafute Hela nipeleke wapi badala ya kulala,na uhakika wa kupiga k vant big ninao.
 
Hahhaha M5 za mello ni jukwa lingine siyo hili mkuu
 
Unachanganya
Kuna umaskini wa akili,na utajiri wa akili.

Hayo mengine ni matokeo kwenye kimaisha.

Hata tukupe pesa vipi kama una umaskini wa akili uwezi fika .
Hapo kweli mkuu
 
Yaani nilale masaa machache kisa utajiri! Tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…