Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Ninaelewa kuwa Kodi ni malipo yasiyo ya hiari ambayo raia analipa serikalini kutokana ama na mapato au kutokana na mali anayomiliki. Kuna Kodi ya Ardhi, Kodi ya Mapato, Kodi ya Gari na kadhali.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuja neno jipya linalotwa Tozo, ambayo nayo ni malipo yasiyo ya hiarai ambayo raia analipa serikalini kwa kutumia huduma fulani na ambayo ni juu ya zile gharama ambazo anatakiwa alipe ili kupata huduma hiyo kwa mfano huduma za kibenki au huduma za miamala ya simu.
Je, kuna haja gani ya kutumia neno jipya la Tozo ilihali ni malipo ya lazima yanayofanywa na raia serikalini kama KodiI? Kuna faida gani ya kutofautisha Kodi na Tozo?