Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upande mmoja kumsifia Ali Kiba na upande mwingine ni kumponda Diamond... nayo inatoka kwa mpendwa wa Ali Kiba! Kama nilivyosema awali... kwenu nyinyi Ali Kiba akisema yeye ndie kam-release Diamond ni sawa lakini Diamond akisema yupo tayari kumsadiai Ali Kiba, inageuka nongwa... aaaaaaaargh! Kiba wakati akihojiwa na Sporah alisema "mimi nipo tayari kum-support mwanamuziki yeyote yule...!" Hebu ondoa hiyo kum-support kisha weka neno la kiswahili!
ndo mjue kwamba diamond na kiba hawana bifu..tatizo ni nyie mashabik mav..kutupigia kelele humu jf..
Mkuu Matola unasumbuliwa na mahaba... kwani Ali K kumtaja Diamond ndio nini? Inawezekana kamtaja kinafiki tu, moja lakini mbili ni huku kwa social networks na media ndiko tunachochea bifu! Binafsi sina nongwa na Kiba ila nina nongwa na wale wanaomchukia mtu bila sababu za msingi!! Kuna mmoja kaja na kali ya mwaka kwamba eti Diamond anawavua sana chu*pi mademu.... aaaaaargh, wanaovuliwa wenyewe halalamiki anakuja kulalamika mtu mwingine.... nyie watu vipi???!!!! Afadhali basi angekuwa anavua watoto wa shule tungesema anawarubuni lakini mimama mijitu mizima imevuliwa chu*pi na wanaume kibao wengine sawa na baba zao, akawavua Dangote inakuwa nongwa.... eheeee!
Mashabiki wa ndomo safari hii inabidi muwe wapole sana.
Manake hakuna jinsi msanii wenu ameshachuja machoni pa watanzania na watanzania ninavyowafahamu wakikuangusha wamekuangusha.
Kilichotokea pale leaders hata davido mwenyewe haamini macho yake.
hahahaaaaaaa Nyasamaki umenichekesha sana LOLNdugu sema baadhi ya Nyie Watanzania usiisemee Mioyo yetu Babu we ! Jina lako linaonyesha wewe ni Mtanzania wa aina gani ? Pia wewe Mbinafsi na Unakijiba cha roho toka 2012 hata hujawapa wenzio Like !
Mpwa ni jinai kumshabikia Kiba? Refer to my thread Banana Zoro rudi kwenye muziki tumechoka na kelele za Diamond.
Yes ni kweli tumechoka backup anayopewa leo Ally Kiba msije mkajidanganya labda na si wote ni wapenzi wa wabana pua hapana, bali tumechoshwa na kelele za pro Diamond na kwenye vita vya haki ushindi ni lazima wapenda huwa tukiamuwa kusimama mtu mkiwa huwa tunaonesha nguvu ya umma ni nini.
Ukitaka kunisoma vyema waulize
Clouds tuliwafanya nini pake walipohujumu tamasha la Sugu na Vinega na concert ya Jide pale nyumbani Lounge.
Sasa wapenda haki kupiga kelele na diamond hatuwezi bali ni kutuma clear msg kwamba heshima ni kitu cha bure
Mimi kiasilia ni mpenzi wa hiphop na Mr 2 Sugu ndio ninayemuelewa anachoimba kama alivyokuwa 2pac Shakur na wapili ni hawa Nako 2 Nako sijui ndio wanajiita weusi sasa hivi, hiyo style ya mziki niupendao na musiki wa dance live band.
Matola bhana... shida yote hiyo ya nini wakati wewe ushabukua? Yaani nirudi shule kujifunza maana ya hayo maneno tu? Kwanini usiweke hapa... hilo moja nimeshindwa kulifahamu bado unaniongezea zigo lingine? Kuna hili lingine nimemsikia Kiba akimweleza Sporah "mimi ndie nimem-release Diamond....!" Ni nini hiyo maana yake kwa kiswahili kisicho na kizungu ndani yake?Hebu rudi shule kwanza ukajifunze maana ya maneno haya Help, support na save.
Wewe huwa humpendi Diamond........ huwezi kusema vile anaimba ni kelele
Ungesema BANANA RUDI KWENYE MUZIKI, hakukuwa na haja ya kumuweka Diamond
hao unaowasema ni kama wanafunzi wenye miandiko mizuri ila hawana akili darasani
halafu unasema "tumechoka' umechoka wewe na nani Mpwa?????????
We mtoto mi ndo maana nakupendaga... mineno yako mifuuupi lakini mibusara kibao... hukasiriki wala ku-panic... niliona cku moja tu ukiwa umekuja juu; nikajua watakuwa wamevuka mipaka tu hao! Si nikatamani kununua kesi... akili za kiutu uzima zikaniambia "come down...!"Wewe huwa humpendi Diamond........ huwezi kusema vile anaimba ni kelele
Ungesema BANANA RUDI KWENYE MUZIKI, hakukuwa na haja ya kumuweka Diamond
hao unaowasema ni kama wanafunzi wenye miandiko mizuri ila hawana akili darasani
halafu unasema "tumechoka' umechoka wewe na nani Mpwa?????????
Matola bhana... shida yote hiyo ya nini wakati wewe ushabukua? Yaani nirudi shule kujifunza maana ya hayo maneno tu? Kwanini usiweke hapa... hilo moja nimeshindwa kulifahamu bado unaniongezea zigo lingine? Kuna hili lingine nimemsikia Kiba akimweleza Sporah "mimi ndie nimem-release Diamond....!" Ni nini hiyo maana yake kwa kiswahili kisicho na kizungu ndani yake?
Mpwa kazi ya kumpenda Diamond ni ya Wema Sepetu siyo ya kwangu.
Unapouliza nimechoka mimi nani ina maana hukuona kilichotokea kwenye Fiesta? Ule ni umma uliochoshwa.
We mtoto mi ndo maana nakupendaga... mineno yako mifuuupi lakini mibusara kibao... hukasiriki wala ku-panic... niliona cku moja tu ukiwa umekuja juu; nikajua watakuwa wamevuka mipaka tu hao! Si nikatamani kununua kesi... akili za kiutu uzima zikaniambia "come down...!"
Unajua hoja ya wivu inakuja pale mnaposhindwa kutoa sababu za kwanini mpo against hiki au kile... mbaya zaidi, issue hapa sio kuzomewa issue ni vile watu wanavyoonekana kufurahia au kutamani wamuone Diamond anakwisha... sasa kama sio chuki ni nini? Hao aliowasema Mrigariga ni kwamba walizomea lakini si kwamba walikuwa wanataani wamuone Witney anapotea... tofautisha! Swahiba mkuu wa Ali Kiba humu jamvini, Somji Juma aliwahi kusema, nanukuu "tena afadhali Diamond alipokosa hizo tuzo manake tusingelala...!" Somji njoo huku ukanushe! Sasa kauli kama hizi zinaonesha wazi kwamba watu wanatawaliwa na chuki na si kingine! Mtu anayemuombea mwenzake mabaya hakuna lingine linalomsumbua zaidi ya khusuda!
Haya mambo ya band bhana mi cjui kabisa ingawaje nakubali kwamba kwenye band ndiko waliko wanamuziki na huku kwingine ni waimbaji... mimi mwenyewe nishawahi kuimba na ku-rap... c unajua sie tuliobalehe in early 1990's ilikuwa ni lazima u-rap kwanza kama ukitaka kung'oa totoz za kishua!!?? Leo hii tukirudi back 1970's kiteknolojia, wala sioni nani atabaki kwenye game... labda Banana!unajuwa kulikuwa na kabend ka msimu kanaitwa TOT Plus kaliota mapembe kwa sababu walikuwa wamemchukuwa Banza stone wakaota mapembe wakataka mpambano na Twanga Pepeta.
Kilichotokea ilikuwa ni aibu kwa TOT Plus na Banza Stone na kuanzia hapo Ally Choki aliijuwa rasmi thamani yake.
Naona na hawa wabana puwa ili tukate mzizi wa fitina inabidi waandaliwe mpambano wa nani zaidi ili tumalize haya mapovu.