Unajua hoja ya wivu inakuja pale mnaposhindwa kutoa sababu za kwanini mpo against hiki au kile... mbaya zaidi, issue hapa sio kuzomewa issue ni vile watu wanavyoonekana kufurahia au kutamani wamuone Diamond anakwisha... sasa kama sio chuki ni nini? Hao aliowasema
Mrigariga ni kwamba walizomea lakini si kwamba walikuwa wanataani wamuone Witney anapotea... tofautisha! Swahiba mkuu wa Ali Kiba humu jamvini,
Somji Juma aliwahi kusema, nanukuu "tena afadhali Diamond alipokosa hizo tuzo manake tusingelala...!" Somji njoo huku ukanushe! Sasa kauli kama hizi zinaonesha wazi kwamba watu wanatawaliwa na chuki na si kingine! Mtu anayemuombea mwenzake mabaya hakuna lingine linalomsumbua zaidi ya khusuda!
NasDaz kauli ya Somji Juma hatuwezi kuitumia kama conclusion ya mada iliyopo mezani. Kwa sababu yeye ni mmoja kati ya wengi wanaopaza sauti zao hapa jamvini.
Mashabiki wanapo zomea ni njia mojawapo ya kuonyesha kuna kitu fulani ambacho hakipo sawa. Au kimekuwa ni kinyume na matarajio yao.
Ndiyo maana wasanii wakomavu huwa wanatoa press release ktk matukio kama haya. Especially kuomba msamaha mashabiki wao. Kwa kuwa wanajua watakuwa wameumia nafsi zao. Na wakati mwingine tukio linaloongelewa halihusiani kabisa na fani ya msanii.
Nitakupa mifano kama mitatu. R Kelly alipofikishwa mahakamani kwa kosa la kujihusisha kimapenzi na Aaliyha. Mashabiki wake walichukia sana kwa sababu Aaliyha alikuwa bado hajatimiza umri wa miaka 18!! Hili halihusiani kabisa na muziki. Ni maisha yake private. Lakini watu walisusa kununua kazi zake na hata albamu zake alizotoa baada ya tukio lile hazikupata support kubwa. Kifupi zili flop!!!
Tiger Woods aliopokamatwa ugoni na mkewe. Kitu cha kwanza aliomba msamaha mashabiki wake kwa kuwakosea. Hujiulizi hili lina uhusiano gani na golf? Kilichofuata pale ni nini? Tiger Woods alishuka toka No.1 mpaka sijui No.7 na imemchukua miaka kadhaa kurudi tena ktk top positions.
John Terry (Captain wa Chelsea na England Football Team) alipokumbwa na kashfa ya kutembea na mke wa mchezaji mwenzake. Mashabiki sio tu walimzomea kila alipoingia uwanjani bali walipaza sauti ya kuwa hafai kuongoza kikosi cha England kwa sababu ya maadili. Na kweli alivuliwa ukepteni akapewa Rio Ferdinand!!!
Michael Jackson alipokumbwa na kashfa ya kunajisi mtoto mdogo. Ndo ulikuwa mwanzo wa anguko lake la kimuziki. Ule msongo aliopata ulimpelekea kujiingiza ktk matumizi ya madawa hadi kifo chake. Management yake ilikanusha lakini pia iliwaomba msamaha mashabiki kwa kuwaumiza mioyo yao!!!
Nimetoa mifano hiyo michache kwa nini?? Ninataka kukuonyesha kuwa watu wakishakukupenda sana. Inabidi uangalie muenendo wa wa maisha yako. Ndiyo maisha ni yako lakini yana athari kubwa kwa wapenzi wako. Especially matamshi yako. Ukiwa Star wewe ni watu. So chochote utakachofanya kinyume na matarajio yao, ujiandae...
Ndo maana halisi ya kioo cha jamii. Watu wanakuangalia wewe kama mfano. Sasa kama wewe ni mjivuni/malaya,mlevi n.k sidhani wewe uta fit hiyo role ya kioo cha jamii.
Kuna mifano mingi hapa nyumbani nikupe mmojawapo. Unamkumbuka yule dada wa African Stars mnenguaji mahiri ambaye watu walimpenda sana? Alipoanza vituko vya madawa ya kulevya na picha za utupu sijui. Watu walimchukia na wala hawakuwa na huruma naye. Angeweza kusema ni chuki kwa mafanikio aliyoyapata ktk fani.Kwa nini?!! Kwa sababu ukishapendwa na watu wanategemea wewe utajiheshimu au you behave in a certain way. Kwani kuna watoto wao wanakuangalia wewe kama kioo...
Nadhani umenielewa na wengine wote wenye mtazamo kama wako. Tusikimbilie majibu mepesi kama wivu,husda,chuki nk.